Panya Road ni mtandao unaolelewa na Jeshi letu la Polisi

MwanaWA Ebrania

JF-Expert Member
Oct 6, 2017
940
1,138
Hili tatizo la hawa watoto waliokosa malezi bora kwenye familia zao (Panya Road) linazidi kuwa kubwa siku hadi siku. Sababu kubwa wahusika wanadili na matawi, badala ya kuchimbua mizizi ili shina likaushe matawi.

Hawa watoto hawawezi hata siku moja kujipanga na kufikia kupanga uharifu. Kuna watu nyuma yao ambao ndio mastar plan wa kupanga matukio haya pamoja na mengine hatarishi.

Watu hao katili na wenye fikra dumavu ya Afya ya Akili, kazi yao kubwa kuwakusanya watoto kwa njia za ukatili.

Baadhi ya njia hizo ni kuwateka watoto na kuwaficha kwenye mapagala ya majumba yasiyoisha ama majumba ambayo hayakaliwi na watu pamoja sehemu zingine wanakojua wao.

Wengine wana wasafirisha watoto toka mikoa mbalimbali kwa kuwarubuni kwa visenti vidogo huku wakiwaambia maneno mengi ya kuwajaza sumu ya ulaghai na kisha kuwapa mafunzo ya kuwatumikisha kutenda Uovu na Uharibifu.

Hiyo ni mbaya sana maana mtoto ukimfundisha atafanya mara mbili zaidi ya mafunzo Utakayompa.

Zaidi sana watoto hawa ambao walitakiwa kuwa raia wema wanaokatishwa ndoto zao na watu waharibifu wanapokuwa huko kwenye makambi yao hutumikishwa kutumia madawa mbalimbali ya kulevya na kupewa vilevi vikali na kuaminishwa kuwa wanapoona mchuzi wa damu ya mwanadamu inapochuruzika ndio Mungu huwafungulia milango yao ya baraka .

Kwa hiyo Serikali kupitia Jeshi letu la Polisi lazima liangalie kwa makini jambo hili. Maana haya makundi ya watoto yana mtu mwenye akili kubwa nyuma yake, siyo bure bure tu. Hata siku moja watoto hawawezi kujikusanya na kufanya jambo lenye msimamo mmoja tena wa kuhatarisha uhai wa jamii kwa ukubwa kiasi kinachofanywa.

Polisi wetu waache kuchukulia mambo haya kwa wepesi wepesi bila uchunguzi makini. Matukio kama haya yakitokea Polisi wetu mara kwa mara wanawasingizia watoto wanaoishi mitaani (mazingira hatarishi) huku wakijua kabisa siyo kweli.

Maana watoto hao wanaoishi mitaani kuna wakati hawajui chochote! Mtoto anayeishi mtaani, asili yake anaijua pesa, hivyo hawezi hata nukta moja kuambiwa na mtu akaibe kisha wajaze pesa kwenye kiroba halafu huyo mtu amfikirie kumgawia ujira wa kuvuta bangi ama madawa mengine.
Ni kweli watoto wanaoishi mitaani ni wezi, japo kuwa sio wote.

Watoto hao wa mtaani likija suala la pesa wenyewe tu hawaaminiani, sasa kwanini leo wavamie watu halafu pesa wazijaze kwenye shangazi kaja kisha wapeleke kwa kilanja wasubiri mgao? Huyo anayeaminiwa kubeba kiroba cha pesa ni nani na ulinzi wake upoje? Mbona kila wanapokamatwa Panya Road huyu mbeba shangazi kaja la pesa hakamatwi?

Nani mfadhili mkuu wa yale magari yanayowabeba hawa Panya Road? Kwanini hizo gari zisikamatwe zikaangaliwa usajili wake?

Binafsi najua maisha wanayoishi vijana na watoto wengi wa mitaani, ni miongoni pia mwa watoto waliokulia mitaani.

Nakumbuka wakati fulani nikiwa mdogo nasoma pale Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko K/koo siku moja nikiwa mapumziko, nilitekwa na kundi la wadada pisi kali za Kisomali walisimamisha gari pale Barabara ya Shauri Moyo na Lindi Street wakijifanya wasamaria wema wakaniambia niingie kwenye gari nilipoingia wakanipa biscuit na juice nilipokunywa na kula nikajikuta kama fahamu zimekata hivi!

Nilipokuja kushtuka nikajikuta nipo ndani ya jumba fulani maeneo siyaelewi, halafu kushtuka kwenyewe ilikuwa Usiku. Nilikaa mazingira yale kama siku 5 hivi, kila baada ya saa moja anakuja mtu mmoja ananisemesha maneno mazuri ya kunitia moyo wa faraja nami nikawa naendelea kuyasoma mazingira taratibu kwa kujifanya nakubali kila kitu nachoambiwa.

Nje ya ukuta niliokuwepo kuna ukumbi mwingine nasikia sauti pamoja na vishindo vya watu wakifanya mazoezi makali sana, mwisho nikajua kuwa ni kundi ambalo linaandaliwa kwenda kujiunga na Jeshi la Al Shabab, Somalia.

Siku ya saba ndipo nikajua pale mahali ni Keko Mwanga, hiyo ni baada ya kuanza darasa rasmi la mafunzo, hapo niliweza kuwaona watoto wenzangu wengi kutoka sehemu tofautitofauti. Watoto wengine hata Kiswahili hawajui, inaonekana wametolewa vijijini kabisa huko, wakati huo Kimasai nilikuwa nakijua-jua pia nilikutana na watoto wa Kimasai zaidi ya sita. Darasa letu lilikuwa na watoto themanini na tano (85).

Tulikuwa tunafundishwa mafunzo fulani hivi ya kujiona sisi ni mashujaa na zaidi kuwa na roho mbaya. Nilijifanya mtiifu na mnyenyekevu huku nikitafuta njia ya kutoroka, namshukuru Mungu nilifanikiwa kutoroka kwa kutoroshwa na mdada mmoja aliyeonekana mke wa Boss wa wale wasomali wafia dini.

Nimeunganisha hii simulizi fupi kwa sababu, ninaamini watoto hawawezi kujitengenezea uongozi bila kuwa na mtu mzima anayewaongoza.

Hivyo, kuna mambo mengi sana yanatakiwa kufanyiwa kazi na Jeshi letu la Polisi. Natamati kuiona Tanzania ikiwa salama na imara zaidi, kwa maana Inawezekana.

Inawezekana hii mitandao ya uharamia Polisi wetu wakawa wanaijua ama baadhi wasiijue lakini inawezekana kuvunjwa na kusambaratishwa kabisa.

Narudia tena "Watoto pekee yao hawawezi kuwa na umoja hatarishi kama huo." Waswahili walisha sema "Ngoma ya watoto haikeshi," hawa watoto wanajuaje kuua kama hawajafundishwa kuua?

Hawa wote wanaotumikisha watoto ni sehemu ya watu katili, wanahitaji kufikiwa, kufichuliwa na kupewa hukumu kali zaidi .

Screenshot_20230212-093750.jpg
 
Polisi kazi yao kuzuia uarifu wengine tangu waanze kazi mpaka wanastaafu bila kuhamishwa kila siku hiyo ndio kazi yao heti hawajui waalifu walipo nchi hii ina vituko sana
 
polisi kazi yao kuzuya uarifu wengine tangu waanze kazi mpaka wanasitafu bila kuhamishwa kila siku hiyo ndio kazi yao heti awajui waalifu walipo nchi hii invituko sana
Yaani! kuna wakati inaumiza sana, kuona nguvu kazi ya taifa inapotelea kuzimu kabla ya kuziishi ndoto zao
 
Nilikuwa sijui chochote kuhusu kureport ndugu yangu.
Kwa sasa ndio naona nilikuwa mkosaji mkubwa sana
Hujachelewa mkuu nenda karipoti huenda ukaokoa vijana wengi.kama miaka hiyo Kuna watoto hawakuweza kutoroka kama wewe sasa hivi ni watu sampuli Gani Kwa sasa?watakuwa watu wema Kwa mafunzo hayo?Nenda karipoti sasa hivi mkuu.
Pole Kwa yaliyokukuta.
 
Hujachelewa mkuu nenda karipoti huenda ukaokoa vijana wengi.kama miaka hiyo Kuna watoto hawakuweza kutoroka kama wewe sasa hivi ni watu sampuli Gani Kwa sasa?watakuwa watu wema Kwa mafunzo hayo?Nenda karipoti sasa hivi mkuu.
Pole Kwa yaliyokukuta.
Asantee sana Mheshimiwa Nitaenda boss wangu
 
Kuna muda tuna report na police wanashindwa kwa ukosefu wa ushahidi na wakiwakamata mahakama zina shindwa kuhukumu kwasabu mashaidi wanaogopa kujitokeza kutoa ushaidi...

Raia wajipange vizuri tu... Sungu sungu nk.
 
Kuna muda tuna report na police wanashindwa kwa ukosefu wa ushahidi na wakiwakamata mahakama zina shindwa kuhukumu kwasabu mashaidi wanaogopa kujitokeza kutoa ushaidi...

Raia wajipange vizuri tu... Sungu sungu nk.
Ni kweli.
Lkn tusikate tamaa tukaacha kutoa taarifa za uharifu kwa vyombo vyetu vya dola, hatujui siku wala saa chochote kinaweza tokea
 
Basi sio lazima uende, katoe maelrzo hayo polisi watajua namna ya kufuatilia, usije ukatekwa tena
Loh!
Kwa sasa kutekwa kizembe kama vile haiwezekani.... Labda niwateke wao Panya wale Ilikuwa Akili ya kitoto tu' kwa sasa ndio nimejua mambo mengi sana mabaya kuhusu utumikishwaji wa watoto Naumia sana
Haya makundi kama M-23 na mengine ya kigaidi yanamaliza sana watoto wetu
 
Back
Top Bottom