Tatizo lissu haijulikani anafanya yote hayo kwa maslahi ya kitu gani!!
Kama ni democrasia, lissu alitakiwa aanze kuhoji democrasia ya ndani ya chama chake kwanza, iweje mwenyekiti mbowe awe madarakani kwa miongo yote hiyo? Vp kuhusu Matumizi ya pesa za chama? Vipi kuhusu kumpokea lowassa ambaye waliimba ni fisadi? Vipi kuhusu kumpa ugombea wa uraisi mwanachama huyo(lowassa) wa wiki moja?
Utaratibu huu unafanywa na wanaharakati wengi sana, huanza kuhoji walipokaa kwanza, kina usafi? Turejee kwa Malema na ANC, Chacha Wangwe na CHAdema.... Na wengineo.
2. Lissu aseme yupo against na dunia nzima na watu wote wanaomuona magufuli anafanya haya yote kwa kutaka kuiokomboa nchi.
Toka JPM aingie, ameungwa mkono ktk move zake na watu mbalimbali kwasababu amekua akiyafanyia kazi yale ambayo kwa miongo mingi wapinzani wamekua wakiyapigia kelele. Mf. Tuneona jinsi aliyekua mbunge, mwanaharakati Kafulila, akimpongeza JPM kwa move yake ya kuifanyia kazi ishu ya escrow.
NINACHOKIONA MIMI
ninachokiona mimo ni kwamba, lissu ana kitu kinaitwa "political egoism" ambayo ameijenga juu ya "political trust" wananchi waliyoieeka kwake.
Lakini trust ya wananchi sasa inapotea dhidi ya kauli za lissu anazoendelea kuzitoa kila siku, ni wazi kwamba, hata ukifuatilia mitandao ya kijamii, wananchi wengie wamepoteza imani na lissu kwasababu wameshamuona lissu amekua "political ignorant"!!
Hii anayoicheza lissu ni kamali, tena kamali kubwa sana. Lissu anasahau kua mbali na vyama vya siasa nchi ina misingi yake.
Lissu ananikumbusha kauli za morgan tswangiray kule Zimbabwe aliposimama akasema anaunga mkono ushoga na kwamba akichukua madaraka atatudisha ardhi kwa wazungu walionyangaywa na mugabe, ili apate huruma ya wazungu, akisahau kwamba waafrika wanabaki waafrika bila kujali wapo kwenye hali gani...
Kilichomkuta mpinzani huyo wa zimbabwe, ule ndio ukawa mwisho wa siasa zake za upinzani kule zimbabwe.
Kwa hiyo namuona lissu anapoendelea kutoa kauli zake hizi ataishiwa kuchukukiwa na wananchi na vile vile kuendelea kupata kibano kutoka kwa serikali ambayo ni ya mabavu.
Nawasilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app