Polisi Dar yampa saa 24 Nabii Mwingira ili ajisalimishe kwa Mahojiano

Hii ni Taarifa iliyotolewa na Jumanne Murilo ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam .

Kamanda ameagiza Polisi kumtafuta popote alipo na kumleta kanda maalum kwa mahojiano , kwa tafsiri ya kiswahili tangazo hili la Kamanda ni AGIZO LA KUMKAMATA Askofu Mwingira .

====

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

Pia soma:

Thread 'Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali' Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali
Ili uwe polisi = urefu+ mbio+ feli mitihani ya form four na kuwa muongo
 
Ni kazi ya watumishi wa Mungu kuinyooshea serikali vidole, na kuikosoa kila inapokosea! Mwingira amesimamia wajibu wake muhimu! Kuhusu kuimba mapambie, yana paswa kuelekezwa kwa Mwenyenzi Mungu pekee!
Sasa kufungwa ni kawaida tu, Mbona Yesu alikufa kwa kuusimamia ukweli?! Na hata manabii na mitume wengi walifungwa au kuuwawa kwa kuisimamia imani yao?!!
 
Tunarejea kwa kasi sana. Kwani hivi utaratibu ukoje, mtuhumiwa na hasa mwenye address permanent kama askofu kuna sababu ya kumuita kwa media?
Yale makanisa ya mfukoni Kama efata ndo unaita permanent address.! Mda wowote anaweza kusepa na vitu vyake Mana kanisa ni lake siyo la waamini ndo Mana amesema Mali zake ziliharibiwa na siyo Mali za kanisa. Jamani zindukeni hayo siyo makanisa Ni vitega uchumi vya watu.
 
CCM ijitafakari.Kabla ya anguko kiburi hutangulia.katika mambo ambayo nitaendelea kumlaumu Nyerere ni pamoja na kutuletea CCM!
 
Naona prejudice katika hili agizo la kumuita Mwingira. Hajaitwa ili waweze kupambanua mahojiano yatawaambia waanze na mguu gani ama wa kumshtaki Mwingira kwa uchochezi au mguu wa kutafuta ukweli wa alichosema.

Agizo linaonyesha tayari wanachukulia Mwingira ni mchochezi. If they did some mind games wangeweza mnasa wanapopataka lakini unapoanza kwa kushambulia naona wametangaza vita kabla hata hawajapata facts kutoka katika kauli za Mwingira.
 
Ajisalimishe kwa uhalifu gani alioufanya? Kamanda Murilo tafuta maneno sahihi ya kutumia maana unaweza ongea kishujaa alaf mbele ya safari ukaja kuonekana kituko kwa watu ikiwemo familia yako
Kujenga hofu na chuki dhidi ya mtu mwingine au Serikali ni kosa la jinai. Leo huwezi kujitokeza tu ukasema uongo kuwa mtu fulani au Serikali inataka kukuua then uachwe tu. Ni lazima uwajibike kwa kauli hiyo .
 
Hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao. Serikali ya wananchi huchaguliwa na wananchi. Sasa kamanda anaizungumzia serikali ipi ya wananchi?
 
Ajisalimishe kwa uhalifu gani alioufanya? Kamanda Murilo tafuta maneno sahihi ya kutumia maana unaweza ongea kishujaa alaf mbele ya safari ukaja kuonekana kituko kwa watu ikiwemo familia yako
Kwani wewe maelezo aliyoyatoa yeye Mwingira hujayasoma na kuyaelewa kuwa ni ya kijinai? Unaposema watu wa serikali walitaka kukuua mara tatu basi kataje ili hata umma wa Kitanzania uwajue hao watu hatari wa serikali na sheria ichukue mkondo wake, la sivyo mwenyewe lazima uende na maji kwa kuleta chuki ya raia hasa waumini wako dhidi ya serikali! Wewe kwa kweli ndiyo kituko cha familia yako!
 
Hahah...

Jamaa wana mikwara utadhani ofisi yake pale Mwenge hawaijui, au kule Kibaha au maskani kwake kule Kawe...
 
Kimya kimya kama nani vile yeye alisema kimyakimya ,alitamka wazi atakamatwa wazi full stop

USSR

Alaf akishakamatwa unadhani kuna kipi cha maana kitaendelea? Acheni kupoteza rasilimali za watu
 
Dah keyboard warrior mnavo mpa bichwa huyo mwingira utafikiria mtaenda kuhojiwa wote hasa akiambiwa atoe ushahidi, I think mashabiki maandazi wa mtandaoni hamjawahi hojiwa na mapolice walio serious na kazi.

Hatujuani we pita kimya kimya usishambulie mtu
 
Hii ni Taarifa iliyotolewa na Jumanne Murilo ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam .

Kamanda ameagiza Polisi kumtafuta popote alipo na kumleta kanda maalum kwa mahojiano , kwa tafsiri ya kiswahili tangazo hili la Kamanda ni AGIZO LA KUMKAMATA Askofu Mwingira .

====

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LIMEAGIZA KUANZA KUHOJIWA KWA ASKOFU MWINGIRA.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam limeagiza ndani ya saa 24 kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa kanisa la Efatha Josephat Elias Mwingira juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa dhidi ya Serikali ikiwemo njama za Maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo na kuona kuwa zinajenga hofu na chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa uzito wa mambo yanayodaiwa kutolewa na Askofu huyo ni lazima apatikane haraka iwezekananavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho Jeshi linaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa tahadhari kuwa halita sita kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye anatumia vibaya Uhuru wa maoni ya kikatiba, na kuwakumbusha wananchi kuwa uhuru huo lazima uzingatie Sheria za Nchi na usikiuke haki na uhuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

MULIRO JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

Pia soma:

Thread 'Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali' Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali
Kuna mtumishi mmoja wa Mungu alionyeshwa ktk maono miaka 25 iliyopita Tanzania ikiwa imetapakaa Damu tupu,yaani alionyeshwa vita, civil war ndani ya Tanzania.
CCM wanatafuta kwa nguvu zao zote Damu imwagike Tanzania, yaani kuwachapa na maisha magumu haitoshi wanagusa hadi watumishi wa Mungu.
Ndani ya kanisa la EFATHA kuna kundi zito la majenerari na Brigedia wanasali hapo na wanamhusudu Mwingira hata huyu boya wa Guinea hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku wanajeshi watamlaza selo.
CCM wana kiburi cha kipumbavu sana,wanatengeneza machafuko kwa nguvu zao zote.
Eti wana kiburi cha Dola, hiyo Dola kuna siku itakuwa mdoli.
Kuna Jambo lina mwisho.
 
Back
Top Bottom