Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 53,246
- 50,468
Ewe mchungaji ama mwinjilist, hiyo posho ungeikataa angalau hayo maswali ungeweza kuyauliza pale pale.
Ndugu wana jf na wa Tanzania kwa ujumla ,leo katika sikukuu hizi za Noel na Mwaka mpya na taka niwapashe yaliyo jili katika jijij la Mwanza .Jana nili bahatika kukutana na January Makamba katika hotel ya Victoria Palace,alitukusanya tulikuwa Wachungaji na Wainjilisti 152 kutoka kakitika madhebu mbalimbali ya kikristo katika mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Mara,na Kagera.Kikao kilianza saa mbili na dakika hamsini na tisa usiku na kumalizika saa tano na dakika ishilini na tatu usiku.Katika kikao hicho January alikuwa amevalia suti yake nyeusi na shati nyeupe ikiambatana na tai nyekundu, kweli kijana ulipendeza kwa vazi hilo cha kunisiki tisha ni pale ulipo anza kujifananisha na nabii Yeremia,nilikusikiliza ukisoma kitabu cha Yeremia moja na kwamba kwa maneno yaliyomo katika kitabu hicho yanakushawishi kutangaza nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 vivyo unatuomba sisi watumishi wa Bwana tukuunge mkono na tuwashawishi waumini wetu pia.Ndugu January nikweli unashauku ya kuwa Raisi wa Tanzania lakini naomba nikuulize kupitia waraka huu maswali yafuatayo
1. Watanzania wameshuudia chama chako kupitia wabunge wake mkimzushia mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani kwamba alifanya siasa za udini kwa kukutana na watumishi wa Bwana kule Arusha ,sasa hiki ulicho kifanya jana ni Kuharalisha udini au ulikuwa unabadili dini?.
2.Mfuasi wako uliye mtuma kuandaa kikao hicho,Bwana Mustafa kada wa chama cha mabinduzi nikati ya watuhumiwa ,wa mipago hovu ya kuandaa vijana waliyo kwenda na nia ya kudhuru kule Kigoma hivi majuzi sasa nikuulize unapata wapi mamlaka ya kimahadili ya kuandaliwa kikao na mtuhumiwa wa utesi tena kikao na watumishi wa Bwana uoni kwamba unamsanifu Mungu?.
3.Ulitupatia posho ya shillingi elfu hamsini kwa kila mmoja wetu,ulitupatia chakula na vinywaji ,ulitukodishia hoteli, ulitukudishia gari aina ya costa no T926 BDP mali ya bwana Mukeshi ambayo ndiyo ili beba mabaunsa wa Matata kwenda Kigoma hivi majuzi,gharama zote ni takribani millioni ishilini tunashukuru lakini tujiulize,hizo pesa za kutuonga ulipata wapi?,kwanini unataka kununua Uraisi?,Je kwa pesa hiyo unge chonga madawati mangapi kwa ajili ya watoto wanao kaa chini uko Bumbuli? na je unafikili kutuonga sisi utakuwa umewaonga na waumini wetu?.
4.Wewe ni mshilika wa Bwana Rowasa,ambaye pia anakiu ya Uraisi kama wewe lakini pia wewe pia ni mshilika wa Ngeleja ambaye pia kiu ya Uraisi sasa niku ulize tumpigie debe nani kati yenu? ,au mnatafuta kura za sambusa yaani wawili tujitoe mmoja apite?.
5.Umelifanyia nini taifa mpaka uone unaweza kuwania Uraisi,wakati suala la tozo za simu ambalo ni mzigo wa dhambi kwa wananchi,limekushinda ukiwa kama naibu waziri wa wizara usika au una maslahi na makampuni ya mawasiliano,kama sivyo uoni ukiwa Raisi utaleta na kodi ya kusikiliza redio.
6.Unalisemeaje suala la operationi tokomeza ujangili ambayo imetesa na kuuwa wasiyo na atia wakati watuhumiwa wa ujangili akiwemo kinana katibu mkuu wa chama chako bado wana kula bata?.
7'Tuambie nini kimekushawishi kuwa na nia ya kuwa Raisi?.
8.Tuambie nikiongozi ghani wa upinzani unaona anaweza kuwa Raisi kama wewe utopata fursa ya kuwania uraisi?.
9.Kunatetesi kuwa wewe na baba yako mlishiliki kumuondoa Sherukindo kwenye nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Bumbulina kukupitisha wewe bila kupingwa kwenye CCM,Sherukindo aliye kuwa mwenyekiti wa kamati yakudumu ya Bunge ya nishati na madini ambaye alisimama kidete juu ya kashfa ya Rich mond iliyo muondoa Rowasa kwenye kiti cha uwaziri mkuu,ambaye ni swahiba mkubwa kabisa wa Mzee Makamba baba yako aliye kuwa katibu mkuu wa CCM?[Comflictof interest] leo ukifanikiwa kuwa raisi si utatengeneza mamlaka ya kifamilia?.
10.Nikumbushe ile divishion four ya formu six kule kigoma uli isafisha lini?.Au na wewe ni muhumini wa division five
11.Niambie leo unawambia nini wa endesha boda boda wa Mwanza au unaomba day waka?.
Mwisho jipime
Wewe mchungaji ni mnafiki sana tena sana na sijui una chunga kondoo gani?
hivi haya maswali kwa nini haukumuuliza mlipokuwa pamoja kama wewe ni msema kweli?
Ukimsoma huyu so called mchungaji utagundua ni mwana siasa wa chadema kwa maneno yake na anajificha kwa kujifanya hawajui viongozi wa upinzani heti anasema kiongozi fulani wakati anamjua kabisa jina.
Wewe mchungaji acha siasa.
Tunajua umetumwa kusafisha tuhuma na unatakiwa kujua tuhuma hazisafishwa kwa tuhuma.
HAPA HAKUNA MCHUNGAJI BALI NI MWANA MWANA SIASA.
HII HABARI INA UONGO MWINGI SANA.
Mtoa mada ni muongo na amebainisha jinsi gani yeye ni pandikizi aliye kazini kumchafua January kwa manufaa ya watu anaowajua yeye. Huyu hawezi kuwa ni mtu wa Mungu aliyeandika haya. Kama alikuwapo kwenye kikao hicho, basi anadanganya kwa makusudi au hakuhudhuria kabisa kwahiyo ametunga ya kwake baada ya kuhadithiwa machache.
Mimi nilikuwapo katika mkutano huo na naweza hata kukuleteeni sauti ya hotuba yenyewe ili msikilize uwongo uliomwagwa hapa. Kimsingi maaskofu walimualika kuwahutubia kuhusu changamoto za Kitaifa na juu ya uongozi unaohitajika kupambana na changamoto hizo. Hakuna yoyote aliyepewa pesa na January katika mkutano huo. Hakuna.
Hakuna sehemu ambapo January aliwaomba maaskofu wamuunge mkono kugombea urais. Mambo aliyozungumzia ni kuhusu "inequality" katika jamii (yaani tofauti kati ya maskini na matajiri), kuhusu nyufa za kitaifa alizoongelea Nyerere miaka 20 iliyopita, kama rushwa, udini, uzanzibari na uzanzibara. Alizungumzia pia kuhusu kumomonyoka kwa maadili na kushamiri kwa uwongo, utapeli, ubakaji, wizi na mauaji katika jamii yetu, na jinsi gani viongozi wa dini wanavyofanya kazi kubwa kupambana na haya, na jinsi gani wanahitaji kusaidiwa na viongozi wa serikali.
Alisema kwamba kama Taifa tunahitaji uponyaji. Akasema katika uponyaji huo viongozi wa dini wana nafasi kubwa, kama viongozi wa kisiasa, hivyo lazima washirikiane. Akasema ili nchi ipone, lazima viongozi wa dini na wa kisiasa wawe wasafi na "wasipende kulamba sukari". Asema uongozi wa nchi hauna umri, alipotumia mfano wa Yeremia kwamba aliaminiwa na Mungu katika umri mdogo kuwa kiongozi. Haina maana kwamba alijifananisha naye. Alimaanisha tu kwamba hata vijana wanauwezo wa kuongoza na waaminiwe. Alimaliza kwa kusema japo tumefikisha miaka 50 ya Tanzania, safari yetu ya kujenga nchi ndio kwanza imeanza, lakini ili kupambana na changamoto zilizopo, nchi inahitaji kufanyiwa "reset" ili kujengwa upya na kizazi kipya.
Maneno yake yote yalikuwa na ushawishi mkubwa, hasa pale alipotumia mistari ya Biblia kujenga hoja zake. Imemuonyesha mbele ya viongozi hawa wa dini jinsi gani January ni kiongozi ambaye ni mcha Mungu, asiye mdini, anayekubalika na dini zote na aliyetayari kushirikiana na viongozi wa ngazi zote za jamii ili kupata majawabu ya changamoto zinazotukabili.
Basi wewe huwajui maaskofu kama kweli una-doubt wanaweza kumualika mwanasiasa. Sio jambo la ajabu kwa wao kuwa na round-table discussions na viongozi wa kisiasa kwa vile nao ni sehemu ya jamii. Tatizo ni pale kikaragosi anakuja hapa JF na kudai kwamba maaskofu wamepewa rushwa, ya tena elfu 50,000 wakati hakuna ukweli wowote. Hilo ni tusi kubwa kwa maaskofu wetu kuliko kwa January Makamba ambaye ndiye mlengwa wa tusi hilo.
Hakuna mchungaji mnafiki kama wewe.
kama ulivyojipambanua wewe ni mchungaji na ulihudhuria. Embu weka jina lako kamili mtu wa Mungu la sivyo na wewe nitakuwaka katika kundi lileee.......... Maana kama kiongozi wa dini utapitia mlango wa uani nani atapitia mlango wa mbele. Pili kwa nini wewe hukutoa taarifa mapema kuwa kuna kitu kama hicho? Nadhani na wewe una kitu unaficha ila katika maelezo yako ya mwisho inaonyesha ni kwa jinsi gani unampigia debe dogo
Tena aeleze kwanini alimwambia Pinda kuwa kiwanda cha chai - Bumbuli hakiwezi kufanya kazi hata angekuja rais? kwanini anadhani akianzisha yeye ushirika wa wakulima wa chai utafaa kuliko ule ulioanzisha na baba pamela (makai) aka shelukindo?
Kwanini halmashauri mpya ya bumbuli inaitwa halmashauri ya wilaya wakati hakuna wilaya inaitwa bumbuli?
MKAMA6 i-join kwenye thread pale juu
Mtoa mada ni muongo na amebainisha jinsi gani yeye ni pandikizi aliye kazini kumchafua January kwa manufaa ya watu anaowajua yeye. Huyu hawezi kuwa ni mtu wa Mungu aliyeandika haya. Kama alikuwapo kwenye kikao hicho, basi anadanganya kwa makusudi au hakuhudhuria kabisa kwahiyo ametunga ya kwake baada ya kuhadithiwa machache.
Mimi nilikuwapo katika mkutano huo na naweza hata kukuleteeni sauti ya hotuba yenyewe ili msikilize uwongo uliomwagwa hapa. Kimsingi maaskofu walimualika kuwahutubia kuhusu changamoto za Kitaifa na juu ya uongozi unaohitajika kupambana na changamoto hizo. Hakuna yoyote aliyepewa pesa na January katika mkutano huo. Hakuna.
Hakuna sehemu ambapo January aliwaomba maaskofu wamuunge mkono kugombea urais. Mambo aliyozungumzia ni kuhusu "inequality" katika jamii (yaani tofauti kati ya maskini na matajiri), kuhusu nyufa za kitaifa alizoongelea Nyerere miaka 20 iliyopita, kama rushwa, udini, uzanzibari na uzanzibara. Alizungumzia pia kuhusu kumomonyoka kwa maadili na kushamiri kwa uwongo, utapeli, ubakaji, wizi na mauaji katika jamii yetu, na jinsi gani viongozi wa dini wanavyofanya kazi kubwa kupambana na haya, na jinsi gani wanahitaji kusaidiwa na viongozi wa serikali.
Alisema kwamba kama Taifa tunahitaji uponyaji. Akasema katika uponyaji huo viongozi wa dini wana nafasi kubwa, kama viongozi wa kisiasa, hivyo lazima washirikiane. Akasema ili nchi ipone, lazima viongozi wa dini na wa kisiasa wawe wasafi na "wasipende kulamba sukari". Asema uongozi wa nchi hauna umri, alipotumia mfano wa Yeremia kwamba aliaminiwa na Mungu katika umri mdogo kuwa kiongozi. Haina maana kwamba alijifananisha naye. Alimaanisha tu kwamba hata vijana wanauwezo wa kuongoza na waaminiwe. Alimaliza kwa kusema japo tumefikisha miaka 50 ya Tanzania, safari yetu ya kujenga nchi ndio kwanza imeanza, lakini ili kupambana na changamoto zilizopo, nchi inahitaji kufanyiwa "reset" ili kujengwa upya na kizazi kipya.
Maneno yake yote yalikuwa na ushawishi mkubwa, hasa pale alipotumia mistari ya Biblia kujenga hoja zake. Imemuonyesha mbele ya viongozi hawa wa dini jinsi gani January ni kiongozi ambaye ni mcha Mungu, asiye mdini, anayekubalika na dini zote na aliyetayari kushirikiana na viongozi wa ngazi zote za jamii ili kupata majawabu ya changamoto zinazotukabili.
Tunakujua sana kwa mabandiko yako humu. Unaendeshwa pia na itikati ileee!
ant you sayng January was invited in Mwanza ha ha you must be frustrated some one spilled the beans ,January the alleged corrupt he should visit JF and tell the truth
There no secrecy in this global, January must know. In fact we thank the pastor to reveal Jan's corruption. One thing I know, God will not allow weaked persons to govern this country.
Wamarekani wanataka Makamba Jr awe Rais, wanaamini chini ya Makamba Jr Masilahi yao yatakuwa salama...Fedha za kumuwezesha tayari zipo...
hatua ya kwanza imepingwa kwa hiyo ni kweli makamba alikuwa mwanza na aliongea na maaskofu..
Hatua ya pili tunaomba ulete hapa mwaliko kutoka kwa maaskofu kwenda kwa bwana makamba.
Hatua ya tatu tuwekee hiyo sauti ya makamba akiwa anaongea na maaskofu
asante
Angemuuliza kulekule, wapiga kura tungejuaje?Mtoa mada,,,haya unayoyauliza hapa ulikosa wasaa wa kumuuliza????ulijua unahongwa ukapokea????Januari ana ukurasa wake wa fb,tweeter,nenda kamuulize,,,,nyie viongoz wa kidini ni wanafki tu,unataka tujue kuwa ulikua na Januari???mxiuuuuuuuu
halafu wapiga kura tungejuaje kama kuna mtu anataka kununua kutuongoza?bado tuna safari ndefu sana maana sijui hata hayo makosa ya matumizi sahihi ya lugha tatizo ni shule au nini? pia umefanyiwa yooote then unakuja kumuuliza maswali huku si bora ungeomba namba yake ya simu.