Pole Mhe. Lowassa Kufiwa na mkweo

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Msiba wa Mbunge wa Arumeru, Mhe. Jeremia Solomon Sumari, pia unamhusu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.

Update:
Wanabodi,
Nimepata nafasi kuhudhuria msiba hapa nyumbani kwa Jeremia Sumari.

Kama ilivyo kwa Regia, hapa kwa Sumari ni vivyo hivyo, viongozi wa vyama vya upinzani wameungana na viongozi wa CCM na waombolezaji wengine kuwafariji wafiwa.

Jioni hii, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiongozana na Naibu Katibu Zitto Kabwe wameungana na Mwenyekiti wa UDP Mzew John Cheyo wapo kwa pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali ya JK wakiongozwa na Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa!. na Fredrick Tuluway Sumaye!

Jana rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbrod Slaa wakifika nyumbani hapa kuwafariji wafiwa!.

Mawaziri Wasira, Nchimbi, wabunge wakiongozwa na Katibu wa Bunge Dr Kashilila etc pia wapo!

Ni jambo jema na la kupendeza uonapo ndugu wakikaa pamoja kwa upendo wakati wa shida na raha. Huu ni uthibitisho kuwa licha ya tofauti za kiitikadi, Watanzania tu wamoja kwa upendo na mshikamano miongoni mwetu!.

"Mahali ni Pazuri..Ndugu Wanapokaa...

My Take:
Wanabodi hivi kama ushirikiano, upendo, amani na mshikamano unaofanyika misibani kama ungepelekwa mpaka Bungeni Dodoma, Jee Tanzania tungekuwa wapi?.

Rip Jerry Solomon Sumari!.Thanks kwa Upendo, Amani, Ushirikiano na Mshikamano!

Pasco.
Update:
Ratiba imetolewa.
1. Misa kesho saa 2:00 Msasani Lutheran
2. Saa 5 Mwili kupelekwa Karimjee
kuagwa kitaifa.
3. Mwili kurudi kulala nyumbani.
4. Jumapili asubuhi kusafirishwa kwa ndege kwenda Arusha.
5. Maziko Jumatatu.
 
Wanabodi,
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.

Kwa vile humu jf tuna kikundi chetu kiitwacho PROEL, nawaombeni tumpe pole zetu Mhe. Lowassa!.

Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.

Pole Mzee wetu Lowassa.

Na kwa vile yeye sio member humu, pole zenu mwageni hapa nami nitamfikishia kwa vile nitahudhuria msiba huu mkubwa kwa familia ya Lowassa!

Raisi wetu mtarajiwa anaandamwa na matatizo

alikuwa mdogo wake,sasa tena huyo du

tupo pamoja ktk wakati huu mgumu

R.I.P BABA
ila bado sina chama
naombe ugombea binafsi upite
 
Mkuu PASCO tafadhali sana acha matumizi mabaya ya jukwaa . kama huyo boss wako aliyefiwa na mzazi mwenziye wala huyo aliyekufa siyo member hapa hawastaili kunufaika kwa namna yoyote na jukwaa hili. jukwaa hili ni kwa ajili ya wanachama na kulitumia vinginevyo ni ufisadi kama ufisadi mwingine - Huo ni mtazamo wangu kama member.
 
Pole Pamella kwa kufiwa na BabaMkwe!,Pole Nakaya kwa kupoteza Baba, Pole EL kwa kufiwa na Mzazi mwenzio, Poleni wana Arumeru na PROEL
 
Back
Top Bottom