Polisi kukatiza mitaani na silaha ili hali wakiwa wamevaa kiraia: Je, kanuni za Jeshi la Polisi zina muongozo upi?

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,443
Peace upon you all.

Awali ya yote niwapongeze askari wetu kwa majukumu yao ya kulinda amani tunayoogelea kwayo. Wengine hapa watawasema kwa madhaifu yao kadha wa kadha lakini tafadhali hebu leo tusiwaseme kwanza kila mtu ana madhaifu fulani.

ok, back to the topic wakati fulani nikiwa mkoa wa Morogoro katika shughuli fulani nikiwa mtaani nilishtushwa sana baada ya kuona kundi la watu kama watano wote wakiwa na bunduki na wamevaa kiraia tu jeans na mashati ya kawaida.

kipindi hicho ni wakati ule hapo Kenya wapiganaji wa Al shabab walivadia West Gate na kuua watu wengi. Sasa ghalfa kuona raia wana bunduki mitaani nikachukua taadhari kwa kurudi ndani ya ofiri niliyokua napata huduma fulani, badae ndio naambiwa wale ni askari polisi.

Wakati fulani nikiwa Bukoba nilikwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kuonana na cyber crime officer ili kureport wizi wa laptop na simu (usiende kuriport wizi wa simu jamaa watakuzungusha na simu wataichukua wao na huyo mwizi watamnyofa hela kama watakavyokunyofoa wewe)

Ebo !, kufika kituoni zaidi za 90% ya askari polisi mamevaa kiraia tu na shughuli zinaendelea tu. Ok kwa hapa unameza kusema wako kituoni je wakima uraiani tena wana silaha kabisa si mkanganyiko unameza kutokea.

Jana hapa mtaani viunga vya Butimba the rock city Mwanza kwa kina Fid Q nimeona askari polisi (nilijulisha baadae) mmoja akiwa kavaa kiraia na ana bunduki SMG anakatiza mtaani.

Je hii kikanuni ipoje ? Ni sawa au na kama ni sawa askari wetu kuvaa kiraia ili hali wana silaha na wako mitaani je haiwezi kuleta mkanganyiko kama majambazi wakiamua kujichanganya wakidijai askari, au je raia hawawezi kumdhania askari ni jambazi na kumshambubjia (usiseme anakua na kitambulisho, katika taharuki hakunaga muda wa kutoleana vitambulisho)

Mtu mwingine asiseme ati ni askari mpelelezi,(CID) ndio maana havai uniform hii hoja ya kindezi sana kama ni askari mpelelezi bunduki ya nini si ndio anajienpose na huo upelelezi atampeleleza nani na bunduki yake ?!

Wajuzi au hata askari wetu naomba mnijulishe juu ya jambo hili la kutembea na kunduki mitaani huku mmevaa kiraia, je usalama wenu unazingatiwa kiasi gani na je majambazi hawawezi kupaste wakajifanya wanausalama ikawa shida, na je kanuni za jeshi zinatoa muongozo upi kwa jambo hili.

images (5) (22).jpeg

Picha haiusiani na tukio la askari niliemuona ila inashabiana.
 
Majungu tu haya sijawahi ona tukio la aina hiyo na ukiona hivyo yupo na mwenzake aliyevaa uniform au wakiwa bila uniform basi wapo na gari lao.
 
Thamini majuku ya watu,
Hii amani na utulivu unayoinjoy nyuma ya keyboard unatype uharo ni kwa sababu ya uwajibikaji wao.

Kwanza hiyo uliyosema askari mmoja kabeba bunduki kavaa kiraia anatembea mtaani ni uongo, askari mwenye silaha hatembei mwenyewe, lazima awepo mwingine mwenye silaha, ziwe mbili.

Hakuna mahali utakuta askari wawili au zaidi wapo wamevaa kiraia wamebeba bunduki wanatembea mtaani, unless wawe na gari la polisi.

Ikiwa watatembea mtaani wamejihami kwa silaha na wamevaa kiraia basi lazima awapo mmoja au zaidi aliye ndani ya sare za polisi, ipo hivyo.
 
Ni kweli hii tabia imeanza kuzoeleka askari polisi kubeba silaha huku akiwa amevaa kiraia.

OCDs na RPCs kwa nini mnaruhusu ujinga huu kufanyika kwa kuwa raia wema tutashindwa kutofautisha kati ya jambazi na polisi na siku isiyofahamika kutatokea maafa makubwa halafu mshindwe kutoa maelezo.

Kama ni lazima askari asiye na sare kutembea na bunduki basi aambatane na polisi mwenye sare vinginevyo watembee na bastola.
 
Acha kubisha hapa wapo tena wengi!
 
Unaandika ushuzi baada ya kushiba makande hapo kwa mume wa dada yako. Hiyo amani uliyo nayo kuna watu wanatimiza majukumu yao waliyosomea. Wewe huna unachojua zaidi ya kugombania rimoti na watoto wa dada yako.
 
Hapana nipo hapa nampumulia mama yako kisogo!
 
Nimewahi kukutana na issue kama hii mida ya saa mbili usiku nikashtuka ila kwa vile ilikuwa mita kama 100 kutoka kituo cha polisi nikajiaminisha tu ni askari.

(Ke&Me wote wamebebelea machine wamevaa kiraia wanatembea mtaani)

Haina afya sana hii ikizoeleka.
 
Unadhani hiyo amani na uhuru wa wewe kuandika uzi umepatikana hivihivi? Acha kukosoa mambo usiyoyajua. Watu wapo kazini kuhakikisha usalama. Acha kuingilia yasiyokuhusu
Ukiwa CCM lazima ujifanye mpumbavu? Askari wa Doria wanapita kiraia na wengi wanabaki nyuma mbali kabisa na wenzao wako mbele yeye ana libunduki kwapani. Ikikosolewa Jambo la serikali unakuja mbio Kisa ni wafadhili wa CCM?
 
Back
Top Bottom