DOKEZO Polisi tunaomba msaada. Tunahisi dada yetu ameuawa na mume wake ambaye ni Polisi, inasikitisha sana!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Binti yangu sitaki aolewe na hao watu wengi wao ni zero brain.
Wanajiona nchi hii ni mali ya mama zao.
 
Unaleta umbea Tu usiokuwa na mashiko.

Vifo vyote vyenye utata ndugu hawawezi kuruhusu kuzikwa mpaka ifanyike postmortem itakayoshirikisha Wana ndugu.

Marehemu she is dead and buried, unataka JF tuanze kujadili umbea na illusions?

Pambana na January usirudishe muda nyuma.
Hilda Newton

@HildaNewton21
·
2h

INAHUZUNISHA Askari wa
@tanpol
pale ufundi Dar, Josephat Aron, alimuua mkewe ila akasingizia alikuwa anaumwa, familia iliomba mwili wa marehemu uchunguzwe ili wajue chanzo cha kifo akatishia kuwauwaHii ni siku ya mazishi, ndugu walikuwa wanasisitiza binti yao asizikwe bila.
UKIFUATILIA TWITTER KWA HUYO HILDNEWTON21 KUNA VIDEO.
YWEZEKANA MADAI YAO YAKAWA YA KWELI.
 

Mbona mlikubali kunyamazia sintofahamu hii kwa muda wote huo? Ndugu yenu kafariki toka January 2023 na amezikwa ndio mnakuja kuushtua umma leo January 2024?

Familia nzima ndio mmetishwa na kunyanyaswa na Koplo? Koplo kabisa? Kweli? Hii familia imenitia simanzi.

Na kwa maelezo yenuyenut tu ya upande mmoja, inaonesha kuna kitu nyuma ya pazia juu ya kifo cha ndugu yenu.

Watanzania msiidharau mitandao ya kijamii, inasaidia kidogo katika nchi hizi ambazo mtu akipata kacheo kadogo tu anaanza kupanda juu ya vichwa vya wengine. Kelele za mitandaoni zinasaidia sana.
 
Mngewahi mahakamani kuzuia mwili.

Mungu atawalipia kisasa msiogope.

Rumi 12:19​

Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
 
Kutoka kwenye mtandao wa X, Akaunti ya Lisa Ildephonce (@LIldephoce)

“Tarehe 23/1/2023 Tulipata msiba wa dada angu alifariki katika mazingira ya kutatanisha aliolewa na kijana anaitwa Josephat Aron ambaye ni Police pale Ufundi (Kilwa Road) cheo Kopro

Kifo chake kilitupa mashaka kutokana na mgogoro wa ndoa waliokuwa nao na sababu hiyo hatujui mpaka leo hii dada yetu amekufa na tatizo gani kwani baada ya kufariki kijana huyo alitunyima kupima mwili pamoja na taarifa za hosptal juu ya kilichomuua dada yetu

Imefika hatua familia ya marehemu wanatishiwa na hawana amani

Siku ya kumuaga marehemu mdogo wa kike wa marehemu alinyimwa kwenda kumstiri dada yake badala yake alienda mume na kaka ake kumstiri dada yetu ndugu tulichukizwa na iko kitendo cha shemeji mtu kwenda kumstiri marehemu tukaingilia kati hilo mwisho wa siku wakamruhusu mdogo mtu kuingia lakini haikusaidia kwani mume na shemeji wa marehemu walikuwa wameshatangulia

Baada ya kuruhusiwa mdogo wa marehemu na mama zake wadogo wawili walinyimwa gloves kwaajili ya kumvalisha marehemu na walikuta dada yetu amezuriwa maeneo mengi

Ndugu wa mwanamke waliokuwa hospitalini walikatazwa kumuona mgonjwa aliyekuwa anaingia ni Josephat na ndugu yake anaitwa Mwinyi walimuamisha mochwari kutoka hospital alipofia (Hindu Mandal)na kumpeleka mochwari ya kazini kwao anapofanyia kazi ndugu wasiweze kupima mwili

View attachment 2860643
View attachment 2860644

View attachment 2860794
Hii ni siku ya msiba [Video] baada ya ndugu wa mwanamke kutaka mwili ukafanyiwe vipimo ili kujua ndugu yetu kwa nini amepatwa na kifo ila tukaletewa mapolisi waliokuja na mwili wakashika na mabunduki kutaka kuyafwatua baada ya wananchi waliokuja msibani kuwaambia tuuweni tu kama hamtaki tumpime ndugu yetu. Kijana huyo Josephat Aron akaamuru Polisi waingie ndani ya gari. Tulimzika ndugu yetu chini ya ulinzi wa mapolisi waliotoka Dar es Salaam kuja Rombo na mwili tukiwa na majonzi”
Uchunguzi ufanyike.....Taarifa za Hospitali ziwekwe Mahakamani
 
Unaleta umbea Tu usiokuwa na mashiko.

Vifo vyote vyenye utata ndugu hawawezi kuruhusu kuzikwa mpaka ifanyike postmortem itakayoshirikisha Wana ndugu.

Marehemu she is dead and buried, unataka JF tuanze kujadili umbea na illusions?

Pambana na January usirudishe muda nyuma.
Comment ya Kipumbavu toka mwaka huu uanze
 
Jeshi la polisi limejaa uozo mtupu, wahusika wanapita huku, kuna walakini hapa
 
Ndo hivyo. Ila kwenye case kama hiyo ndugu wa mke wangesimama vizuri uchunguzi ungefanyika, inaonyesha ni waoga
Labda ana nguvu kubwa nyuma yake ndo mana wanamuogopa.
Halafu hii issue sio mara ya kwanza.nliwahi ona mke kauliwa na mtoto wa wifi Ake familia ya mume ikawakataza hata kuaga mwili.nlishangaa!
 
Bila shaka jamaa alikua anatoa kibunda cha haja kwenye hiyo familia.

Yaani ndgu hmna say juu ya mwili wa ndgu yenu?

Je alikua hana baba, hana mama, hakuna watu wazima kwenye ukoo wenu.
Suala kama hilo polisi hulindana sana ila mngesimama kidete walau mngetendewa haki.
 
Wanaume wasiohudhuria vikao ndio wanatujengea picha mbaya,tushasema pisi Kali ni za kunyandua na kuacha ila mchizi kaweka ndani anategemea nn!!
 
Koplo koplo koplo ndio wakukutisha. Angekuwa officer kabisa ingekuwaje?
Hahahaa...

A corporal is usually appointed as a section commander, and is in charge of 7–14 soldiers of private rank. They are assisted by a second-in-command, usually a lance-corporal or senior private.
 
Hivi Tanzania hakuna sheria inayolazimisha kila kifo kipate cheti kutoka kwenye mamlaka kudhihirisha chanzo cha kufariki kabla ya maziko? Kama hali iko hivyo basi ni hatari sana.
Tanzania mwenye sheria ni yule aliyekuwa na pesa/mamlaka na yule anaemjua mwenye pesa/mamlaka.
 
Huko Rombo kuna nini? Mauaji kila kukicha.

Kijana Mtenga wa Israel, Beatrice wa Lukas Tarimo na sasa huyu wa Polisi na bado mambo ni mengi
 
Back
Top Bottom