Ilipoishia... .
..Kizungu zungu kikanitawala hapo
hapo nakupoteza fahamu hapo
hapo...
'
Endelea...
Nilishtuka nakushangaa mwili wangu wote
umelowa maji hivyo akili yangu ikafanya kazi
nakujua kumbe yule mtu aliyenileta huku bafuni
ndiye aliyenimwagia maji pale nilipohisi kizungu
zungu nakuanguka mpaka chini..
"...amka hukoo..? Amkaa husikii..?" yule mtu bado aliendelea kunifokea nakujikuta
nikiamka kwa kupepesuka, lakini ile nainuka tu
nguvu zikaniishia nakujikuta nandondoka tena
mpaka chini kabisa..
Niliinuliwa na yule mtu kwa nguvu huku
akinishambulia kwa vibao pamoja na mangumi mwili wangu wote, nakilichofuata alinivuta nywele
zangu mpaka mlango wakutokea, sikuwa na sauti
kwani ilishanikauka, mwili wangu sasa ulikuwa
kama uliyepigwa ganzi kutokana na maumivu
kupitiliza.
Yule mtu aliendelea kuniburuza mpaka getini huku nikiwa uchi tena mtupu kama nilivyozaliwa, aliacha
kunivuta kwa kutumia nywele zangu na safari hii
alikuwa kayashikilia matiti yangu yote mawili huku
akiyaminya nakuyavuta kwa nguvu zake zote
mpaka nje ya geti..
Masikio yangu yakawa kama yananasa sauti za watu huku macho yangu yaliyojawa na ukungu
wa maji uliochanganyika na zile damu zangu
yakikosa nguvu yakujua ni wakina nani
ninaowasikia, nikajaribu kupiga kelele kama sauti
itatoka..
"..nisaidieni jamani, niokoeni nakufa mie.." Nikahisi kama sauti imetoka tena kwa nguvu
mpaka mwili ukanisisimka, haraka haraka
nikapikicha macho yangu yakapata uwezo
wakuona mbele,
"..Ahsante sana Mwenyezi Mungu kwa kunionesha
tena duniani.." Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiuangalia ule
umati wa watu uliokuwa umetanda na
kunishangaa nikiwa uchi wa mnyama.
Niliinuka pale chini nakurudi mpaka ndani ambapo
breki yakwanza ilikuwa kwenye kinyumba cha
mlinzi napo sikumkuta, nikachukua bunduki lake na panga kisha nikaingia mpaka ndani kwa hasira,
nilipofika sebuleni nilizikuta zile damu zangu
zimetapakaa mpaka kwenye masofa, nikaingia
vyumbani chumba kimoja kimoja nikifungua bila
kumuona mtu yeyote mpaka nikafikia chumba
kilichokuwa kimelokiwa, nikatumia lile gobole kuvunja, ile namalizia tu
nageuka nyuma namuona Jerry akiwa na John
pamoja na baba Latifah wakinifuata huku
wakicheka.
Kwa hasira niliyokuwa nayo nikachukuwa lile
bunduki nakuwaelekezea huku nikitaka kuwafyatua mara.. **** "...Aaah.., aah.., wanabahati kweli..?, uuhf..! Uuuf..!
Uuuf..!"
Niliropoka kwa sauti ya juu na ya ukali huku
nikikodoa macho huku nakule kwa mshangao
ulioambatana nakuhema juu juu mpaka jasho
likanitoka huku nikiwa kitandani nisiamini kilichotokea kama ni ndoto..
Haraka haraka niliwasha taa nakuangaza chumba
chote kulikuwa kimya hivyo nikaamini nilikuwa
naota.
Na wakina Aisha watakuwa waliniacha wameenda
'club bills'.. Nilianza kupata kumbukumbu sawa
nakukumbuka mara ya mwisho nilimwambia Aisha
aniache nipumzike kidogo halafu ndio twende nao
huko 'club' nadhani hawakuniamsha hivyo
nikapitiwa na usingizi nakuanza kuota ndoto za
ajabu ajabu eti nimeteswa na baba Latifah wakisaidiana na John pamoja na mtu
nisiyemfahamu, mpaka wakanishona sehemu
zangu za siri..
Bado nilikuwa sijiamini na ile ndoto niliyokuwa
naota, mwili wangu wote ulikuwa unanitetemeka,
nikajifunua nguo yangu ya ndani nakuhakikisha sehemu zangu za siri zipo salama..
Nilibaki natikisa kichwa cha dharau huku nikishika
shika vizuri sehemu zangu za siri, kwani zilikuwa
nzima kabisaa..
"...eti Tina mie wanishone..? Mbona wangejuuuta
kunijua..?" nilijisemea mwenyewe huku nikiinuka nakuelekea
bafuni kuoga.
Ndani ya muda mchache nilikuwa nimesharudi
nakujifuta tayari kwa kulala tena.
Usingizi kwangu ulikuwa wa shida sana hivyo
nilishindwa kulala mpaka alfajiri waliporudi wakina Aisha na Lucy ambapo napo ilikuwa ni makelele
mtindo mmoja mpaka kunakucha..
Asubuhi ilipofika nilijikuta mtu wa mawazo
mawazo haswa kwa kile kitendo nilichowaambuki
za ukimwi kwa makusudi John na baba Latifah,
nafsi yangu ilinisuta nakujikuta nanyanyua simu yangu tayari kwa kuwapigia ili nikawaombe
msamaha kwa nilichowafanyia nakuwaelezea huo
ukimwi nilipoupatia..
Nilianza kwa kupiga namba ya John napo ikawa
inaita tu lakini haipokelewi nikaikata nakupiga
namba ya baba Latifah, "...Hallow.. Kwanza nianze na samahani Mzee
wangu.."
Nilijivika moyo wa kijasiri huku nikiwa pembeni ya
ukuta wa chuoni huku nikiongea kwa kujiamini..
"..enhee ulikuwa unasemaje binti..?"
"..najua nimekukosea tena sana na haukustahili kupewa adhabu hiyo uliyonaye, nakuomba
unisamehe mzee wangu.."
"...Nakusikiliza vizuri, unamuona huyo Mama
anakuja nyuma yako..?"
Sikuamini amini nikageuka nyuma huku
nikitetemeka nakumjibu.. "..ndio nimemuona Latifah akiwa na Mmama.."
"..huyo ndiye mke wangu na hapo yupo na Latifah
pamoja na Polisi mie nawasubiri, nadhani
umeshajua nini kinachofuata...?
Nikaikata ile simu nakugeuka tena nyuma kwa
mara ya pili kuhakikisha. Maskini Tina mie nilikuwa tayari kama mtu
aliyechanganyikiwa kwani ile simu niliyokuwa
nimeipiga hakuwa baba Latifah bali alikuwa ni
'classmate' wangu na wale niliowaona walikuwa ni
wapita njia tu tena mtu na mtoto wake.
Ile hali ya kuchanganyikiwa bado iliendelea kunitawala ndani ya ubongo wangu, niliizima
kabisa simu yangu nakuelekea 'intarnate cafe'.
kama kawaida yangu nilifungua moja kwa moja
mtandao wa kijamii 'facebook' nakuanza kuchati
na marafiki zangu ikiwa ni pamoja nakupokea
marafiki wapya. Nilipomaliza tu nikaingia moja kwa moja kwenye
group la Stories kwani stori zake huwa
nazipenda sana haswa ile ya play boy yani hadi
natamani ningepata kukutana na huyo Jeff ryder
mbona angejuta kwa Tina mie..
Ilinichukuwa kama nusu saa nikawa nimesharidhika kwa ile story ya play boy, nikaanza
kufuatilia zile comment mpaka nikakutana na jina
la 'Biggy'
"..mh siku nyingi sijakutana na mabonge embu
wacha nimchokoze..?"
Nilijisemea peke yangu huku nikilikagua profile lake, niliangalia picha zake zikaanza kunivutia
taratibu.
"..mh hapa kaisha, na lazima afuatane na wenzake
kina baba Latifah na Jerry.."
Nilijesemea kimoyo moyo huku nikifurahia kuipata
namba yake ya simu ambapo alikuwa ameiweka kwenye mtandao huu wa facebook.
Bila kupoteza muda Tina mie nikaichukua ile
namba kisha nikatoka pale intarnate huku
nikitafuta sehemu nzuri iliyotulia nakuanza
kumpigia..
"..hallow..?" "..yap mambo vipi? samahani naongea na nani?.."
"..mh, biggy mara hii umeshanisahau?"
Nilimtega makusudi kwani wanaume huwa
hawanibabaishi hata kidogo..
"..Sauti kama ya Gizzle hivi..?"
"..yeah, lakini siyo Gizzle unayemjua wewe..?" "..haya ndio uniambie sasa naongea na Gizzle
yupi..?"
Nilisita kidogo halafu nikafikiria jina lolote la mbele
kisha nikamjibu..
"..unaongea na Gizzle precious beiby wa tabata.."
"..enh bado sijakupata vizuri, 'anyway' niambie mambo vipi lakini.."
"..am mh mh mie nilitaka tu kukusalimia coz ni rafiki
yangu kwenye facebook.."
Nikamtia simu makusudi ili tu nimpime nione kama
atanipigia.
Nikiwa bado nimezubaa peke yangu mara simu yangu ikaita kuiangalia ni huyo huyo Biggy..
"..mh wanaume bwana,?"
Nilijichekea kimoyo moyo huku nikiipokea ile simu
nakumlegezea sauti kabisaa.
"..yeaah ni a a ambie Biggy..?"
"..dah poa tu, ujue nini?" "..yeah nini?"
Biggy akakaa kimya kwa muda na hapo ndipo
ukawa mwanya wangu kwani zile ndoto za jana
usiku zimenifanya nisiendelee kuambukiza ukoo
wa kina baba Latifah..
"..Biggy nikuulize kitu?" "..uliza tu wala usihofu.."
Nilikaa kimya kidogo kisha,
"..unapenda kwenda 'club'?"
"..yeah kwanini nisipende wakati mwili
unaniruhusu..?"
Nilimtega makusudi, "...aah, tumrudie Mwenyez Mungu, nakuomba leo
jioni tukutane kwenye ibada pale magomeni
mwembe chai.."
Biggy aliguna kisha akahaidi kutokea muda
utakapofika.
Nilirudi zangu mpaka hosteli kwetu pale Cbe huku nikiwa na furaha ya ajabu na nikiomba jioni ifike
haraka ili niwe na Biggy.
Ilipofika tu saa tisa na nusu Tina mie nikawa
nimeshaoga na nimevalia gauni refu mpaka chini
huku mkononi nikishikilia biblia niliyoazima kwa
rafiki yangu Rose. Ndani ya lisaa tayari nilikuwa ndani ya Magomeni
mwembe chai pale kituoni huku nikimtumia meseji
Biggy kumtaarifu kuwa namsubiria..
Haikuchukuwa muda akawa tayari amefika, sura
yake haikunipotea kwani tayari niliinasa katikaa
picha zake alizokuwa ameziweka facebook. Alikuwa amevalia mavazi ya kikanisani kweli.
"..angejua naenda kumpa ukimwi leo..?"
Niliusemea moyo huku nikimtolea jicho la
kiheshima kana kwamba ni binti mlokole kweli.
"..Biggy kanisa liko mbali kidogo, utanisamehe.."
Nilimdanganya huku nikiingia kwenye gari ya Biggy tena ki 'Starlet' kilichokuwa na vioo vyeusi,
"..haya niambie tunaelekea njia ipi?"
Aliniuliza Biggy.
"..pita njia hii, ukifika kwa mbele kuna kona
ntakuelekeza tena.."
Nilimdanganga huku akili yangu yote nikiielekeza ni jinsi gani nitamteka aweze kufanya mapenzi na
mie..
"..Biggy lakini hujaniambia kama umeoa, mie nilijua
utakuja na mkeo..?"
"..dah bado hata sijaoa lakini ndani ya miezi hii
mitatu ntakuwa nimeshaoa.." Hapo hapo ndo ukawa mwanya kwangu. Inaendelea…