Pole Mhe. Lowassa Kufiwa na mkweo

Pole Mhe. Lowassa Kufiwa na mkweo

Pasco this is too much,hapa unataka kutuambia nini?unachoki-target wala hutokipata,mambo ya kujipendekeza pendekeza naona yanavuka mpaka sasa,aliefariki ni Sumari wewe unaibuka na EL sijui mna kikundi,kwa hiyo unataka kutuambia mwenye uchungu zaidi ni Lowasa na wala sio wanae marehemu Sumari?kwanini usingeelekeza pole hizi kwa familia ya Sumari?
Tukikwambia humu wewe ni mfuasi wa CCM-magamba unabisha,sasa yako wapi?
Very sorry ni mtizamo wangu

Wee jigoku, tena kila siku ukijiita Msukuma mwenzangu, Msukuma gani wewe mwenye tabia za kike kike?. Mbona wasukuma sio watu wa kujipendekeza pendekeza na kimbelembele kama wale jirani zetu kule juu?. Mijitu mingine kudandia tuu makabila ya watu kwa vile umezaliwa Usukumani?.

Pale nimesema tusitaje taje majina wala hii sio thread ya RIP, ni thread ya kukusanya tuu pole na mimi nimpelekee mzee kuwa hata jf tunamjali. Sasa kimbembele chako cha kutaja majina ndio kujulisha wewe unawajua sana au umetaja majina ili nini?
Tena nakuomba sana ukijibu post yangu yoyote, usithubutu tena kunitaja "Msukuma mwenzangu", sitaki kuniaibisha!
 
Sasa sikumbuki family tree ya kidhungu. Afu m'baba mwenyewe mkubwa hivyo atadumbukiaje kwenye karatasi tu, kha! Mnanchosha!
Tunachosha mi na nani? Zigo ulitwisha na Pasco aje akutue yeye....

Eeh agiza kabisa karatasi maalum mgololo, wee uliona wapi mkaza mwana akaingia kwenye family tree? Asipotoshea kwenye karatasi, pitiliza hadi udongoni
 
Wee jigoku, tena kila siku ukijiita Msukuma mwenzangu, Msukuma gani wewe mwenye tabia za kike kike?. Mbona wasukuma sio watu wa kujipendekeza pendekeza na kimbelembele kama wale jirani zetu kule juu?. Mijitu mingine kudandia tuu makabila ya watu kwa vile umezaliwa Usukumani?.

Pale nimesema tusitaje taje majina wala hii sio thread ya RIP, ni thread ya kukusanya tuu pole na mimi nimpelekee mzee kuwa hata jf tunamjali. Sasa kimbembele chako cha kutaja majina ndio kujulisha wewe unawajua sana au umetaja majina ili nini?
Tena nakuomba sana ukijibu post yangu yoyote, usithubutu tena kunitaja "Msukuma mwenzangu", sitaki kuniaibisha!
Mmmh wasukuma ninaowafahamu wanawaheshimu sana wanawake, sasa wewe kwani ufananishe madhaifu ya mtu binafsi na jinsia ya kike?

Niki question usukuma wako nakosea?
 
Wanabodi,
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.

Kwa vile humu jf tuna kikundi chetu kiitwacho PROEL, nawaombeni tumpe pole zetu Mhe. Lowassa!.

Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.

Pole Mzee wetu Lowassa.

Na kwa vile yeye sio member humu, pole zenu mwageni hapa nami nitamfikishia kwa vile nitahudhuria msiba huu mkubwa kwa familia ya Lowassa!

Mkuu badilisha kauli yako si waziri mkuu mstaafu ni waziri mkuu aliyejiuzulu
 
Pole Pamella kwa kufiwa na BabaMkwe!,Pole Nakaya kwa kupoteza Baba, Pole EL kwa kufiwa na Mzazi mwenzio, Poleni wana Arumeru na PROEL
Born Town nakuomba zingatia
Wanabodi,
Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.
Please ondoa hayo majina!
 
Pasco this is too much,hapa unataka kutuambia nini?unachoki-target wala hutokipata,mambo ya kujipendekeza pendekeza naona yanavuka mpaka sasa,aliefariki ni Mzazi mwenzake wewe unaibuka na EL sijui mna kikundi,kwa hiyo unataka kutuambia mwenye uchungu zaidi ni Lowasa na wala sio wanae marehemu, kwanini usingeelekeza pole hizi kwa familia ya marehemu?
Tukikwambia humu wewe ni mfuasi wa CCM-magamba unabisha,sasa yako wapi?
Very sorry ni mtizamo wangu
zingatia
Wanabodi,
Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.
Please ondoa hayo majina!
 
Pole sana Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa.
 
Mkuu Pasco,

Kila nikisoma haya mabandiko yako ambayo mengi huwa ni ya kujipendekeza kwa wanene huwa najikuta naelekea kuuamini ule uzushi ambao uliwahi kuukana hapa jamvini. Wakati mwingine matendo yako hapa jamvini yanasupport sana ule uvumi!
 
Wana JF, Marehemu anayetajwa hapa ni Mh. Jeremiah Sumari (mbunge)

Mkuu Pasco, jinsi ulivyoileta ni kiajabu sana. Marehemu mwenyewe ni mtu maarufu: Mbunge. Nadhani kama kweli alikuwa mwakilishi wa wananchi watu wa Jimbo lake wangepewa pole wa kwanza. Watoto wake pia ni maarufu akina Nancy Sumari, kwa nini umwelekezee msiba EL??

Kutangaza kifo chake kwa kumuunganisha na Lowasa inasaidia nini sasa?
 
Pole mh. Fisadi nambari wani, na bado wewe.
utakufa utamuacha.kusudi lake la kuwa duniani halijatimia bado
hadi yatimie yale yaliyotabiriwa na kunenwa ndo ataondoka
 
Wanabodi,
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.

Kwa vile humu jf tuna kikundi chetu kiitwacho PROEL, nawaombeni tumpe pole zetu Mhe. Lowassa!.

Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.

Pole Mzee wetu Lowassa.

Na kwa vile yeye sio member humu, pole zenu mwageni hapa nami nitamfikishia kwa vile nitahudhuria msiba huu mkubwa kwa familia ya Lowassa!
(1)Wewe umejuaje kama yeye siyo member???kwani wewe ni Moderator wa JF??
(2)Wewe mbona umemtaja Mh,Lowassa??kwani wengine ndo wanakinga katika thread yako Lowassa hana kinga??
(3)Mashariti hata katika rambirambi!!!
(4)Mimi Hata pole sitoi bado ninaomboleza msiba wa Legia, R.I.P Legia
 
Nilitaka kuuliza hili swali.................Pasco sijui kawaje aisee eti ampelekee pole za wana JF??

Lengo la hii thread bado sijaelewa kabisa
 
Back
Top Bottom