Uchaguzi 2020 Unapomwita binadamu mwenzako Msukule mbele ya vyombo vya habari unataka Taifa ligawanyike upate nini?

Humphrey Polepole tuliasa asiruhusiwe kuendelea kutumia media, anachofanya siyo siasa nikuwalisha sumu ya mpasuko wanaomsikiliza.

Huwezi kumwita mgombea na binadamu mwenzako MSUKULE ukadhani unaimarisha chama, unakiua. Unaondoa roho wa utii miyoyoni mwa wapiga kura. Unaondoa utu unajivika unyama kwa madaraka yakupita kwanini?

Leo CHADEMA wakiwaita CCM misukule patakalika au ndo maelekezo yatatolewa kwa vyombo vya ulinzi?

Viongozi wa dini mnayaona haya? Tume mnayaona haya? Wazee mnayaona haya?

Wananchi wamechoka kusikia Lisu amefanya hiki na kile wanataka kuambiwa mtafanya nini?

Kama hamna familia sisi wengine familia tunazo na tuna haki ya kuzilinda, Kama mna nchi yakwenda kwa uwezo wenu wa kiuchumi cc hatuna pakwenda. Msituvuruge kwa kushindwa kwenu kutambua wananchi wanataka nini.
 
Hiyo yote ni mipango ya Mungu. Huyu polepole yupo ili litimie lililokusudiwa. Mungu amemuweka ili afanye maudhi, akere watu, apandishe hasira ili wapigakura wafanye maamuzi yaliyosahihi.
Kumbuka kutukana hakuongezi kura za anayetukanwa, huenda zitamnufaisha anayetukanwa.
Polepole anamharibia mgombea wa CCM badala ya kumsaidia. Kama hawajaweka msemaji mwingine, CCM wataendelea kupoteza.
 
Na

Nadhani angeusema huo ukweli ingetosha watu wangeelewa anacuokusudia lakin kutukana tena
 
Back
Top Bottom