Vulmeko
JF-Expert Member
- Jul 15, 2025
- 295
- 237
Mheshimiwa Polepole, kuna clip nimeiona mahali, ulikuwa unafundisha kwa makini sana masuala ya imani ya kikristo. Ulifundisha kwa weledi mkubwa kiasi kwamba waliokuwa wanakusikiliza walikuelewa na kukubaliana nawe 100%. Hiyo video imenidhihirishia kuwa wewe pasina shaka ni muumini mzuri wa Biblia na mafundisho ya Masihi Yesu.
Sasa katika video yako uliyoirusha hivi majuzi kuhusu wanamtandao, umesema kwamba Mungu akiwavusha, mtaweka sheria ya kuwafunga viongozi wakuu wastaafu wenye makosa. Mimi si mjuzi sana wa Biblia lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba usipowasamehe waliokukosea hautasamehewa. Kwenye video hiyo ulisema unatoa msamaha kwa mambo mengine, lakini mambo ya kisiasa hapana kusameheana.
Kwa unyenyekevu mkubwa swali langu ndio hili: Hiyo kauli umeitoa wapi kwenye Biblia? Ni wapi Yesu alisema msamaha hautolewi kwa watu waliokosea kisiasa?
Natanguliza shukrani kwa majibu mema, na yenye lengo la kunisaidia niijue Biblia kama wewe. Asante, mkuu.