Polepole - Hii kauli yako umeitoa wapi kwenye Biblia?

Polepole - Hii kauli yako umeitoa wapi kwenye Biblia?

Sheria za nchi haziendeshwi na biblia. Unaweza ukawa mtu wa Mungu lakini ikija kwenye sheria za nchi hata kama ni dhambi lazima itekelezwe. Kama tunapaswa kusamehe basi jela ziondolewe na wahalifu wote wasamehewe waachiwe huru
Yes. Na kama dhambi zote zinasamehewa, hakuna atakayeingia motoni!
 
😹😹😹 Kwahiyo kila atakayekujibu ni Polepole?
Mimi sijui. Ila nashangaa, swali nimemuuliza Mh. Polepole, inakuwaje majibu yanatoka kwa mtu asiyeitwa Polepole? Ndo maana nikahisi labda Polepole ana ID nyingi. Vinginevyo labda Polepole amewatuma mumsaidie kujibu.
 
Kwa sababu alitubu
Na Serikali za muDuniani zingekuwa na utaratibu kama huo ingekuwa poa sana 😳 !
Unaenda unaiba unakwapua kweli kweli unawaacha watu na vilema vya kudumu kisha unawahi chapchap unakwenda kutubu 🙏. Biashara imeisha unasamehewa ! Hiyo ni poa sana 🤣🤣🤣 🫡
 
Yesu alisema dhambi zote zitasamehewa lakini dhambi ya kukufuru roho mtakatifu haitasamehewa kamwe!!

Naweza kusema Kuna dhambi unaweza kusamehe kabisa lakini vilevile Kuna dhambi unaweza usisamehe.

Mathayo 12:31–32
"Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kukufuru watasamehewa wanadamu; ila kufuru ya Roho haitasamehewa."
🙏😄
 
Mheshimiwa Polepole, kuna clip nimeiona mahali, ulikuwa unafundisha kwa makini sana masuala ya imani ya kikristo. Ulifundisha kwa weledi mkubwa kiasi kwamba waliokuwa wanakusikiliza walikuelewa na kukubaliana nawe 100%. Hiyo video imenidhihirishia kuwa wewe pasina shaka ni muumini mzuri wa Biblia na mafundisho ya Masihi Yesu.

Sasa katika video yako uliyoirusha hivi majuzi kuhusu wanamtandao, umesema kwamba Mungu akiwavusha, mtaweka sheria ya kuwafunga viongozi wakuu wastaafu wenye makosa. Mimi si mjuzi sana wa Biblia lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba usipowasamehe waliokukosea hautasamehewa. Kwenye video hiyo ulisema unatoa msamaha kwa mambo mengine, lakini mambo ya kisiasa hapana kusameheana.

Kwa unyenyekevu mkubwa swali langu ndio hili: Hiyo kauli umeitoa wapi kwenye Biblia? Ni wapi Yesu alisema msamaha hautolewi kwa watu waliokosea kisiasa?

Natanguliza shukrani kwa majibu mema, na yenye lengo la kunisaidia niijue Biblia kama wewe. Asante, mkuu.
Mkuu ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Mstari huu umebeba nukuu hiyo ya HP!
 
Mwanangu sana Lamomy usipoteze muda wako kujibishana na ID ya juzi kati imejoin kwa kazi maalum.
Hehee, sikujua hilo. Kumbe wengine humu mlijoin kwa kazi maalum? Anyway, acha nikutoe hofu. Mimi ni member wa kawaida tu, usiogope kutoa yako ya moyoni.
 
kweli sasa naanza kuamini kama H.Polepole asemavyo " hii ngoma tunashinda " ...
 
Kusamehe au kutokusamehe ni utashi wa mtu binafsi mwenyewe
Kama nilivyotangulia kusema, nimejiridhisha kwamba huyo ni mtaalam wa Biblia. So, nadhani hata hiyo kauli yake amei-base kwenye Biblia. Tusubiri labda atajitokeza kutuambia ameitoa wapi
 
Mimi si mjuzi sana wa Biblia lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba usipowasamehe waliokukosea hautasamehewa
Kusamehe sio lazima, hata Mungu mwenyewe hajawahi kumsamehe Shetani.
 
Kwa sababu alitubu
Mahakamani wahalifu huwa wanakiri makosa lakini badala ya kusamehewa wanatupwa jela maisha! Hakimu anasema: "Iwe fundisho kwa wengine"!!
 
Mheshimiwa Polepole, kuna clip nimeiona mahali, ulikuwa unafundisha kwa makini sana masuala ya imani ya kikristo. Ulifundisha kwa weledi mkubwa kiasi kwamba waliokuwa wanakusikiliza walikuelewa na kukubaliana nawe 100%. Hiyo video imenidhihirishia kuwa wewe pasina shaka ni muumini mzuri wa Biblia na mafundisho ya Masihi Yesu.

Sasa katika video yako uliyoirusha hivi majuzi kuhusu wanamtandao, umesema kwamba Mungu akiwavusha, mtaweka sheria ya kuwafunga viongozi wakuu wastaafu wenye makosa. Mimi si mjuzi sana wa Biblia lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba usipowasamehe waliokukosea hautasamehewa. Kwenye video hiyo ulisema unatoa msamaha kwa mambo mengine, lakini mambo ya kisiasa hapana kusameheana.

Kwa unyenyekevu mkubwa swali langu ndio hili: Hiyo kauli umeitoa wapi kwenye Biblia? Ni wapi Yesu alisema msamaha hautolewi kwa watu waliokosea kisiasa?

Natanguliza shukrani kwa majibu mema, na yenye lengo la kunisaidia niijue Biblia kama wewe. Asante, mkuu.
Hamjamjua bwana Polepole, kinachomfanya aongee yote hayo sio uzalendo bali ni kukosa alichokitaka kwenye CCM. Roho yake imejaa visasi na chuki kwa wote waliopo madarakani, hana ajenda kubwa ya kuwasaidia wananchi anachojali ni kupambana na anaowaita wahuni.
Katika mazungumzo yake ni kama CCM yooote ina watu wabaya kasoro yeye na Gwajima, huu ni ugonjwa wa akili ulio dhahiri.
 
Ehee, kwahiyo viongozi wastaafu wanafananishwa na shetani? Makubwa hayo!
Sijamfananisha mtu yoyote na shetani bali nimesema sio lazima kusamehe maana hata 'Mungu mwenyewe hajawahi kumsamehe shetani' nyie ndio mnawachomesha watu alafu wanashitakiwa kwa makosa kubumba alafu mnabaki kuona aibu huku mnachekesha kwenye familia zao.
 
Yesu alisema kabla hujaenda kutubu lazima uombe msamaha uliemkosea na kama umechukua mali yake urudishe..!!
Really? Kwani lile jizi msalabani lilipata nafasi ya kuwaomba msamaha liliowakosea na kurudisha mali zao? Mbona lilipewa tu msamaha?
 
Back
Top Bottom