Polisi Dar yampa saa 24 Nabii Mwingira ili ajisalimishe kwa Mahojiano

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,295
Hii ni Taarifa iliyotolewa na Jumanne Murilo ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam .

Kamanda ameagiza Polisi kumtafuta popote alipo na kumleta kanda maalum kwa mahojiano , kwa tafsiri ya kiswahili tangazo hili la Kamanda ni AGIZO LA KUMKAMATA Askofu Mwingira .

====

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

Pia soma:

Thread 'Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali' Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali
 
Last edited:
Hii ni Taarifa iliyotolewa na Jumanne Murilo ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Chanzo : Mwananchi

Hata kwa Desmond Tutu haikuwa rahisi:

IMG_20211227_112550_315.jpg

Baba askofu aambatane na jopo zito la mawakili wasomi.
 
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom