Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Mgombea Urais kupitia CHADEMA jana Jumatano alifanya "Press conference" na Vyombo vya Habari hapa nchini, akilalamikia kutomfanyia "coverage" yeye akiwa ni mgombea Urais toka chama kikuu cha upinzani hapa nchini, kwa alichokiita ni Hofu, Hofu, Hofu iliyowajaa waandishi wa habari, pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo.
Jambo la kushangaza ni kuona kuwa hata chombo cha habari cha Umma, Televisheni ya TBC, ambayo gharama za uendeshaji wake tunaibeba walipa kodi wa nchi hii, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, nacho hakitaki kumripoti mgombea huyo wa kiti cha Urais!
Kwa namna ya jinsi inavyotoa ripoti, na kuzifanya habari za Rais John Magufuli, kuwa ni "lazima" zipewe kipaumbele, zinafanya chombo hicho cha habari nchini cha TBC, kuwa kama ni chombo cha propaganda za CCM!
Kinachotakiwa na vyombo vya habari hapa nchini ni kuondoa hofu ambayo imetanda miongoni mwao, katika kuripoti matukio ya kampeni ya mgombea huyo wa Urais wa chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA na kufanya kuwa fair kwa kutoa nafasi iliyo sawa kwa vyama vikuu hapa nchini vya CCM na CHADEMA.
Swali kubwa ninalojiuliza, je baada ya Tundu Lissu kufanya hiyo "press conference" vyombo vya habari hapa nchini vimeanza kubadilika na kuona hakuna "consequences" za kuanza kumripoti huyo mgombea Urais wa chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA?