ze jackal
JF-Expert Member
- Nov 13, 2013
- 528
- 174
aheee mama weee ungekua wewe ungefanyajeee!!!!
Makamba Jr kalala chini,wainjilisti kitandani.
Akihamia kitandani basi ajue mzungu wa nne.
aheee mama weee ungekua wewe ungefanyajeee!!!!
Wamarekani wanataka Makamba Jr awe Rais, wanaamini chini ya Makamba Jr Masilahi yao yatakuwa salama...Fedha za kumuwezesha tayari zipo...
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa
Hakuna mchungaji mnafiki kama wewe.
ahsante mwanachama feki CCM 2015 watakabidhi nchi watake wasitakekwakua Chama changu CDM hakijajipanga kuchukua nchi, mtu makini toka CCM ni January Makamba.
Wengine tusingejua kuwa bwana mdogo anafitinisha watu.
Mungeongeza dau ange ficha siri lakini shllingi 50,000 kama walivyzoe kuhonga masalia wchungaji bei yao kubwa mutayatolea mapepo ya uchu na uroho wa madaraka kwenye mitandao January ana najisi IKULU inatosha alivyokaa pale kama speech writer but not as presidentHakuna mchungaji mnafiki kama wewe.
Mkuu we ni mnafiki ulishindwa nin kuhoji huko hotelini. BTW ni haki ya kikatiba kwa January kugombea urais kwani tatizo ni nini?
Go Makamba.
Ndio aje ajibu January Makamba anataka uraisi sasa hivi anajua hata katiba itaamua nini wanaendekeza libeneke la uroho wa madaraka kwa sababu wanadhani kwa vile alipachikwa ubunge na baba yake na uraisi atapachikwa mambo ya hovyo kabisa awe raisi wa nani juzi hapa kamfuta uenyekiti mwenyekiti wa kijiji kwa kumtishia kumuua ili mradi alichaguliwa na wananchi wote kupitia chademaany way the way alivyoeleza ni kinafki,,,haya maswal ameyaelekeza kwa januari,na jana alikua nae hotelini
Mtoa mada ni muongo na amebainisha jinsi gani yeye ni pandikizi aliye kazini kumchafua January kwa manufaa ya watu anaowajua yeye. Huyu hawezi kuwa ni mtu wa Mungu aliyeandika haya. Kama alikuwapo kwenye kikao hicho, basi anadanganya kwa makusudi au hakuhudhuria kabisa kwahiyo ametunga ya kwake baada ya kuhadithiwa machache.
Mimi nilikuwapo katika mkutano huo na naweza hata kukuleteeni sauti ya hotuba yenyewe ili msikilize uwongo uliomwagwa hapa. Kimsingi maaskofu walimualika kuwahutubia kuhusu changamoto za Kitaifa na juu ya uongozi unaohitajika kupambana na changamoto hizo. Hakuna yoyote aliyepewa pesa na January katika mkutano huo. Hakuna.
Hakuna sehemu ambapo January aliwaomba maaskofu wamuunge mkono kugombea urais. Mambo aliyozungumzia ni kuhusu "inequality" katika jamii (yaani tofauti kati ya maskini na matajiri), kuhusu nyufa za kitaifa alizoongelea Nyerere miaka 20 iliyopita, kama rushwa, udini, uzanzibari na uzanzibara. Alizungumzia pia kuhusu kumomonyoka kwa maadili na kushamiri kwa uwongo, utapeli, ubakaji, wizi na mauaji katika jamii yetu, na jinsi gani viongozi wa dini wanavyofanya kazi kubwa kupambana na haya, na jinsi gani wanahitaji kusaidiwa na viongozi wa serikali.
Alisema kwamba kama Taifa tunahitaji uponyaji. Akasema katika uponyaji huo viongozi wa dini wana nafasi kubwa, kama viongozi wa kisiasa, hivyo lazima washirikiane. Akasema ili nchi ipone, lazima viongozi wa dini na wa kisiasa wawe wasafi na "wasipende kulamba sukari". Asema uongozi wa nchi hauna umri, alipotumia mfano wa Yeremia kwamba aliaminiwa na Mungu katika umri mdogo kuwa kiongozi. Haina maana kwamba alijifananisha naye. Alimaanisha tu kwamba hata vijana wanauwezo wa kuongoza na waaminiwe. Alimaliza kwa kusema japo tumefikisha miaka 50 ya Tanzania, safari yetu ya kujenga nchi ndio kwanza imeanza, lakini ili kupambana na changamoto zilizopo, nchi inahitaji kufanyiwa "reset" ili kujengwa upya na kizazi kipya.
Maneno yake yote yalikuwa na ushawishi mkubwa, hasa pale alipotumia mistari ya Biblia kujenga hoja zake. Imemuonyesha mbele ya viongozi hawa wa dini jinsi gani January ni kiongozi ambaye ni mcha Mungu, asiye mdini, anayekubalika na dini zote na aliyetayari kushirikiana na viongozi wa ngazi zote za jamii ili kupata majawabu ya changamoto zinazotukabili.