- Source #1
- View Source #1
Auwawa kwa kuchomwa Moto na baadhi ya wananchi baada ya kubainika kushiriki kwenye mauaji ya October 29
- Tunachokijua
- Januari 28, 2026 kumekuwapo na video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa ni ya tukio la Polisi kuchomwa moto na kupokonywa silaha mkoani Njombe baada ya wananchi kubaini kuwa alishiriki katika matukio ya Oktoba 29, 2025.
Uhalisia wa video hiyo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kwa kina na kubaini kuwa video hiyo si ya mwaka 2026 na haihusiani na tukio la polisi kuchomwa moto Arusha.
Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo Google lens umebaini kuwa video hiyo ilichapishwa mtandaoni kuanzia Agosti 3, 2025 ambapo ilielezwa kuwa mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwizi alichomwa moto.
Vyanzo mbalimbali viliripoti kutokea kwa tukio hilo tazama hapa na hapa. Vyanzo hivyo vinaibainisha kuwa tukio hilo lilitokea katika mtaa wa Kirika B, kata ya Osinyae mkoa wa Arusha.
Inaelezwa kuwa kijana huyo alitambulika kwa jina la alikutana na mashambulizi hayo baada ya kudaiwa kuiba vinywaji na spika katika bar mmoja katika eneo hilo.