Jeshi la Polisi, weledi wenu hauishii kwenye kubeba Bunduki bali mpaka kwenye Kulinda haki za Watuhumiwa huko Mahabusu kwenu

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,041
71,287
Mtu kua Mtuhumiwa, hakumfanyi kupoteza Haki zake za Msingi za Kibinadamu. Ifike Mahali habari za Mtuhumiwa Kufia mikononi mwao Polisi zikome Mara Moja.

Hizi porojo porojo za Mara alipoenda kutuonyesha Silaha, ghafla akataka kukimbia, Mara alipoenda kutuonyesha Silaha, mara akampokonya askari wetu bunduki, na kukimbia au kuanza kurushiana Risasi, tukamjeruhi, amekufa akiwa njiani akikimbizwa Hospitalini , mara nendeni kituo fulani, na fulani na fulani ndio mtamkuta Ndugu yenu.

Hivi mtuhumiwa anaweza kuwapeleka mafichoni silaha ilipo, bila kufungua pingu? Kama amefungwa pingu inakuaje ajaribu kupokonya Bunduki, Sijui mrushiane?

Haya mambo, msiendekeze utumiaji wa nguvu bila akili, Dunia imebadilika, inahitaji watumiaji wa akili. Yaani mtu mnamuingiza Detention cell akiwa mzima wa Afya, siku mbili tatu, kwamba Amefariki? Kisha mnakuja na Ngonjera za kijinga jinga!

Jeshi la Polisi, lianze utaratibu wa kupima Afya za Watuhumiwa pale wanapoingizwa Detention Cell na pale wanaporuhusiwa kutoka iwe Kwa dhamana au wanapothibitika hawana hatia.

Hizi habari za Watuhumiwa kufa wakiwa mikononi mwa Polisi, MNAHATARISHA USALAMA WA NCHI, KWA UJINGA WENU WENYEWE.

Msichukulie Mzaha suala hili, hili suala likome Mara Moja, kama mtanzania ninawataka Jeshi la Polisi muache Mara Moja kuchukulia Mzaha suala hili.

Kifo Cha Mschana Mahsa Amin mikononi mwa Polisi Nchini Iran, kimepelekea machafuko makubwa Nchini humo hata kama Kuna mkono wa Third party, ila Kitendo Cha Raia Kufia mikononi mwa Polisi kulitosha kuichafua Iran .

Jeshi la Polisi ni walinzi wa amani na Usalama wa Raia na Mali zao. Leo hii watu waanze kuogopa Polisi, wawachukie, watu wasiwe na Imani na Polisi , mnatengeneza Taifa gani?

Shukuruni sana huuu Ujinga, unatokea Tanzania. Taifa la watu wajinga, ila hata kitendo cha kuchoma kituo Cha Polisi, kiwaamshe, bila hiuvyo maandamano ya vurugu Nchi Nzima yalitosha kuwafundisha umuhimu wa kuweka P.G.O kichwani!

Polisi ni Mtanzania, Ila sio Kila Mtanzania ni Polisi. Hivyo basi ,mliibahatika kupata nafasi ya kua Polisi Tanzania, basi kumbukeni mnawajibikia kwa Watanzania wenzenu!
 
Nchi mbona imetulia na Askari hawateki watu nadhani Magufuli ndo alikuwa anaharibu dhana ya kulinda raia na mali zake.
 
Back
Top Bottom