Pole January Makamba

Pole January Makamba

Kama ulikuwa kwenye hicho kikao si ungemuuliza hayo maswali?kama sio unafiki ni nini..

Tena unafiki wenyewe ni wa ushuzi wa mavi hata uutoe polepole utanuka anaaacha kumuuliza mwenyewe analeta ushambenga humu
 
Makamba nae anataka tutuongoza watanzania? sasa nadhani taasisi ya raisi ni kama mchezo vile! .... makamba kwa mtazamo wangu, muda wako wa kufikilia uraisi bado sana, huna hata wizara uliyoongoza leo unataka nchi? nadhani bado ndani ya CCM wako watu wengi wenye sifa, ungana nao
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa

N kwel mkuu huyu jamaa n mnafk... posho kachuka af bado ana disi... af n kiongoz wa dhehebu.
 
mkama6.
Wewe ndugu yangu ni mchungaji wa watu au unachunga nini? Kwanini wachungaji mmekubali kuhongwa na January huku mkijua kupokea rushwa ni dhambi kubwa mbele za Mungu? Kilichokufanya usihoji haya maswali yako ya chuki na kinafiki mbele ya January ni nini mpaka uje huku jf kwa id za uchochoroni? Ninani amekuambia Shelukindo alikuwa na msaada wowote kwa watanzania hasa huko jimboni kwetu alikokuwa mbunge kwa miaka kumi na tano? Unapajua Bumbuli au unaandika tu ili kutimiza lengo lako ovu la kumchafua january makamba. Unajua Bumbuli kwasasa kuna miradi kadhaa inayowanufaisha wanawake na vijana kwa ujumla na ameinzisha ndugu JMakamba. Je unafahamu kuwa Bumbuli ipo njiani kuwa na tawi la benki ya NMB na jengo la tawi hilo ndio linaelekea mwisho na yote kayafanya January Makamba? Unasema kodi ya simu kashindwa kushughulikia tatizo kweli upo Tanzania hii au ndio hawa kina MM ambao hurushia makombora yaoya kinafiki kutoka nje? Hujui kuwa kodi ya simu iliyokuwa imeelekezwa kwa wananchi kuchangia kila mmoja 1000/= imefutwa na kuhamisha kwenye makampuni ya simu za mikononi? Unafiki huo uliouleta hapa unakusaidia nini wewe unaejita muinjilisti/askofu? Kumbe kwenye mafunzo yenu siku hizi mnafundishwa kuongea uongo? Pole sana hata ivo umefeli kabla hata hujaandika upu.uzi wako hapa. Kajipange tena au rudi huko kwenye mafunzo yenu ili ukajifunze jinsi ya kufanya majungu na propaganda.

Kumbe CHAMVIGA ni wa bumbuli ha ha ha naona povu lina kutoka kumtetea mghosi wa kaya......komaaa hivyo hivyo 2015 makamba akiwa rais utapata u DC......Ila nakubaliana na wewe kitu kimoja tu kwa jinsi januari anavyo ipigania bumbuli tofauti sana na shelukindo siku atleast ukiwa bumbuli utajihisi uko duniani maendeleo yana anza kuonekana kwa effort za makamba junior...hayo mengine ya kuhonga wachungaji mtajuana wenyewe...
 
Last edited by a moderator:
sina shaka kuwa alichokisema ndugu alinda ni uongo tena uongo mtupu! Kanda ya ziwa pekee haina maaskofu 152 vinginevyo kama anadhani kila kiongozi wa dini ya kikristo ni askofu!

Ujinga ni mzigo unaoelemea sana! amesema walikuwepo na wainjilisti.

wewe unajua kusoma lakini hujui kuelewa.
 
January makamba ni mtu anayeabudu sana rushwa.
ana umri mdogo kuliko pesa alizonazo. kwa umri wake akithibitisha kazi/biashara halali iliyompatia haya mapesa itakuwa ajabu la dunia.

Tuvunje utamaduni unaoanza kukomaa wa wananchi watoa rushwa kupitishwa kugombea nyadhifa za uongozi.

Rais Kikwete anawajibika kupeleleza, akibaini ukweli wa hili jambo ampoke unaibu waziri aliomzawadia huyu muumini wa rushwa. Ubakie upofu wa wana bumbuli kwenye ubunge wao.

NAMPIGA MUHURI JANUARY MAKAMBA KWENYE PAJI LA USO WAKE UKISOMEKA "HUYU NDIYE KIONGOZI MKUU WA RUSHWA KWA KUPOKEA NA KUTOA"
 
wanaomtete huyo kilaza makamba ni uvccm walihongwa simu kumtetea kwenye mitandao ya kijamii.....makamba hana sifa ya kuwa rais,what did he run to show up the society that he can????hapo alipo haja hasle kasaidiwa na baba yake mzee makamba kwa kutumia ukatibu mkuu kujinufaisha na familia yake,you cant compare him na vijana kama mnyika,lema,filikunjombe etc
 
Tena unafiki wenyewe ni wa ushuzi wa mavi hata uutoe polepole utanuka anaaacha kumuuliza mwenyewe analeta ushambenga humu

Hebu nikuulize wewe zuzu....Bila ya yeye kumwaga hapa ukweli wote mimi ningejuaje kama January Makamba anataka kununua viongozi wa dini?
 
Ndugu wana jf na wa Tanzania kwa ujumla ,leo katika sikukuu hizi za Noel na Mwaka mpya na taka niwapashe yaliyo jili katika jijij la Mwanza .Jana nili bahatika kukutana na January Makamba katika hotel ya Victoria Palace,alitukusanya tulikuwa Wachungaji na Wainjilisti 152 kutoka kakitika madhebu mbalimbali ya kikristo katika mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Mara,na Kagera.Kikao kilianza saa mbili na dakika hamsini na tisa usiku na kumalizika saa tano na dakika ishilini na tatu usiku.Katika kikao hicho January alikuwa amevalia suti yake nyeusi na shati nyeupe ikiambatana na tai nyekundu, kweli kijana ulipendeza kwa vazi hilo cha kunisiki tisha ni pale ulipo anza kujifananisha na nabii Yeremia,nilikusikiliza ukisoma kitabu cha Yeremia moja na kwamba kwa maneno yaliyomo katika kitabu hicho yanakushawishi kutangaza nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 vivyo unatuomba sisi watumishi wa Bwana tukuunge mkono na tuwashawishi waumini wetu pia.Ndugu January nikweli unashauku ya kuwa Raisi wa Tanzania lakini naomba nikuulize kupitia waraka huu maswali yafuatayo

1. Watanzania wameshuudia chama chako kupitia wabunge wake mkimzushia mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani kwamba alifanya siasa za udini kwa kukutana na watumishi wa Bwana kule Arusha ,sasa hiki ulicho kifanya jana ni Kuharalisha udini au ulikuwa unabadili dini?.

2.Mfuasi wako uliye mtuma kuandaa kikao hicho,Bwana Mustafa kada wa chama cha mabinduzi nikati ya watuhumiwa ,wa mipago hovu ya kuandaa vijana waliyo kwenda na nia ya kudhuru kule Kigoma hivi majuzi sasa nikuulize unapata wapi mamlaka ya kimahadili ya kuandaliwa kikao na mtuhumiwa wa utesi tena kikao na watumishi wa Bwana uoni kwamba unamsanifu Mungu?.

3.Ulitupatia posho ya shillingi elfu hamsini kwa kila mmoja wetu,ulitupatia chakula na vinywaji ,ulitukodishia hoteli, ulitukudishia gari aina ya costa no T926 BDP mali ya bwana Mukeshi ambayo ndiyo ili beba mabaunsa wa Matata kwenda Kigoma hivi majuzi,gharama zote ni takribani millioni ishilini tunashukuru lakini tujiulize,hizo pesa za kutuonga ulipata wapi?,kwanini unataka kununua Uraisi?,Je kwa pesa hiyo unge chonga madawati mangapi kwa ajili ya watoto wanao kaa chini uko Bumbuli? na je unafikili kutuonga sisi utakuwa umewaonga na waumini wetu?.

4.Wewe ni mshilika wa Bwana Rowasa,ambaye pia anakiu ya Uraisi kama wewe lakini pia wewe pia ni mshilika wa Ngeleja ambaye pia kiu ya Uraisi sasa niku ulize tumpigie debe nani kati yenu? ,au mnatafuta kura za sambusa yaani wawili tujitoe mmoja apite?.

5.Umelifanyia nini taifa mpaka uone unaweza kuwania Uraisi,wakati suala la tozo za simu ambalo ni mzigo wa dhambi kwa wananchi,limekushinda ukiwa kama naibu waziri wa wizara usika au una maslahi na makampuni ya mawasiliano,kama sivyo uoni ukiwa Raisi utaleta na kodi ya kusikiliza redio.

6.Unalisemeaje suala la operationi tokomeza ujangili ambayo imetesa na kuuwa wasiyo na atia wakati watuhumiwa wa ujangili akiwemo kinana katibu mkuu wa chama chako bado wana kula bata?.

7'Tuambie nini kimekushawishi kuwa na nia ya kuwa Raisi?.

8.Tuambie nikiongozi ghani wa upinzani unaona anaweza kuwa Raisi kama wewe utopata fursa ya kuwania uraisi?.

9.Kunatetesi kuwa wewe na baba yako mlishiliki kumuondoa Sherukindo kwenye nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Bumbulina kukupitisha wewe bila kupingwa kwenye CCM,Sherukindo aliye kuwa mwenyekiti wa kamati yakudumu ya Bunge ya nishati na madini ambaye alisimama kidete juu ya kashfa ya Rich mond iliyo muondoa Rowasa kwenye kiti cha uwaziri mkuu,ambaye ni swahiba mkubwa kabisa wa Mzee Makamba baba yako aliye kuwa katibu mkuu wa CCM?[Comflictof interest] leo ukifanikiwa kuwa raisi si utatengeneza mamlaka ya kifamilia?.

10.Nikumbushe ile divishion four ya formu six kule kigoma uli isafisha lini?.Au na wewe ni muhumini wa division five

11.Niambie leo unawambia nini wa endesha boda boda wa Mwanza au unaomba day waka?.

Mwisho jipime

Hizi ni nyakati za Mwisho na ww ni mtumishi wa mungu...umekula takrima na unafanya majungu
 
Mwanza. Katika kile kinachoonekana kama kujipigia debe katika kinyang'anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewaambia viongozi wa dini Kanda ya Ziwa kwamba vijana wanapofika kuomba ridhaa yao, muwaangalie, msiwabeze.

Huku akikataa kuweka bayana nia yake ya kuwania urais kwa maelezo kwamba muda wa kufanya hivyo haujawadia, Makamba aliwaambia viongozi hao wa dini kwamba wagombea hao wanapopita wawasomee sifa za uongozi katika Biblia na kusema kumekuwapo mjadala wa sifa za uongozi kuhusu kijana na kusema amekuwa akitoa mwito kwa vijana wasiokuwa na makandokando kushiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.

Akizungumza juzi usiku mjini hapa katika chakula cha pamoja na maaskofu na wachungaji kutoka Umoja wa Makanisa ya Kikristo wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema: "Huu ni wakati wa kila mmoja kutafakari hatima ya nchi yetu. Ndugu zangu… nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu sote ni Watanzania na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu."

Alisema vijana wengi wamekuwa waoga kwa madai kwamba hawana fedha, uzoefu lakini akasema maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo.

"Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimi mdogo mimi siwezi, lakini Mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) …. Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa," alisema na kuongeza:

"Bwana alimwambia usiseme, mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe."

Alisema Tanzania inapita katika kipindi kigumu, hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuongoza maombi yatakayoiwezesha kupata kiongozi mwenye sifa ya kuivusha katika kipindi hicho.

Makamba amesema nchi inakabiliwa na nyufa kama vile rushwa, udini, ukabila, Uzanzibari na Uzanzibara, huku akirejea hotuba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya Machi 1995, ambayo aliyataja mambo hayo kuwa nyufa zinazoweza kuliangamiza taifa.

Alisema Tanzania inahitaji uponyaji na ikibidi kuanza upya kwa maana ya aina ya uongozi unaohitajika hivi sasa na kwamba ili kutimiza lengo hilo, viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutafakari na kuielekeza nchi njia sahihi ya kufuata.

"Shughuli za siasa zimeingiliwa na matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingiliwa na matapeli. Sasa tunapotafuta uponywaji wa nchi yetu ninyi mna nafasi kubwa kwani uponyaji tunaouzungumzia ni wa maovu ya kiroho, uongo, ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mna nafasi kubwa sana," alisema.

Alisema viongozi wa kisiasa pia wanayo nafasi yao katika kuponya taifa lakini lazima wanapofanya kazi hiyo wawe wasafi.

Alisema askofu au mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
SOURCE: MWANANCHI

 
Naomba kuuliza hivi umri wa kugombea URAIS kwenye katiba mpya umependekezwa miaka mingapi?

Nijuavyo katiba ya sasa inasema mgombea URAIS wa JMT lazima awe na 42+ years. Huyu January Makamba hajafikisha huo umri.

Kama ameanza KUHONGA sasa hivi anajuaje kwenye katiba mpya UMRI utateremushwa? Au Katiba tayari CCM wanayo MFUKONI.

Mleta uzi tunakushukuru sana kwa kuleta habari hii, vinginevyo tusingeweza kufahamu madudu ya January Makamba.

Nafahamu amewapatia UVCCM laptop za kumtetea na kuitetea CCM mitandaoni, lakini always mafuta na maji havikai pamoja. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio na asikie
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa
Kuna tatizo??? Nadhan hakuna tatizo kuuliza maswali hayo humu ndani, Makamba na viongozi wengine wengi wamekuwa wakiulizwa humu na kutoa majibu humu humu. Sioni dhambi yoyote hapa.
 
Back
Top Bottom