Poleni Rais Magufuli na KUB Mbowe kwa vijana wenu kupata maambukizi ya Covid 19, Mungu ni mwema amewaponya

Sidhani kama kuna MTU Wa kuchagua chama cha mawakala Wa mabeberu chadema! Yalikuwa yanalilia lockdown na kufunga nyumba za ibada ili kuwafurahisha makafiri mabeberu!!
 
Namshukuru Mungu kwa ushuhuda wa uponyaji kwa mtoto wa Rais Magufuli kadhalika mtoto wa Kiongozi wa Upinzani Bungeni mh Mbowe.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli mtoto wake alitibiwa nyumbani kwa tiba zetu za asili ikiwemo kula malimao, tangawizi na kujifukiza na Mungu wa mbinguni amemponya.

Naye mtoto wa KUB Mbowe ilielezwa kuwa alilazwa hospitali ya manispaa ya Temeke kwa zaidi ya siku 50 na Mungu wa mbinguni amemponya.

Mungu ni mwema wakati wote.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Mungu awape afya njema ndugu zetu
 
Back
Top Bottom