Uchaguzi 2020 Je, Vyombo vya Habari vitaanza kumpa "Coverage" kubwa Tundu Lissu, mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Ingawaje kwenye sekta ya habari, kuna kanuni moja Kuu kuwa ni lazima waandishi hao wazisake kwa nguvu zote habari zinazouzika, lakini kwa hapa nchini hali imekuwa tofauti sana, kwa vyombo vyote vya habari nchini, ambapo "vimelazimishwa" kutangaza habari za upande mmoja pekee, za Rais Magufuli pekee, katika kile kinachoitwa, kutangaza juhudi zake za kuliletea maendeleo Taifa letu

Kwa msingi huo huo ni kama habari nyingine zozote zilikuwa zimewekewa "blackout" hususani habari zinazohusu, chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA na zinazomuhusu Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, ambaye pia ndiyo mgombea wa nafasi ya Urais kwa chama hicho, Tundu Lissu.

Nikitoa mfano halisi ni namna serikali hii ya awamu ya tano, ilivyotoa "kibano" cha kutoa onyo kali kwa baadhi ya vyombo vya habari vya hapa vya hapa nchini na vingine kupigwa faini kubwa kwa "dhambi" ya kutangaza habari za washirika wao, mashirika ya habari ya nje ya BBC, DW na VoA, walipomhoji mgombea huyo wa kiti cha Urais Tundu Lissu!

Hakika sheria ya vyombo vya habari vya hapa nchini zimekuwa kandamizi mno, kiasi ambacho kunakuwa na "censorship" kubwa mno kiasi ambacho waandishi wa habari wa hapa nchini wanafanya kazi katika mazingira magumu mno, kwa kuwa hawajui ni habari gani ambayo wahariri hao wa vyombo vya habari wataiafiki itolewe kwenye vyombo vyao vya habari!

Kwa hiyo siyo ajabu kuviona baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini, yakiwemo magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, yakipewa vifungo vya maisha kwa kosa tu la "kubalance story" na siyo kujiegemeza upande mmoja kwa kutangaza mazuri pekee ya serikali hii, bila kukosoa yale ambayo hayafanyiki vyema, ambapo ni kanuni muhimu sana kwenye sekta ya habari.

Kinachoshangaza ni kwa chombo cha habari cha Umma, cha televisheni ya Taifa nchini ya TBC, ambayo inagharimiwa na wananchi wote wa nchi hii, bika kujali itikadi zetu za chama, kwa maana tupo walipa kodi wana-CCM na wana-CHADEMA, kujiunga katika "praise and worship" kwa kumtangaza Rais Magufuli kwa "almost" masaa 24 ya matangazo yao

Kinachotakiwa na watawala wetu wa Serikali hii ya Awamu ya 5 ni kutaka kuona habari zinazowapa wao pekee sifa na mapambio katika kile kinachoitwa maendeleo makubwa sana, yanayofanywa na serikali hii.

Swali ninalojiuliza hivi sasa, je vyombo vya habari vitabadilisha mwelekeo wao na kuanza kuwatangaza wagombea Urais wa vyama vingine, hususani wa kutoka chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA?

Kwa kuwa siyo siri tena kuwa habari yenye mvuto mkubwa hivi sasa hapa nchini ni za Tundu Lissu pamoja na chama chake cha CHADEMA, kwa hiyo kama wamiliki wa vyombo hivyo vya habari nchini, vitataka ku-survive, hawana budi kuzitangaza habari hizo za Vyama vya Upinzani.
 
Mlishavitukana mnavitaka vya nn. Usitukane mamba kabla haujavuka mto. Haya sasa nendeni huko hard talk mkasemelee

Vyombo vya nje vinapenda kutangaza balanced story tatizo linabaki hawana mwandishi mwakilishi na hawana TV inayowawakilisha ambayo ni huru, hivyo njia pekee ambayo upinzani wanayo ni hii mitandao ambayo nayo naona wameshaanza kuikorofisha kwani siku mbili zilizopita kuna dalili ya kukosekana kwa maksudi.
 
Mlishavitukana mnavitaka vya nn. Usitukane mamba kabla haujavuka mto. Haya sasa nendeni huko hard talk mkasemelee
Hauwezi kuyazuia maji ya mafuriko kwa mkono.

Mkuu elewa kuwa tulikuwa tunawapa lawama hivi vyombo vyetu vya habari, ambayo ni "genuine" kwa kuwa vyombo vya habari vya hapa nchini, vikikuwa siyo tu "biased" Bali vilizidisha ushabiki katika kile wanachokiita "praise & worship" kwa kazi wanayoiita ya kutukuka ya Rais Magufuli!

Hisusani TV ya Umma ya TBC inayoendeshwa kwa kodi zetu sote bila kijali itikadi zetu za siasa
 
mvuto mkubwa hivi sasa hapa nchini ni za Tundu Lissu pamoja na chama chake cha CHADEMA, kwa hiyo kama wamiliki wa vyombo hivyo vya habari nchini, vitataka ku-survive, hawana budi kuzitangaza habari hizo za vyama vya upinzani.
Kwa Nini mnalazimisha muwe covered?

Ninyi ndio mnatakiwa muvialike vyombo kwenye mikutano yenu,lakini wameshakubaliana Kama Kuna matusi hakuna kuandika wala kuhudhuria mtarusha kupitia facebook
 
Hauwezi kuyazuia maji ya mafuriko kwa mkono.

Mkuu elewa kuwa tulikuwa tunawapa lawama hivi vyombo vyetu vya habari, ambayo ni "genuine" kwa kuwa vyombo vya habari vya hapa nchini, vikikuwa siyo tu "biased" Bali vilizidisha ushabiki katika kile wanachokiita "praise & worship" kwa kazi wanayoiita ya kutukuka ya Rais Magufuli!

Hisusani TV ya Umma ya TBC inayoendeshwa kwa kodi zetu sote bila kijali itikadi zetu za siasa
Nani aripoti matusi yenu bana
 
Kwa Nini mnalazimisha muwe covered?
Ninyi ndio mnatakiwa muvialike vyombo kwenye mikutano yenu,lakini wameshakubaliana Kama Kuna matusi hakuna kuandika wala kuhudhuria mtarusha kupitia facebook
kabombe
Kuwa mkweli, hivi ni nani hasa mwenye kutoa matusi makubwa kati ya viongozi wetu wa vyama vya upinzani na Mwenyekiti wenu?

Au ndiyo unafuata ule msemo wa wahenga, unaosema nyani halioni kundule?
 
ITV Jana walibalance habari, walilipoti habari za kuenguliwa mkurugenzi wa UCHAGUZI Jimbo la Vunjo, walilipoti kuhusu kuuwawa kwa mvamizi dhidi ya Mgombea CHADEMA Ukara Mwanza, na walilipoti habari ya Lisu baada ya kutangazwa na NEC kuwa mgombea uraisi kwa Tiketi ya CHADEMA. Mambo mazuri yanakuja
 
Mlishavitukana mnavitaka vya nn. Usitukane mamba kabla haujavuka mto. Haya sasa nendeni huko hard talk mkasemelee
Hivi huyu Mwenyekiti wenu kuvipiga mkwara mzito vyombo vya habari hapa nchini, kwa kuviambia "watch out, you don't have that freedom of speech to that extent" unadhani hiyo ni sawa kweli?
 
Tutapashana wenyewe. Mimi mtaani kwangu kijijini,nimehakikisha. Ni Yeye, mpaka kwa Wazee 60+
Hata hivyo hizi social networks zinafanya kazi kubwa sana.

Yeye Jiwe mawazo yake ni kuwa kwa "kuvilazimisha" vyombo vya habari nchini, viandike habari zake pekee, basi atakuwa amezoa umaarufu mkubwa sana, amenoa, kwa kuwa pamoja na kumwuwekea,"blackout" Tundu Lissu lakini anashangaa kuona kuwa umaarufu wake umeongezeka maradufu!
 
Kwani mgombea yupo pekee mpaka apewe hiyo coverage unayotaka?
Hakuna ubishi kuwa Tundu Lissu ndiye mgombea Urais kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema.

Kwa hiyo hata waandishi wa habari wanazichukulia habari zake kuwa ni "hottest"
 
Chadema wangekuwa na social media consultants
Wamalize mchezo
Sijui kwanini had Leo hawana radio yao jamani..mie Kuna mambo yananikera Sana .Kama baadhi ya majimbo kupitia bila kupingwa .hivi chadema walishindwa toka muda kuwatafuta vijana smart wakawekwa kila Jimbo kupinzana na Hawa NYAU wa Kijani? Yaani najiskia Moto moyoni!Mnyika na Mbowe mnaboa kinyama.🤨😏
 
Back
Top Bottom