Polisi: John Kohe aliingia benki na kumlazimisha mhudumu ampe fedha bila kufuata utaratibu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikionesha Askari Polisi akipambana na mtu mmoja huku akiwa na silaha ya moto.

Taarifa sahihi ni kuwa, mnamo Januari 15,2026 majira ya saa nane mchana katika Benki ya CRDB tawi la Sirari - Tarime, mtu aitwaye JOHN KOHE AMOSI, Mkurya, Mkazi wa Kijini cha Sokoni – Sirari, alifika katika benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja hadi kwa mtoa huduma wa benki (bankteller) kama mteja huku akiwa amebeba begi dogo na kumwamuru kwa nguvu mtoa huduma ampe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.

Hali hiyo ilisababisha wasiwasi ndani ya benki na kulazimu Askari Polisi waliokuwa lindo nje ya benki hiyo wajulishwe na wakamfuata mtu huyo na kumtaka atoke nje na alitii amri hiyo.

Wakati anasindikizwa na Askari kutoka nje ghafla alimvamia askari kwa lengo la kumpora silaha kwa kupambana na askari, hata hivyo askari walifanikiwa kumdhibiti na kumtoa nje ya benki bila kutumia silaha pamoja na kitendo alichofanya.

Aidha, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa, mtu huyu hana akaunti kwenye benki ya CRDB. Uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini nia ya mtu huyo ilikuwa ni nini na alikuwa anasukumwa na kitu gani hadi kufanya aliyoyafanya ili hatua zingine za kisheria zifuate.

1768831517621.png
 
Dah nimeona video . Mwamba yaani mvamizi ana bahati sana. Askari pia alijikaza kiume kutokuachia silaha Ile. Askari waliokuja kumsaidia mwenzao pia walichelewa kumuwasha chuma mtu yule. Sheria inaruhusu mtu aina Ile ale pipe bila kuchelewa.
 
Daah aisee watu wengine wanakua na ugonjwa wa akili mkuu kama hawakumchapa chuma walikua na akili sana..
 
Polisi wanapenda kujichanganya sana. Sasa hiki kipeperushi chao mbona hakieleweki?
 
Dah nimeona video . Mwamba yaani mvamizi ana bahati sana. Askari pia alijikaza kiume kutokuachia silaha Ile. Askari waliokuja kumsaidia mwenzao pia walichelewa kumuwasha chuma mtu yule. Sheria inaruhusu mtu aina Ile ale pipe bila kuchelewa.
Tumia akili kidogo. Kuna watu wenye ugonjwa wa akili hivyo silaha inatakiwa itumike pale tu njia nyingine zinaposhindikana.
 
Sawa boss. Ingekuwaje kama chizi angefanikiwa kuchukua chuma afu akawachachafya raia waliokuwa pale?
Mkuu uhai wa binadamu ndiyo kitu chenye thamani kuliko vyote duniani. Yaani harakati zote unazoona kila siku mpaka huko benki alikokwenda na hiyo bunduki aliyobeba polisi ni ili binadamu aishi. Hivyo basi tunatakiwa tutumie mbinu zote kuhakikisha uhai hautolewi bila sababu maalum. Hao polisi walifanya vizuri na ndivyo inavyotakiwa. Ndicho nachosizitiza. Sisemi kuua mtu mwenye kusababisha hatari kwa wengine kama ikibidi ni vibaya.
 
Ok boss
 
Ilikuwa hatari sana koz video inaonesha watu zaidi ya 6 eneo lile ikiwemo askari hao. Hivyo angefanikiwa sa hizi tunaongea mengine.
Wanaweza hata kuwa watu kumi ndio kazi yao hiyo mkuu mimi nawapongeza kwa kutotumia Risasi maana hauwezi jua ingewapata wangapi hapo sema Tanzania mnaona risasi inapiga pale tu unapotaka aisee huyo ni mgonjwa afungwe kudu apelekwe milembe akapimwe utaua wangapi wananchi wako wanaochanganyikiwa..
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikionesha Askari Polisi akipambana na mtu mmoja huku akiwa na silaha ya moto.

Taarifa sahihi ni kuwa, mnamo Januari 15,2026 majira ya saa nane mchana katika Benki ya CRDB tawi la Sirari - Tarime, mtu aitwaye JOHN KOHE AMOSI, Mkurya, Mkazi wa Kijini cha Sokoni – Sirari, alifika katika benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja hadi kwa mtoa huduma wa benki (bankteller) kama mteja huku akiwa amebeba begi dogo na kumwamuru kwa nguvu mtoa huduma ampe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.

Hali hiyo ilisababisha wasiwasi ndani ya benki na kulazimu Askari Polisi waliokuwa lindo nje ya benki hiyo wajulishwe na wakamfuata mtu huyo na kumtaka atoke nje na alitii amri hiyo.

Wakati anasindikizwa na Askari kutoka nje ghafla alimvamia askari kwa lengo la kumpora silaha kwa kupambana na askari, hata hivyo askari walifanikiwa kumdhibiti na kumtoa nje ya benki bila kutumia silaha pamoja na kitendo alichofanya.

Aidha, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa, mtu huyu hana akaunti kwenye benki ya CRDB. Uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini nia ya mtu huyo ilikuwa ni nini na alikuwa anasukumwa na kitu gani hadi kufanya aliyoyafanya ili hatua zingine za kisheria zifuate.
Mtu huyo anaonekana anamatatizo ya Afya ya akili
wangempima kwanza kabla ya kumchukulia hatua nyingine
Niwape pongezi askari waliokuwa zamu kwa kutotumia silaha; kwani kutumia silaha ni hatua ya mwisho kabisa na hasa unavyobaini mtuhumiwa anakuzidi nguvu....silaha haitumiwi kizembe kama fimbo.
WAMEFUATA WELEDI WA MAFUNZO YA KIASKARI
 
Back
Top Bottom