Pole Mhe. Lowassa Kufiwa na mkweo

Ooh!..Kumbee.....Sasa ndio nimefunguka.....Nashukuru BornTown kwa kuweka mambo hadharani. Japokuwa pasco aliomba mtu yeyote asiweke majina halisi au kuweka wazi hizo pole ziende kwa nani ila wewe naona umepuuzia angalizo lake.

Pole Pamella kwa kufiwa na BabaMkwe!,Pole Nakaya kwa kupoteza Baba, Pole EL kwa kufiwa na Mzazi mwenzio, Poleni wana Arumeru na PROEL
 
Wanabodi,
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.

Kwa vile humu jf tuna kikundi chetu kiitwacho PROEL, nawaombeni tumpe pole zetu Mhe. Lowassa!.

Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.

Pole Mzee wetu Lowassa.

Na kwa vile yeye sio member humu, pole zenu mwageni hapa nami nitamfikishia kwa vile nitahudhuria msiba huu mkubwa kwa familia ya Lowassa!


Mkuu Pasco pole sana kwa msiba, mpe pole pia Laigwanani Mkuu. Waambie na PROEL wenzako kuwa tuko pamoja kwenye msiba huo!
 
umesahau kukamilisha utambulisho wake....rais mtarajiwa wa jmt..!

Kazi uliyopewa na el ni kubwa pasco!!

hata dunia igeuke rangi, huyu mtu kamwe hawezi kuwa rais wa hii nchi!its just a matter of time, poleni waganga njaa!
 
watanzania tuna ufinyu mkubwa sana wa mawazo, kama tunawaza kumpa urais mtu ambaye intergrity yake ni questionable basi sijui mungu mnataka asaidie nini, make akili kawapa laikin hamzitumii!huu ni ujinga wa wachache na wanaofaidi na bila kujua ujinga unapenya hadi kwa wengi!tuwe makini sana na hili hasa kwa mtu kama huyu ambaye anadiriki kuhonga kila mtu kuanzia ngazi ya dini, je lengo lake ni nini, yapi ambayo anataka kuyafanya kwa watanzania???jiulizeni sana swali hili na ikumbukwe ngazi ya juu kiserikali kaanza mwaka 1989 mkurugence aicc, alikaa mwaka mmoja tu, kilichomtoa sijui!sasa endelea na ushabiki wenu wa kipuuzi kwa ubinafsi na ukosefu wa uzalendo wenu.

NCHI HAIWEZI KAMWE KUENDELEA KWA KUWA NA WATU WENYE MTAZAMO WA PACCO, NDO MAANA ITAFIKA MAHALA HII NCHI TUTAIKIMBIA, MNATAKA NINI NA MNATOA MFANO GANI NDANI YA JAMII KAMA WATU WENYE UELEWA, MNAOJUA KINACHOENDELEA, MNA ACCESS YA MITANDAO INAYOWASAIDIA KUPATA INFO TOFAUTITOFAUTI BADO HAMUONESHI TOFAUTI NA WATU WALIO KINSHUMUNDU???
 
huyu ndo yule mwenye majibu ya hovyo hovyo !?

Haswaaa!!!! ndiye huyu ulitegemea majibu yenye tija kwa misingi ipi, aliyetakiwa kujibu hoja nzito ya zito kabwe ndiyo hivvyo alikuwa ameshajikatia tamaa ya maisha kwa jinsi maradhi yalivyokuwa yamemzonga. Na hao wataalamu aliokuwa amefuatana nao huko dodoma mawazo yao yote yalikuwa kwenye posho zao wenyewe na jinsi ya kuchakachua zile za wengine through forgery kujiongezea kipato kama alivyofanya JAIRO natimu yake na wala mawazo hayakuwa kwenye kumtafutia waziri majibu yenye tija . mungu ibariki tanzania roho mtakatifu atushukie na kutuongoza ili tusirudie makosa haya 2015
 
Kati ya watu walioifanya hii nchi iwe ka mbao unayoiona nzuri kwa nje ila ndani imeliwa yote na mchwa, ukiigusa tu inaanguka basi ni huyu mtu wenu!bado watu hawaoni kwa sababu zao za kishabiki na ujinga wanatuletea sumu kwa vizazi vya sasa na kumuona ni mtu mwema na mchapakazi ukiuliza kafanya nini hata hawajui, ushabiki tu!eti alikuwa anafukuza
 
Ukiona mtu anamsema anakwambia el ndo anafaa kuwa rais muulize kwa nini then msikilize sababu zake na bado huyo mtu atajiita msomi, nahisi ka huyu ndo msomi wa tanzania kuna kila sababu ya nchi kupotea!
 
Jamani hata dunia iwe ya blue nchi haitaongozwa tena na majambazi tumeamka watanzania!
 
Poleni mlioguswa na msiba wa fisadi mwenzenu Lowassa wenye kugawa hela kama jungu makanisani na misikiti ili awe rais wa Tz,huyu Lowassa ni mwizi mkubwa wa Taifa hili la Tanzania.
 
Mheshimiwa Sumari alikuwa mgonjwa kabla ya kampeni za mwaka 2010 na ilijulikana wazi kabisa pasipo shaka yoyote asingemaliza kipindi chake cha miaka mitano.Nilitegemea Mheshimiwa Sumari angestaafu siasa ili apate muda wa kupambana na ugonjwa wake lakini kwa mshangao wa wengi aliingia ulingoni akahakikisha wanaCCM wenzake wenye afya nzuri hawapati nafasi ya kugombea.

Sehemu kubwa ya kampeni zake zilibebwa na Lowassa na makada wa CCM huku nguvu kubwa ya fedha ikichukua mkondo wake.Tangu achaguliwe hakupata nafasi ya kuwakisha wapiga kura wake kwakuwa hali yake iliendelea kuwa mbaya kama ilivyotarajiwa na wengi.Taifa litaingia hasara ya uchaguzi mwingine hali ambayo ingeweza kuepukika kama sheria na kanuni za uchaguzi zingekuwa zinaangalia afya ya mgombea kama wafanyiwavyo wafanyakazi wanao omba ajira sehemu mbali mbali.

Nawapa pole familia,ndugu jamaa na marafiki wa Mheshimiwa Sumari.



Bado wako wengi!
 
ah ha ha ha...King'asti umelegeza mbavu....Wifi kumbe hata kwa wanaume....BTW Pole kwa Msiba Mh. Lowassa

Kwani lowasa huingia humu? labda kama nowadays zinaiva na nape atamfikishia, manake jengo la vijana eti wa ccm liliwakoroga hawa jamaa ile mbaya!!!!!
 
Though cpendi awe rais bt nampa pole xana coz thts the way we r leading!
 
Mkuu pasco, naamini unaweza kutupa ufaham mpana juu ya kichwa cha uzi huu. mimi nimeelewa kuwa aliyefariki ni mwanamke aliyepata kuzaa mtoto na lowasa, iweke sawa mkuu, naongelea heading.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom