Akamatwa na pikipiki 32 za wizi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Omari Mlopa (28), mkazi wa Mlandizi na wenzake wawili wakiwa na pikipiki 32, zilizoibiwa na baadae kuzifanya zao kwa kukodisha kwa mikataba kwa watu mbalimbali na kujipatia pesa kila siku.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema “Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kuwa Watuhuhumiwa hao walibadilisha namba za usajili za pikipiki hizo na kuweka namba bandia ili zisitambulike na pikipiki 13 tayari zimetambuliwa na Wamiliki”
 
Kuna dogo boda huwa tunamtumia ofisini kaibiwa pikipiki yake Alhamis iliyopita, inasikitisha sana.
Aliingia msikitini kuswali wakaiba.
 
Back
Top Bottom