Polisi: Lissu hatoki

Polisi: Lissu hatoki

Huyo Mkondya nae ni wa kupuuzwa tu! Unaona Sifa kuvunja Sheria? Sheria inahitaji nini katika hili?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu, ni vizuri ukatufafanulia polisi wamevunja wapi sheria ya kumshikilia Tundu Lissu na kumzuia kuonana na mawakili wake?

Kama sheria ipo ya kuruhusu au kutoruhusu kuonana kwa anaeshikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi, naomba uweke hapa tuichambue.
 
Lissu akipimwa mkojo si ajabu ukakutwa na chembechembe nyingi sana za Mihadarati, japo yupo ndani siku ya nne sasa. Combination ya Police wa TZ plus maagizo kutoka juu ni hatari zaidi ya Messi, Neymar na Luis Suarez.
 
Shule za kata zimedumaza akili yako hivyo huwezi kuelewa kile ambacho anakipigania lissu. MAZUZU kama wewe ndiyo mtaji mkubwa wa MACCM maana hamtambui haki zenu katika nchi huru hata chembe.

Uanasheria wake anautumia vibaya
Why?
Anachopigania ni nin haswa?
Kutumia lugha za kukejeli kwa taasisi ya raisi kisa tu anajua akienda mahamamani atashinda kesi.
Ni sawa na wew kwenye familia kuwe na watoto wanakudharau kwa kukukebehi kisa tu hujawazaa wew.
TUNDU ANATAFUTA VERY CHEAP POPULARITY, ni bora nchi ya kidikteta kuliko uhuru uliopitiliza
You have a right to speech but I no guarantee to you right after speech.
Chuma up to 2025

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule za kata zimedumaza akili yako hivyo huwezi kuelewa kile ambacho anakipigania lissu. MAZUZU kama wewe ndiyo mtaji mkubwa wa MACCM maana hamtambui haki zenu katika nchi huru hata chembe.
Mnapigania
UJINGA, UKABILA, UKANDA
Hamna hoja ya msingi kwa sasa
Ndio maana mzee wa gia za angan lockedman mpaka sasa na chama chake hawajatoa tamko la chama
Poor low thinkers.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: nao
Na huyu anapigania nini mpumbavu mkubwa wewe!?



Mnapigania
UJINGA, UKABILA, UKANDA
Hamna hoja ya msingi kwa sasa
Ndio maana mzee wa gia za angan lockedman mpaka sasa na chama chake hawajatoa tamko la chama
Poor low thinkers.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkondya hana vyeti sasa anatumia mgongo wa Lisu kusaka chcheo cha kamanda wa kanda maalum ya Dsm atambue kuwa ICC inakuja na yy atakuwa mshitakiwa namba moja.
Huu wimbo wa ICC aliuimba sana Mbatia kabla na baada kidogo ya uchaguzi mkuu lakini akanyamaza,naona nawe umeamua kumpokea mkuu.Endelea uimbisha ukichoka kuna mtu atakupokea....kawimbo katamu.
 
POLISI: LISSU HATOKI

KIBATALA-NA-KARUME-300x208.jpg


KUNA kila dalili zinazoonyesha kuwa Jeshi la Polisi limeamua kushughulika na mwenendo wa kauli za mwanasiasa machachari, Tundu Lissu.

Hilo linaweza kuthibitishwa na kauli iliyotolewa jana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lucas Mkondya, kuwa Jeshi hilo halitamwachia huru Lissu hadi pale upelelezi utakapokamilika na kisha kumfikisha mahakamani.

Si hilo tu, hatua ya Jeshi hilo kuwazuia mawakili wa Lissu, Peter Kibatala na Fatma Karume kuonana naye inaweza kuwa na tafsiri hiyo hiyo.

Watu ambao wamekuwa wakifuatilia matukio ya Lissu kukamatwa na Jeshi la Polisi wanasema wanashangaa hatua ya sasa kutokana na huko nyuma Lissu kuruhusiwa kuonana na wanasheria wake na kupata dhamana kwa wakati.

Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, anashikiliwa tangu juzi na jeshi hilo kwa tuhuma za uchochezi.

Alikamatwa juzi saa 12 jioni katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa anaelekea Kigali, nchini Rwanda, kuhudhuria mkutano wa Wanasheria wa Afrika Mashariki ulioanza jana.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mkondya, ambaye alikiri kuendelea kumshikilia Lissu, alisisitiza kwamba hawawezi kumwachia hadi upelelezi utakapokamilika, kwa kile alichodai kuwa amekuwa akitumia kichaka cha ubunge kuchochea uhalifu.

“Bado tunaendelea kumhoji, hatumwachii, anatumia kichaka cha ubunge kuchochea uhalifu, tunaye na tukikamilisha upelelezi ni mahakamani,” alisema Mkondya.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata jana jioni na kuthibitishwa na wakili wake, Kibatala, zilieleza kuwa Lissu amekataa kutoa maelezo yoyote hadi atakapofikishwa mahakamani na zaidi amekataa kuchukuliwa vipimo vya mkojo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pamoja na hilo, inaelezwa kuwa, Polisi pia walifika nyumbani kwa Lissu na kisha kufanya upekuzi.

Taarifa hizo za Lissu kupekuliwa na kisha kufikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali zilithibitishwa pia na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

“Ni kweli wamempeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kutaka kumpima mkojo, lakini alivyofika Lissu alikataa akawaambia mashtaka waliyomfungulia hayahusiani na yeye kupimwa mkojo.

“Baada ya hapo walikwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi na walianzia maktaba yake, mpaka sasa (12:41 jioni) wanaendelea na huo ukaguzi wao na hatujui ni nini wanatafuta hasa,” alisema Mrema.

Awali akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo Kikuu cha Polisi, baada ya kukataliwa kumuona Lissu, Wakili wake, Fatma Karume, alisema mwanasiasa huyo anashikiliwa kwa kosa la uchochezi.

“Alipokamatwa jana (juzi) alinipigia simu, akaniomba nimwakilishe, na nilimwambia niko tayari, nimekuja jana usiku (juzi) na polisi walimhoji akasema hana masuala yoyote ya kujibu, lakini usiku wa jana wamemcharge (wamemshitaki) kwenye saa 1:30 hivi kwa kosa la uchochezi,” alisema Fatma.

Fatma alisema suala la uchochezi ni la kisheria zaidi na kwamba inapaswa ionekane nani kachochewa na kwa kufanya jambo gani la uhalifu.

Alisema Lissu alimpigia simu akimwomba kumwakilisha kwa kuwa pia ni rafiki yake na kwamba jana alifika kituoni hapo saa 4:45 za asubuhi, lakini alizuiwa getini kuingia kwa madai kuwa ni amri kutoka juu.

“Jana (juzi) tulivyouliza hawajasema kamchochea nani, na kamchochea kufanya jambo gani, kwa hivyo wametumia tu lile kosa la kuchochea kama kisingizio tu,” alisema Fatma.

Alisema baada ya dakika 45 za yeye kukaa nje, Wakili Peter Kibatala alionana na Ofisa mmoja wa Polisi ambaye alizungumza naye na baadaye waliruhusiwa kuingia ndani.

“Baada ya kama dakika 45 hivi, wakili mwenzangu Kibatala alizungumza na Ofisa mmoja wa Polisi, nafikiri jina lake Kingai, akatoa ruhusa tuingie. “Nilimuuliza Kingai, Lissu mtampeleka mahakamani lini, jana (juzi) msham-charge (mshitaki) kimebaki kumpeleka mahakamani, akaniambia hawajui watampeleka lini, na bado wanaendelea na upelelezi,” alisema Fatma.

Fatma alisema anavyofahamu ni kwamba upelelezi unafanyika na kupata ushahidi ndipo mhusika anakamatwa na kupelekwa mahakamani.

“Hivyo Polisi kama wanadhani wanaweza kumkamata mtu bila ya upelelezi kukamilika ili waendelee kumweka mahabusu, hiyo haiwezekani,” alisema Fatma.

Alisema kutokana na hilo, waliamua kulishtaki Jeshi la Polisi Mahakama Kuu wakiomba Lissu afikishwe mahakamani.

“Leo ndio tumepeleka nyaraka za kuiomba mahakama ili Lissu kama ana kesi waikabidhi mahakama na si kumweka selo ya polisi mpaka wao watakapotimiza uchunguzi wao,” alisema Fatma.

Alisema kutokana na jana kuzuiwa kuonana na mteja wake, alimwomba Ofisa huyo wa Polisi amruhusu afike kituoni hapo leo, lakini alimjibu kuwa hajui.

Hali nje ya Kituo

MTANZANIA Jumamosi ambalo lilifika kituoni hapo saa nne asubuhi, lilizuiwa kuingia ndani kwa madai kuwa hakukuwa na taarifa za mkutano wa waandishi na kwamba kama kuna lolote lisubiri pembeni litajulishwa.

Licha ya waandishi kuruhusiwa kukaa pembeni, saa 5: 58 alifika Ofisa mmoja wa Polisi na kuwataka kuondoka eneo hilo.

“Mna appointment? Hapa sio sehemu ya mkusanyiko. Nendeni mkatafute habari huko sehemu maalum au mpigieni Inspekta,” alisema Ofisa huyo.

Hata hivyo, waandishi ambao muda huo walikuwa wamejibanza katika eneo la stesheni karibu kabisa na kituo hicho waligoma kuondoka na kuwataka polisi kuwaacha kwani nao wako kazini.

Baada ya mabishano hayo ya muda, polisi hao waliondoka kurudi kituoni hapo.

Mbali na waandishi, pia walikuwapo baadhi ya wafuasi wa Chadema, ambao nao waliondolewa eneo hilo, huku wengine wakizuiwa kuingia ndani.

Nje ya geti la kituo hicho, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi ambao walionekana kuzunguka wakiwa na silaha.

Wakati hayo yakitokea Kituo Kikuu cha Polisi, maofisa wa jeshi hilo walikuwa wakihaha kukamilisha upelelezi dhidi ya Lissu.

Katika kukamilisha upelelezi huo, kwa nyakati tofauti jana, maofisa hao waliwahoji waandishi wawili wa habari walioripoti mkutano wa Lissu uliofanyika Jumatatu ya wiki hii.

Waandishi waliohojiwa ni pamoja na mwandishi wa gazeti hili, Aziza Masoud na Ibrahim Yamola wa gazeti la Tanzania Daima.

Maofisa hao wawili wanaume na mmoja mwanamke, wakijitambulisha kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, walifika kuwahoji waandishi hao kila mmoja katika kituo chake cha kazi.

Taarifa ilizonazo gazeti hili, Yamola alihojiwa saa 3:00 asubuhi, wakati Aziza akihojiwa saa 5:30 asubuhi katika ofisi za gazeti hili, zilizopo Sinza Kijiweni.

Mahojiano kati ya maofisa hao na Aziza yalichukua takribani saa moja.

Akizungumza na gazeti hili, Yamola alisema: “Mimi walinipigia simu, awali walitaka niende Central (Kituo Kikuu cha Polisi), lakini niliwaambia sitaweza, ndipo walipoahidi kunifuata leo (jana) kwa kunihoji”.

Alisema katika mahojiano yake, ambayo yalichukua takribani dakika 55, walikuwa wakiuliza kuhusu habari aliyoiandika na alipata fursa ya kutolea ufafanuzi kile nilichokiandika tu.

“Kuna muda walikuwa wanataka kutoka nje ya kitu nilichoandika, lakini nilisimamia kilichomo kwenye gazeti kulingana na misingi ya uandishi, ilifika muda nililazimika kushika gazeti ili niwasomee kilichomo,” alisema Yamola.

Wakati huo huo, Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata na kuendelea kumshikilia Rais wa chama hicho, Lissu, kwa makosa ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa jana na Makamu Rais wa TLS, Godwin Ngwilimi, ilieleza mawakili walipojaribu kuhoji Lissu aliwachochea akina nani, na alifanya kosa hilo wapi, wakajibiwa kuwa uchunguzi bado unaendelea.

“Kwa maoni na mtazamo wetu, Lissu anashikiliwa kwa kitendo cha kutoa maoni yake binafsi, basi kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria za nchi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa katika vipindi tofauti, hususan Ibara ya 18 ya Katiba hiyo, kwani inatoa na kulinda uhuru wa kutoa maoni kwa watu wote bila kujali kabila, rangi na imani.

“Haki hii ya msingi pia inatamkwa bayana katika mikataba mbalimbali ya Kimataifa ambayo Tanzania imetia saini na kuiridhia, kama vile Tamko la Kimataifa la Haki za Kijamii na Kisiasa la mwaka 1966 (International Covenant on Civil and Political Rights) na Tamko la Afrika la Haki za Binadamu la mwaka 1986 (The African Charter on Human and Peoples’ Rights),” alisema Ngwilimi.

Alisema TLS inalaani na kupinga vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanapotoa maoni yao binafsi kuhusu masuala mbalimbali ya nchi yao, kwamba ni vema nchi ikaendeleza utamaduni wa kuvumilia maoni tofauti na kukosoana bila kupigana.

Lissu alikamatwa ikiwa ni siku moja baada ya Jumatano kung’ang’ania ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, ili kukwepa kukamatwa na polisi.

Lissu anadaiwa kukamatwa kutokana na kauli alizozitoa katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya hivi karibuni, ambapo alizungumza mambo mbalimbali kuhusu serikali na viongozi wake.

Kubenea na Polisi

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, kutokana na malalamiko aliyoyatoa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Tunamtafuta popote alipo Tanzania hii na ajitokeze yeye mwenyewe, hii Tanzania ni ndogo, aje atupe ushirikiano tumalizane na hili,” alisema Mkondya.

Hivi karibuni, Kubenea alifanya mkutano na vyombo vya habari kama Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF iliyo chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif na kutangaza operesheni ya kumwondoa Profesa Lipumba katika ofisi za chama hicho, zilizopo Buguruni.
Baada ya Kubenea kutangaza operesheni hiyo, siku mbili baadaye, Profesa Lipumba alikwenda kutoa malalamiko polisi.

Mbali na hilo la Kubenea, taarifa nyingine zinadai kuwa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, jana alihojiwa kwa mara nyingine na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, taarifa hizi zilishindwa kuthibitishwa na Kaimu Kamanda Mkondya, huku simu ya Sheikh Khalifa ikiita pasipo majibu.

Bado haijajulikana iwapo Sheikh Khalifa alikuwa bado mikononi mwa polisi au aliachiwa.

Hivi karibuni Sheikh Khalifa alizungumza na kuunga mkono hotuba ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, juu ya masheikh wa uamsho pamoja na matamshi mengine aliyotoa juu ya Waislamu nchini.


Chanzo: Mtanzania
Kinamdamalum kushikiliwa nahisi wanasheria wamejipanga na hilo
 
Haya yanayompata TL ni kwasababu wanasheria wa nchi hii wako usingizini,kama wangekuwa kama TL haya tunayo yashuhudia yasingekuwepo.
Wangekuwa na moyo kama wa TL kupinga na kupaza sauti pale katiba ya nchi inapo kanyagwa,huyu jamaa asingekuwa huko aliko,yuko huko maana yupo mwenyewe tu.
Nawaomba wanasheria wote waliangalie hii na kama wataona vema akina TL wawepo wengi.
 
Wanazidi kuumbuka " if you look at magufuli speech kila siku anaongea same shit if u look at polisi kila siku wanafanya same vioja if u look at those idiots supporting huu ukandamizaji njaa zinaongezeka" tanzania is a loosing nation na i pray for the worse ili akili ziwakae sawa.
You pray for the worse, brace yourself for disappointment, the worse will fall on you. Magu yupo hadi 2025+
 
Madhara ya kua na serikali inayo ongozwa na watu wenye akili ndogo ndio haya.
 
Kubenea hana janja ya kujificha porini ... hana pa kwenda kwa hiyo Tanzania ni ndogo kwake tofauti na wale jamaa

Kwa hiyo kwa wale jamaa Tanzania ni kubwa, kwa Kubenea Tanzania ni ndogo.

Chizi wewe kuruta. Kazi yenu kuonea unarmed, defenseless citizens.

Huu si wakati wa Polisi wa Tanzania kumtakia mtu "Tanzania ni ndogo jitokeze mwenyewe..." atakuwa polisi chizi. Last week Kamanda Sirro amesema kuna ungoverned areas ambazo polisi hawawezi kufika, ni mbali sana, watu tujilinde wenyewe.

Sasa ghafla utachimbaje mkwara kwamba Tanzania ni ndogo Kubenea jitokeze wenyewe?

Imagine polisi unatamka mbele ya umma kwamba kuna sehemu za nchi hii ni mbali sana. Mbali kutoka wapi, Central Police? Nyinyi polisi wazima kweli nyinyi?

Magufuli, hebu fukuza hawa makamanda waliosema Pwani ni mbali sana polisi hawana jinsi ya kufika, achana na Kubenea.
 
We jinga kweli, unaona kubenea ni jambazi kwamba kumtafuta itakuwa shida? Atakimbilia wapi na kwa kosa lipi la kumfanya asionekana, we hujaelewa nilichokiandika ndo maana umekuja na mihemko ya kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kwa wale jamaa Tanzania ni kubwa, kwa Kubenea Tanzania ni ndogo.

Chizi wewe kuruta. Kazi yenu kuonea unarmed, defenseless citizens.

Huu si wakati wa Polisi wa Tanzania kumtakia mtu "Tanzania ni ndogo jitokeze mwenyewe..." atakuwa polisi chizi. Last week Kamanda Sirro amesema kuna ungoverned areas ambazo polisi hawawezi kufika, ni mbali sana, watu tujilinde wenyewe.

Sasa ghafla utachimbaje mkwara kwamba Tanzania ni ndogo ma suspect wajitokeze wenyewe?

Imagine polisi unatamka mbele ya umma kwamba kuna sehemu za nchi hii ni mbali sana. Mbali kutoka wapi, Central Police? Nyinyi polisi wazima kweli nyinyi?

Magufuli, hebu fukuza hawa makamanda waliosema Pwani ni mbali sana polisi hawana jinsi ya kufika.
We jinga kweli, unaona kubenea ni jambazi kwamba kumtafuta itakuwa shida? Atakimbilia wapi na kwa kosa lipi la kumfanya asionekana, we hujaelewa nilichokiandika ndo maana umekuja na mihemko ya kisiasa.
 
We jinga kweli, unaona kubenea ni jambazi kwamba kumtafuta itakuwa shida? Atakimbilia wapi na kwa kosa lipi la kumfanya asionekana, we hujaelewa nilichokiandika ndo maana umekuja na mihemko ya kisiasa.

Kama hamuwezi kuwapata majahili wa Kibiti basi msichimbe mkwara kwa Kubenea kwamba Tanzania ni ndogo. Kwa hiyo kwa Kubenea kumpata rahisi, kwa majambazi ndio hamuwezi? Nakwambia chizi wewe!
 
Back
Top Bottom