Polisi Dar yampa saa 24 Nabii Mwingira ili ajisalimishe kwa Mahojiano

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Jeshi hili lisiendeleze udhalimu kwa kumfurahisha mtu mmoja.
Lijitafakari kuna mengi sana yako kati hivyo lisikurupuke.
J2 hii yamesemwa menginsana kwenye nyumba za ibada wayatafakari.

Jingine watuletee majibu ya mambo mengi ambayo wamedili nayo na bado hayajajibiwa. Mfano nani hasa mhusika wa wizi wa mafuta huko kigamboni? Kama.ni wao wenyewe Chama chakavu na wakubwa wao wanaona aibu gani.kuwataja na kuwafungulia mashtaka?? Ina maana mche ule unaendelea hadi leo! Tuweni wakweli.

Tanzania haina Ugaidi hili liko wazi!. Maridhiano muhimu.
 
Huenda huku kuogopa kuambiwa wajisalimishe ndiko kunakofanya wengine wasiseme pindi yakiwakuta ya kuwakuta....

Badala ya Polisi kuwa rafiki na kimbilio wengine wanapaona pa kupakimbia na sio Salama
 
Ajisalimishe kwa uhalifu gani alioufanya? Kamanda Murilo tafuta maneno sahihi ya kutumia maana unaweza ongea kishujaa alaf mbele ya safari ukaja kuonekana kituko kwa watu ikiwemo familia yako
Dah keyboard warrior mnavo mpa bichwa huyo mwingira utafikiria mtaenda kuhojiwa wote hasa akiambiwa atoe ushahidi, I think mashabiki maandazi wa mtandaoni hamjawahi hojiwa na mapolice walio serious na kazi.
 
Hii ni Taarifa iliyotolewa na Jumanne Murilo ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam .

Kamanda ameagiza Polisi kumtafuta popote alipo na kumleta kanda maalum kwa mahojiano , kwa tafsiri ya kiswahili tangazo hili la Kamanda ni AGIZO LA KUMKAMATA Askofu Mwingira .

====

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

Pia soma:

Thread 'Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali' Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali
Kwanini askari huwa hawana kauli za busara na zenye kuonesha wanatumia akili, yaani ni mwendo wa kubwatuka kama uharo, sijui wana shida gani.
 
Ajisalimishe kwa uhalifu gani alioufanya? Kamanda Murilo tafuta maneno sahihi ya kutumia maana unaweza ongea kishujaa alaf mbele ya safari ukaja kuonekana kituko kwa watu ikiwemo familia yako
Murilo naye ameaagizwa na Simbachawene.
 
Back
Top Bottom