Polisi: Lissu hatoki

Polisi: Lissu hatoki

Katika Wilaya maskini na zenye wananchi wanaoishi maisha magumu , Ikungi iko mstari wa mbele. Kama Lisu angetumia juhudi na nguvu zake hizi , angaliweza kupunguza adha ya maisha ya wananchi hawa maskini wa kutupwa. Ili ujue akili ya Lisu, kawaulize wananchi wake jambo gani amechangia kuboresha maisha yao miaka 10 hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
kikwete alikuwa Rais hakumaliza umasikini jimboni wala wilayani kwake hivyo hivyo kwa mkapa hata huyo magufuli hakumaliza umasikini chato wakati akiwa waziri, kazi ya Mbunge si kugawa pesa kwa wana jimbo na unasikini wa jimbo umeletwa na CCM kwa kutopeleka Bajeti ya maendeleo jimboni kwa Lisu makusudi wakimkomoa, na kaa ukijua Lisu ni kiongozi wa chama kitaifa lazima apaze Sauti kulalamikia Udikteta wenu pasipo kujali kuwa CCM mnamkomoa kwa kutopeleka maendeleo jimboni kwake.
 
Anaudhi sana huyo mtu na ilikuwa inaonekana polisi wanamuogopa. Huoni Lema amekuwa mstaarabu!

Mtu anaejua ni anajua tu, Lissu alishaga mdhalilishaga SACP wa polisi mahakamani. Ngoja kesi iungurume uuone moto wa Lissu.
 
Angalau yeye kajaribu kuliko yule anayekimbia kukutana na viongozi wq kimataifa kisa lugha akisingizia kubana matumizi wakati huo huo anatuma mwakilishi anayejua kiingereza

fent ford
Huna lolote zaidi ya utumwa wa kifikra. Nenda kamfariji huyo Lisu huko mahabusu na Kiingereza chake.
 
Leo ni jumapili Padre katusisitizia leo kuwapenda maadui zetu na kuwaombea .Nakushangaa kufurahia mateso ya mwenzio hata kama ni adui yako.Sijui hicho kiguest house chako Bariadi ndicho kimefanya upoteze utu au ni ukabila. Mbona ulikuwa mtu wa maana hapo awali?!!.
Lisu anasota selo.
 
Katika Wilaya maskini na zenye wananchi wanaoishi maisha magumu , Ikungi iko mstari wa mbele. Kama Lisu angetumia juhudi na nguvu zake hizi , angaliweza kupunguza adha ya maisha ya wananchi hawa maskini wa kutupwa. Ili ujue akili ya Lisu, kawaulize wananchi wake jambo gani amechangia kuboresha maisha yao miaka 10 hii?

Sent using Jamii Forums mobile app

Dah! Akili za Lumumba ni shida tupu aisee,
Kwa hiyo Lissu anatakiwa awaletee hao Ikungi maisha bora?
 
POLISI: LISSU HATOKI

KIBATALA-NA-KARUME-300x208.jpg

KUNA kila dalili zinazoonyesha kuwa Jeshi la Polisi limeamua kushughulika na mwenendo wa kauli za mwanasiasa machachari, Tundu Lissu.

Hilo linaweza kuthibitishwa na kauli iliyotolewa jana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lucas Mkondya, kuwa Jeshi hilo halitamwachia huru Lissu hadi pale upelelezi utakapokamilika na kisha kumfikisha mahakamani.

Si hilo tu, hatua ya Jeshi hilo kuwazuia mawakili wa Lissu, Peter Kibatala na Fatma Karume kuonana naye inaweza kuwa na tafsiri hiyo hiyo.

Watu ambao wamekuwa wakifuatilia matukio ya Lissu kukamatwa na Jeshi la Polisi wanasema wanashangaa hatua ya sasa kutokana na huko nyuma Lissu kuruhusiwa kuonana na wanasheria wake na kupata dhamana kwa wakati.

Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, anashikiliwa tangu juzi na jeshi hilo kwa tuhuma za uchochezi.

Alikamatwa juzi saa 12 jioni katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa anaelekea Kigali, nchini Rwanda, kuhudhuria mkutano wa Wanasheria wa Afrika Mashariki ulioanza jana.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mkondya, ambaye alikiri kuendelea kumshikilia Lissu, alisisitiza kwamba hawawezi kumwachia hadi upelelezi utakapokamilika, kwa kile alichodai kuwa amekuwa akitumia kichaka cha ubunge kuchochea uhalifu.

“Bado tunaendelea kumhoji, hatumwachii, anatumia kichaka cha ubunge kuchochea uhalifu, tunaye na tukikamilisha upelelezi ni mahakamani,” alisema Mkondya.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata jana jioni na kuthibitishwa na wakili wake, Kibatala, zilieleza kuwa Lissu amekataa kutoa maelezo yoyote hadi atakapofikishwa mahakamani na zaidi amekataa kuchukuliwa vipimo vya mkojo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pamoja na hilo, inaelezwa kuwa, Polisi pia walifika nyumbani kwa Lissu na kisha kufanya upekuzi.

Taarifa hizo za Lissu kupekuliwa na kisha kufikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali zilithibitishwa pia na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

“Ni kweli wamempeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kutaka kumpima mkojo, lakini alivyofika Lissu alikataa akawaambia mashtaka waliyomfungulia hayahusiani na yeye kupimwa mkojo.

“Baada ya hapo walikwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi na walianzia maktaba yake, mpaka sasa (12:41 jioni) wanaendelea na huo ukaguzi wao na hatujui ni nini wanatafuta hasa,” alisema Mrema.

Awali akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo Kikuu cha Polisi, baada ya kukataliwa kumuona Lissu, Wakili wake, Fatma Karume, alisema mwanasiasa huyo anashikiliwa kwa kosa la uchochezi.

“Alipokamatwa jana (juzi) alinipigia simu, akaniomba nimwakilishe, na nilimwambia niko tayari, nimekuja jana usiku (juzi) na polisi walimhoji akasema hana masuala yoyote ya kujibu, lakini usiku wa jana wamemcharge (wamemshitaki) kwenye saa 1:30 hivi kwa kosa la uchochezi,” alisema Fatma.

Fatma alisema suala la uchochezi ni la kisheria zaidi na kwamba inapaswa ionekane nani kachochewa na kwa kufanya jambo gani la uhalifu.

Alisema Lissu alimpigia simu akimwomba kumwakilisha kwa kuwa pia ni rafiki yake na kwamba jana alifika kituoni hapo saa 4:45 za asubuhi, lakini alizuiwa getini kuingia kwa madai kuwa ni amri kutoka juu.

“Jana (juzi) tulivyouliza hawajasema kamchochea nani, na kamchochea kufanya jambo gani, kwa hivyo wametumia tu lile kosa la kuchochea kama kisingizio tu,” alisema Fatma.

Alisema baada ya dakika 45 za yeye kukaa nje, Wakili Peter Kibatala alionana na Ofisa mmoja wa Polisi ambaye alizungumza naye na baadaye waliruhusiwa kuingia ndani.

“Baada ya kama dakika 45 hivi, wakili mwenzangu Kibatala alizungumza na Ofisa mmoja wa Polisi, nafikiri jina lake Kingai, akatoa ruhusa tuingie. “Nilimuuliza Kingai, Lissu mtampeleka mahakamani lini, jana (juzi) msham-charge (mshitaki) kimebaki kumpeleka mahakamani, akaniambia hawajui watampeleka lini, na bado wanaendelea na upelelezi,” alisema Fatma.

Fatma alisema anavyofahamu ni kwamba upelelezi unafanyika na kupata ushahidi ndipo mhusika anakamatwa na kupelekwa mahakamani.

“Hivyo Polisi kama wanadhani wanaweza kumkamata mtu bila ya upelelezi kukamilika ili waendelee kumweka mahabusu, hiyo haiwezekani,” alisema Fatma.

Alisema kutokana na hilo, waliamua kulishtaki Jeshi la Polisi Mahakama Kuu wakiomba Lissu afikishwe mahakamani.

“Leo ndio tumepeleka nyaraka za kuiomba mahakama ili Lissu kama ana kesi waikabidhi mahakama na si kumweka selo ya polisi mpaka wao watakapotimiza uchunguzi wao,” alisema Fatma.

Alisema kutokana na jana kuzuiwa kuonana na mteja wake, alimwomba Ofisa huyo wa Polisi amruhusu afike kituoni hapo leo, lakini alimjibu kuwa hajui.

Hali nje ya Kituo

MTANZANIA Jumamosi ambalo lilifika kituoni hapo saa nne asubuhi, lilizuiwa kuingia ndani kwa madai kuwa hakukuwa na taarifa za mkutano wa waandishi na kwamba kama kuna lolote lisubiri pembeni litajulishwa.

Licha ya waandishi kuruhusiwa kukaa pembeni, saa 5: 58 alifika Ofisa mmoja wa Polisi na kuwataka kuondoka eneo hilo.

“Mna appointment? Hapa sio sehemu ya mkusanyiko. Nendeni mkatafute habari huko sehemu maalum au mpigieni Inspekta,” alisema Ofisa huyo.

Hata hivyo, waandishi ambao muda huo walikuwa wamejibanza katika eneo la stesheni karibu kabisa na kituo hicho waligoma kuondoka na kuwataka polisi kuwaacha kwani nao wako kazini.

Baada ya mabishano hayo ya muda, polisi hao waliondoka kurudi kituoni hapo.

Mbali na waandishi, pia walikuwapo baadhi ya wafuasi wa Chadema, ambao nao waliondolewa eneo hilo, huku wengine wakizuiwa kuingia ndani.

Nje ya geti la kituo hicho, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi ambao walionekana kuzunguka wakiwa na silaha.

Wakati hayo yakitokea Kituo Kikuu cha Polisi, maofisa wa jeshi hilo walikuwa wakihaha kukamilisha upelelezi dhidi ya Lissu.

Katika kukamilisha upelelezi huo, kwa nyakati tofauti jana, maofisa hao waliwahoji waandishi wawili wa habari walioripoti mkutano wa Lissu uliofanyika Jumatatu ya wiki hii.

Waandishi waliohojiwa ni pamoja na mwandishi wa gazeti hili, Aziza Masoud na Ibrahim Yamola wa gazeti la Tanzania Daima.

Maofisa hao wawili wanaume na mmoja mwanamke, wakijitambulisha kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, walifika kuwahoji waandishi hao kila mmoja katika kituo chake cha kazi.

Taarifa ilizonazo gazeti hili, Yamola alihojiwa saa 3:00 asubuhi, wakati Aziza akihojiwa saa 5:30 asubuhi katika ofisi za gazeti hili, zilizopo Sinza Kijiweni.

Mahojiano kati ya maofisa hao na Aziza yalichukua takribani saa moja.

Akizungumza na gazeti hili, Yamola alisema: “Mimi walinipigia simu, awali walitaka niende Central (Kituo Kikuu cha Polisi), lakini niliwaambia sitaweza, ndipo walipoahidi kunifuata leo (jana) kwa kunihoji”.

Alisema katika mahojiano yake, ambayo yalichukua takribani dakika 55, walikuwa wakiuliza kuhusu habari aliyoiandika na alipata fursa ya kutolea ufafanuzi kile nilichokiandika tu.

“Kuna muda walikuwa wanataka kutoka nje ya kitu nilichoandika, lakini nilisimamia kilichomo kwenye gazeti kulingana na misingi ya uandishi, ilifika muda nililazimika kushika gazeti ili niwasomee kilichomo,” alisema Yamola.

Wakati huo huo, Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata na kuendelea kumshikilia Rais wa chama hicho, Lissu, kwa makosa ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa jana na Makamu Rais wa TLS, Godwin Ngwilimi, ilieleza mawakili walipojaribu kuhoji Lissu aliwachochea akina nani, na alifanya kosa hilo wapi, wakajibiwa kuwa uchunguzi bado unaendelea.

“Kwa maoni na mtazamo wetu, Lissu anashikiliwa kwa kitendo cha kutoa maoni yake binafsi, basi kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria za nchi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa katika vipindi tofauti, hususan Ibara ya 18 ya Katiba hiyo, kwani inatoa na kulinda uhuru wa kutoa maoni kwa watu wote bila kujali kabila, rangi na imani.

“Haki hii ya msingi pia inatamkwa bayana katika mikataba mbalimbali ya Kimataifa ambayo Tanzania imetia saini na kuiridhia, kama vile Tamko la Kimataifa la Haki za Kijamii na Kisiasa la mwaka 1966 (International Covenant on Civil and Political Rights) na Tamko la Afrika la Haki za Binadamu la mwaka 1986 (The African Charter on Human and Peoples’ Rights),” alisema Ngwilimi.

Alisema TLS inalaani na kupinga vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanapotoa maoni yao binafsi kuhusu masuala mbalimbali ya nchi yao, kwamba ni vema nchi ikaendeleza utamaduni wa kuvumilia maoni tofauti na kukosoana bila kupigana.

Lissu alikamatwa ikiwa ni siku moja baada ya Jumatano kung’ang’ania ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, ili kukwepa kukamatwa na polisi.

Lissu anadaiwa kukamatwa kutokana na kauli alizozitoa katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya hivi karibuni, ambapo alizungumza mambo mbalimbali kuhusu serikali na viongozi wake.

Kubenea na Polisi

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, kutokana na malalamiko aliyoyatoa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Tunamtafuta popote alipo Tanzania hii na ajitokeze yeye mwenyewe, hii Tanzania ni ndogo, aje atupe ushirikiano tumalizane na hili,” alisema Mkondya.

Hivi karibuni, Kubenea alifanya mkutano na vyombo vya habari kama Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF iliyo chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif na kutangaza operesheni ya kumwondoa Profesa Lipumba katika ofisi za chama hicho, zilizopo Buguruni.
Baada ya Kubenea kutangaza operesheni hiyo, siku mbili baadaye, Profesa Lipumba alikwenda kutoa malalamiko polisi.

Mbali na hilo la Kubenea, taarifa nyingine zinadai kuwa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, jana alihojiwa kwa mara nyingine na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, taarifa hizi zilishindwa kuthibitishwa na Kaimu Kamanda Mkondya, huku simu ya Sheikh Khalifa ikiita pasipo majibu.

Bado haijajulikana iwapo Sheikh Khalifa alikuwa bado mikononi mwa polisi au aliachiwa.

Hivi karibuni Sheikh Khalifa alizungumza na kuunga mkono hotuba ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, juu ya masheikh wa uamsho pamoja na matamshi mengine aliyotoa juu ya Waislamu nchini.

Chanzo: Mtanzania
Hii yote ni kwa sababu Polisi wote walipata zero au four form four. Polisi wenye akili hawafanyi kazi hivyi, ndio maana siku zote wanashindwa mahakamani
 
Ujinga upi? Nyie kuwabambikia kesi upinzani ni ujanja? Kuwakomoa Wapinzani ni ujanja? Visasi na uonevu ni ujanja? Utakufa kwa roho mbaya malipo ni hapa hapa Duniani.
Mwenye Akili zake anaelewa
Ni Vipi Tanzania hakuna Upinzani kuna wahuni tu
 
Nasi tunaendelea na maombi ili aendelee kukataa kupima mkojo ili waendelee kumshikilia mpaka atakapokubali...Mkondya shikilia hapo hapo,huyo jamaa anachafua hali ya hewa mtaani.
 
Haya haya...
Yepi. Haya ya tundu lisu kusema mataifa yaisusie nchi. Yasiipe misaada kwa sabb kamteua mtoto wa ndugu yake kuwa katibu wa wizara ya fedha????

Kule uganda mseven kamteua mke wake kuwa waziri na mtoto wake kuwa afisa wa juu wa jeshi.

Kule marekani trump kamteua mkwe wake kuwa mshauri wake mkuu wa masuala ya uchumi. Kamteua mpaka mtoto wake, marekani uko.

Putin kamteua mdogo wake kwenye nafasi nyeti jeshin na kampa Dada yake cheo kama katibu mkuu kwenye wizara ya fedha. Uko ni urusi.

Africa kusini, zuma kamteua bint yake. Kateua marafiki zake kutoka jimbo lake kuwa mawaziri. Huko ni bonden

Uhuru kenyata alimteua hawara yake kuwa waziri. Na ndugu zake kibao kuwa government officials. Apo ni Kenya

Mifano ni mingi sana mkuu. Hata siwezi kuandika yote. Lakin hujasikia matamko na maneno ya kejeli kama tundu lisu.

Democracy is about leting the winner do what he/she thinks is right to achieve what was in the promice.

Unajua siku zote, the end justifies the means. Mkapa alianzisha mamlaka ya mapato (tra) tunaambiwa wafanyabiashara waliandamana mpaka basi. Kariakoo kulikuwa na mgomo wa karibia wiki. Lakin mzee hakurudi nyuma. Alikomaa. Ukiuliza viongozi wa kwanza aliowateua kuwa waanzilishi wa tra huwez kuamin. Lakin Leo hii tunajivunia tra.

Mwache tu lisu avune anachotaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu wa Mbinguni ipo siku atajibu hiki kilio cha watu wengi
 
Hata watawala wa kipindi kile walipi maliza kumnyanyasa Yesu na kumzika waliweka jiwe kubwa sana juu ya kaburi lake, pia waliweka na walinzi ili asitokee wa kuiba mwili wa Kristo yesu, lakini muda ulipo fika mbi gu zilifunguka, na walinzi wakaona kishindo kikuu na Kristo alitoka kaburini akawaachia shimo. Hivyo itakavyo kuwa kwa wanaojaribu kukandamiza haki kwa sababu ya mamlaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanazidi kuumbuka " if you look at magufuli speech kila siku anaongea same shit if u look at polisi kila siku wanafanya same vioja if u look at those idiots supporting huu ukandamizaji njaa zinaongezeka" tanzania is a loosing nation na i pray for the worse ili akili ziwakae sawa.
Haujielewi. The worst will be upon you
Shame on you

Back
Top Bottom