*************************
.”Ndio hivyo kama nikuambiavyo kuwa hawa tunawatumia katika malindo yetu kwa muda wa usiku..?”
“..sasa mnawatumiaje tumiaje..?”
“..huwa hairuhusiwi kumwambia mtu yeyote lakini kwa sasbabu na wewe upo hapa kundini mwetu basi haina budi kukuambia kila kitu..”
“..enhee niambie basii..?”
“..yaan ni hivii, watoto wadogo tena wale wachanga kabisa huwa tunawachanja chanjo kwenye nanii zao vivyo hivyo mpaka kwenye vitovu vyao huwa tunawawekea alama ya herufi 666 na 999..”
“…na baada ya hapo..??”
“..baada ya hapo sasa wanakuwa wanatenda matendo kama watu wazima na wenye kujielewa kwa kusaidiwa na nguvu zetu za kishirikina na pia hata watu wa duniani inakuwa si rahisi kuwatambua kwani watoto hawa wana uwezo wakubadilika badilika kama wanyama..”
“sasa ni wakina nani wanakuwa na mamlaka ya kukaa nao karibu au kwenda kuwatumia..?”
“..Mtu yeyote ana mamlaka ya kuwatumia lakini endapo tu tamko litatoka kwa mkuu wetu kama unatakiwa kwenda sehemu fulani kufanya tukio..”
Kila akiendelea kuniambia huyu binti na mwili wangu ulikuwa katika msisimko wa hali ya juu huku nikitamani sana hata iwe ndoto au kama inawezekana kwa muda huu huu niweze kwenda huko walipo hao watoto..”
“naomba unipeleke basi mwenzangu..?”
“..mhh..!! we nenda mwenyewe bwana kwani masaa machache yaliotoka nilikuwa na mtoto mmoja nikimchanja sasa endapo mkuu wetu akiniona tena maeneo yale ataweza kunifanyia vibaya..”
Nilijipa moyo wa kijasiri nakuanza kuchomoka huku nikielekea sehemu husika walipo kundi la watoto ambao ndio wanatumika katika kuchezeshwa kama mizukule. Niliogopa sana lakini haikuwa na jinsi kwani lengo langu kubwanilitamani sana nimuone mwanangu Adrian japo nimtie mikononi mwangu nitaridhika. Kila nilivyokuwa nikipiga hatua ndivyo na halmashauri ya ubongo wangu nilihisi kama inamwagiwa barafu kali. Kitendo cha kufikisha mpaka hatua tano tu huku nikipishana na baadhi ya wazee wengine wakiwa hawajiwezi kabisa mithili ya wale omba omba wa mjini tena wale wenye ukoma. Wengi wao walikuwa wakinitolea macho tu nakupishana nao. Ardhi ilikuwa laini kama imewekewa manyoya huku ubaridi wake nikiufananisha na ule wa kwenye friza japokuwa haukuwa ukitetemesha miguu yangu kwa ubaridi wake. Sikutaka kukata tamaa zaidi ya kuendelea kusonga mbele huku mikono yangu nikiiweka kwa nyuma japo kiuoga uoga mpaka nilipokaribia eneo lile ambalo nilielekezwa na yule binti kuwa mwanangu Adrian na wenzake wapo maeneo haya. Hatimaye baada ya mwendo si mrefu sana na kwa mbali kidogo nikaanza kuhisi sauti za watoto wakilia kwa sauti kubwa. Na kwa muda huu sauti zile zilionesha kupaza sana japokuwa zote zilikuwa zikitokea eneo moja tu. Nikiwa katika hali ya kushangaa zile sauti bila ya kujua zinatokea upande gani mara kwa ghafla nikaanza kuhisi kama mtu ananishika kwa upande wa mgongoni. Taratibu niliinua mkono wangu wa kulia nakuanza kama kujipangusa kwa begani ambapo ndipo nilipokuwa nahisi kuna mtu ananishika. Ile hali ya ubaridi mkali tena ule niliokuwa nikiufananisha kama utakao kwenye friza kwa muda huu ukawa umetawala nakufika mpaka katika bega langu la upande wa kulia. Kila nikijitahidi kujipangusa tena bila kugeuka nakuangalia ndipo na ule ubaridi nikawa nauhisi kama unaniyeyukia katika bega langu taratibu ukivuja maji.
“..Niache hukoo..??, niacheee…????”
Nilitoa sauti kubwa na ya kupaza kabla sijageuka nakutambua ni mtu gani aliokuwa akinigusa ama kuniwekea kitu cha ubaridi katia bega langu la upande wa kulia. Maskini Tina mimi macho yangu na hisia vilikuwa tofauti kwani nilipogeuka tu nyuma ili kugundua ni nani, kumbe alikuwa ni kitoto kichanga kimenigandia kwenye bega langu la upande wa kulia. Nilijitahidi kuangaza kwa macho makali japo kumgundua vizuri yule mtoto lakini nilichoambulia kumgundua ni miguu tu kwani miguu ilionesha fika ni mtoto tena mchanga. Kila nikijitahidi kuichukuwa ile miguu yake nakuivuta kwa mbele kwa dhumuni la kumshusha begani kwangu lakini hali haikuwa hivyo kwani yule mtoto alianza kuyeyuka na kuwa barafu tena lile lichanganywalo na maji ya moto. Kuyeyuka kwa yule mtoto nakubakiwa miguu tu ndiko kulikuwa kukiendelea kunitisha huku nikiihisi kama vile nimeua kwani kiwili wili chote cha mtoto kilikuwa hakipo. Ndani ya muda mchache na ile miguu yote ikapotea kwa ghafla sasa nikabaki mimi kama mimi peke yangu. Sikuonesha kukata tama nikaendelea kupiga hatua nyingine mbele mpaka nikakutana na kundi kubwa la watoto wakiwa wamelala chini kabisa tena uchi wa mnyama.
Zoezi la kumtambua mwanangu Adrian kati ya wale watoto waliokuwa chini likaanza. Baadhi yao walikuwa wakifanana mithili ya Wachina hivyo ikanipa wakati mgumu wa kumtafuta mwanangu Adrian.
“… hapo hapo tulia na wala usiondoke…?? unafanyaje hapo muda huu na hao watoto..?”
Haraka haraka nikageuza macho yangu kwa hofu ya hali ya juu huku nikiifuatilia sauti ilipotokea. Maskini nikamshuhudia mzee mmoja aliokuwa ana mvi nyeupe katibu eneo lote la usoni mwake. Nilishusha pumzi kwanza nakukata fundo la mate kisha nikamjibu.
“..namhitaji mtoto mmoja simuoni Mzee..”
“.. kwa ruhusa ya nani..? kwanza kwanini unanitiita Mzee hapa..? au hujafunzwa hapa wewe..? niite Mkuu..?”
“..sawa mkuu nimekuelewa..”
“haya unataka mtoto yupi na wanini sasa hivi..? kwani hapa kuna utaratibu wake kama mtu anataka mtoto..?”
“..nakuomba sana muongozo Mzee..?”
“..nimekwambia usiniite Mzee husikiii..?”
Maskini Tina mimi nikawa kama vile nimefanya kosa kumuita Mzee badala ya Mkuu.. Alifanya ishara ambayo sikuitambua kisha nikashuhudia wametokea Mabinti kama watatu na mmoja wapo akiwa ni yule aliyekuwa mfanyakazi wa Aisha na kwa muda huu walikuwa uchi kabisa japo eneo la kwenye sehemu zao za siri ziliwekewa kitu kama mwanga mkali ambapo hata ufanyaje huwezi kugundua kama ni sehemu za siri.
“..huyu mkamfunde kwanza halafu mumlete hapa amesema ana shida sana na mtoto na sijui ni mtoto gani..?”
“..aliongea yule Mkuu ambaye nilimkera kwa kumuita Mzee badala ya Mkuu.
Safari ya Tina mimi kutoka katika lile eneo niliokuwepo namfuatilia mwanangu Adrian kuelekea mpaka eneo nisilokuwa hata nikilifahamu ilianza huku nikiburutwa na wale Mabinti watatu. Yule mfanyakazi wa Aisha nadhani sijui alikuwa amenisahau ama ndio alikuwa kazini..? kwani hakuonesha hata kuwa na kumbukumbu vizuri juu yangu nilichokuwa nimekifanya wakati nipo nae sehemu huru ya duniani. Alisaidiana na wenzake kuniburuta. Japo kulikuwa kunatisha sana lakini kiukweli nilipapenda sana kwani hakukuwa na ardhi zaidi ya manyonya tena malaini sana kama yale ya sufi.
“..Unatakiwa upige hatua kuanzia hapa mpaka unafika upande ule kulee halafu utaonana na Mama na Bibi zetu na kisha watakumbia nakukupa kitu hivyo utarudi tena hapa hapa ukipitia njia hii hii tunakusubiri kisha tutakurudisha kwa Mkuu wetu uliyemkuta kule kwa watoto..”
Aliropoka kwa sauti ya ukali naya kukemea huku akisisitizia yule mfanyakazi wa Aisha huku akionesha macho ya ukali na meno yakimtoka mithili ya zile picha za kutisha.
Nilifanikiwa kukanyaga zile nilizokuwa nimeambiwa. Miili mingi ya watu waliokufa ndio ilikuwa njia kuu. Na hata nilipofika katikati nilijikuta nikitema mate nakutapika nyongo hapo hapo chini nakuweza kuhamsha maiti moja.
“..futa mate yako..?? nimesema futaaa….?”
Ile maiti ilishtuka nakuamka kisha ikanikalipia kuwa niifute mate niliokuwa nimemtemea. Haraka haraka nilivuta nguo yangu nakuifuta eneo niliokuwa nimetema mate kisha ile maiti ikajirudisha pale pale ilipokuwa nakulala hivyo kuniacha nikiendelea na safari yangu ya kuendelea kuzivuka hizi maiti zingine. Hatimaye Tina mimi nikafanikiwa kuzivuka zile maiti zote mbele yangu na sasa nikawa upande wa pili huku nikigeuka nyuma nakuwatazama wale Mabinti niliowaacha kwa mbaali.
“..sasa umeingia katika ulimwengu mwingine wa mafunzo..”
Alikuwa ni Mbibi mweupe fupi sana akiongea na mimi huku akiniwahi kunishika mikono nakuniongoza katika eneo jingine nalo sikulijua hata ni eneo gani.. Nilipelekwa eneo ambalo sikuweza hata kuliamini kwani kulikuwa kama vile duniani. Mwanga mkubwa mithili ya jua, pipa kubwa lililokuwa limewekewa vitu vikiendelea kuchemka na huku wakina Mama wengine wakipakuwa. Hakukuwa na mwanaume hata mmoja. Na punde akanifuata mama mmoja alioonesha anachongo yaani haoni upande mmoja.
“..karibu Binti..? unatakiwa unywe hii hapa halafu urudi ulipotokea..”
“..hapana jamani siwezi kunywa..?”
“..Binti..? yaani usije ukathubutu kusema hivyo tena kwani utafanywa kama wale uliopishana nao wamelala kwa hapo nje..!! Embu kunywa halafu ukamchukue huyo mtoto maana hiki ninachokupa kitakutia nguvu za kuweza kufanya jambo lolote huko ukiwa na mtoto bila ya kugunduliwa na mtu yeyote..”
Nilijitahidi sana kugoma kata kata na hata kuwatishia naondoka zangu lakini haikuwezekana kwa Tina mimi kwani kilichofanyika nilishikwa kwa nguvu zote nakulishwa huku nikitishiwa kuwa endapo nitatapika nitaweza kuwafufua wale watu waliotandikwa chini hapo mlangoni hivyo mimi nitachukuwa nafasi yao kulala nakukanywaga kama mfu.. Maskini Tina mimi sikuwa na jinsi tena zaidi ya kukubaliana na ukweli japo nilikuwa siamini kwa asilimia zote lakini illinibidi kuamini hivyo nikaongezwa tena nakufakamia yale matapu tapu yao yaliochanganyika kama mauji uji hivyo hivyo nikijikaza nakutoka nje huku nikitoka nje nakuanza kuzikanyaga zile maiti kwa lengo la kuzivuka.
Nilipofika katikati kabla sijamalizia kuzivuka zile maiti zote mara kwa ghafla nikajihisi kama kichefu chefu kikitawala katika kinywa changu huku kikiupa mdomo nafasi kuwa wazi nakuanza kutapika kile nilicholishwa na wale kinamama.. Nilitapika sana ukichanganyia na kukohoa hovyo. Maskini Tina mimi kitendo kile kikawa kama kimehamsha zile maiti nilizokuwa nimezikanyaga kama njia ya kuvukia upande wa pili. Walianza kuinuka mmoja baada ya mwingine huku wakinicheka kwa sauti za juu. Hapo hapo nikaaza kutambua baadhi ya maiti zilizoinuka. Niliweza kumshuhudia Mchungaji James akiwa kashikilia kitu kama ile Bibilia yake, Biggy akiwa na nguo zake zile zile nilizomwacha nazo mara ya mwisho, Baba Latifah naye alikuwa kamkumbatia mwanake Latifah na mwisho kabisa nikamshuhudia Aisha na Jerry wakishikana mikono huku wote kwa pamoja wakinifuata eneo nililiokuwa nimesimama. Na kwa upande wa Jerry alikuwa amebabuka maeneo ya usoni huku akimshikilia Aisha wake ambaye naye Aisha hakuwa anaona Vizuri zaidi ya kuonesha akifikicha macho kwa shida.
“..Inaamaana Aisha na Jerry walikufa..?”
Nilijikuta nimezubaa huku naongea mwenyewe na punde karibu wale wote waliokuwa wamefufuka wakawa wameshanikaribia kwa ukaribu huku baadhi yao wakinishikilia mabega kwa dhumuni la kuanza kunitafuna tafuna kisha wanilaze chini…
Sasa nikavaa uhusika wangu wa Tina yule wazamani huku nikitimua mbio kuelekea sehemu ile niliowaacha wale mabinti. Kila nikijitahidi kupiga hatua kuwakimbia hawa watu waliofufuka nao walikuwa wanazidisha makelele ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanatibua ngome za masikio yangu sambamba na kuniletea msisimko wa ajabu ule uliochanganyikana na uwoga ndani yake. Baada ya muda mchache nilijikuta nimelowana karibia nguo zote si kwa jasho tu bali kwa yale matapishi niliokuwa nimeyatapika na kwa sasa yalikuwa yanasambaa katika mwili wangu wote huku yakileta harufu kali mithili ya gari la taka likikatiza katika umati wa watu wastaarabu.
“..niokoeeni jamani..?? nyieee…?”
Nilijitahidi kupiga makelele sana kwa upande wa mbele yangu kule nilipokuwa nimewaacha wale mabinti lakini haikuwa na msaada wowote zaidi ya kuwashuhudia wakinicheka huku wakipeana ishara ya mikono kana kwamba wananicheka kinafiki.
“..Wee si Tina..? leo umejileta mwenyewe..? mwanangu yuko wapi..?”
Alizungumza Jerry kwa sauti ya ukali. Maskini kwa upande wa uso wake eneo la mbele karibia lote lilikuwa limeharibika vibaya na hapo hapo halmashauri ya ubongo wangu ikafanya kazi haraka nakugundua kuwa huenda yale maji aliomwagiwa na yule mfanyakazi wa Aisha ndio yaliomsababishia ulemavu wake.
“sasa inamaana hata huyo binti hamtambuai kama yupo humu humu ama..? na Aisha si huyu hapa anaonekana mzima tu..?”
Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza mwenyewe bila ya kupata jibu huku nikiendelea kuwatolea macho mbele yangu ambapo tayari nilikuwa nikiwasubiri wanifikie karibu na kama kuna lolote wacha litokee tu kwani sikuwa tena na jinsi.
Mapigo yangu ya moyo tayari yalikuwa yameshaushinikiza ubongo kukata tamaa kabisa kwa muda huu. Kiukweli walikuwa wanatisha kwani baadhi yao walikuwa hawana hata midomo sasa sijui ndio walikuwa wametoka kupata ajali ama la! Waliponifikia karibu kabisa walinizunguka huku Aisha akimshika Jerry wake mikono nakuanza kunikumbatia kwa kutumia nguvu zao zote. Walinikumbatia kwa nguvu zote mpaka nikahisi kuishiwa nguvu nakudondoka mpaka chini kabisa ambapo napo wote waliiinama mpaka chini nakuanza kunilamba lamba mithili ya zile koni za bakhresa.
“..tumeghairii hatumtaki tena mwanetu..? tunakutaka wewe na piga ua hapa tunahakikisha tumekula nyama yako kisha tunakulaza pale tulipokuwa tuumelala!!”
Waliongea wote kwa pamoja tena kwa sauti mbilimbili huku kila mmoja akigawana kiungo chake. Kuna waliokuwa wananishika matiti yangu nakuyavuta, wengine makalio yangu wanayafinya finya na hata baadhi yao walikuwa wakinichezea sehemu zangu za siri kwa kuzivuta vuta kwa nguvu kiasi cha kunisababishia maumivu makali sana mwilini mwangu. Maskini Tina mimi nikawa sina jinsi zaidi ya kuanza kuhisi kizungu zungu kilichochanganyikana na kukata tamaa ya kuishi nakujiona sasa huu ndio mwisho wangu wa kuishi.
“..kwanini Tina mimi..?? kwanini jamani..??”
NIliusemea moyo wangu pale chini huku ule umati wa watu wafu ukiendelea kunizingira nakunishika shika kila eneo la mwili wangu.
********
Saa saba za mchana jua lilikuwa kali sana. Kila mmoja alionekana akiwa na kitambaa cha kufutia majasho na hata wengi wao waliokuwa na hela waliweza kujipooza makoo yao kwa kukata kiu kwa kinywaji baridi chochote. Mwili wangu wote ulikuwa mweusi sana kutoka kwenye weupe ule niliokuwa nao kipindi cha nyuma. Nilijishika kichwani napo sikuwa hata na nywele zaidi ya ule ule upara wangu. Nikiwa bado katika hali ya kujishangaa mwenyewe mara akapita Dada mmoja mbele yangu nakumsimamisha.
“..hapa ni wapi na nani kanileta hapa..?”
“..hapa mbona ni Manzese Darajani kwani wewe hulijui hilo hapo Daraja..? au umetoka kijijini leo nini..?”
Tina mimi sasa sikuwa hata nakumbukumbu kabisaa. Japo ni kweli macho yangu yalitazamana na Daraja kubwa lakini nafsi yangu ilikataa kabisa kuamini kuwa ni darajani Manzese kama alivyonimabia yule Dada kuwa hapa ni Manzsese darajani. Nilitoka katika lile eneo taratibu huku nikiongoza mpaka kituo cha dala dala ili kuhakikisha kama kweli hapa ni Manzese. Kitendo cha kufika tu maeneo ya kituo cha daladala nikamsikia kondakta wa daladala akimwambia mtu kuwa hapa ni Manzese.
“..sasa nani kanileta hapa..? na ilikuwaje kuwaje mpaka nimefika hapa..?”
Bado nilikuwa mtu wa kujiuliza mwenyewe bila ya kujipatia majibu akilini mwangu. Kila nikijitahidi kuvuta kumbu kumbu inanirudisha mpaka nyumbani Mwanza halafu basi sielewi ikawaje.
“..embu ngoja.., Mwanza..?? Mwanza…??, Mchungani James halafu nikarudi Dar, Dar…? Dar…? Jerry..? aha haaa Aisha..? yap Aisha alinipeleka kwake halafu kama nilijifungua, Mwanangu yuko wapi..? Mwanangu yuko wapi..?”
Maskini Tina mimi akili ikawa kama imeshaniruka kwa sauti ya ukali nikaanza kukimbia huku na kule nikipiga kelele kudai mwanangu. Baadhi ya watu walinishangaa na waliniona kama chizi lakini kiukweli ndio kumbukumbu zilizokuwa zimenirudia japo kidogo niliweza kutambua kuwa nilikuwa na mtoto. Nilikimbia huku na kule mpaka nikachoka mwenyewe kisha nikatafuta sehemu yenye kimvuli nakukaa chini huku nikichomoa matiti yangu nakuanza kuyakamua kwa nguvu.
“..nyonya mwanangu nyonyaaaa.. nyonya enhhh..?”
Bado nilikuwa katika hali ya kutojielewa elewa japo kidogo kidogo nilianza kupata ufahamu. Niliyarudishia maziwa yangu nakuanza kuongoza moja kwa moja kwenye kituo cha daladala kisha na mimi nikawa nasubilia kama abiria wengine.
“..hatupakizi vichaa..? weee Dada unakwenda wapi embu shuka huko..?”
Kwa hasira niligeuza jicho langu nakumtizama vizuri yule kondakta ambaye alikuwa hataki mimi nipande nakuniona kama chizi.
“..mwacheni apande mimi nitamlipia, hivi nyie makondakta hamnaga hata utu..?”
“wee mama vipi yaani ufanye utu kwa machizi ka hawa..?”
Waliendelea kubishana huku Tina mie nikiingia ndani ya daladala wala hata sikujua inaelekea wapi zaidi ya kuingia na kukaa kwenye siti. Baadhi ya abiria waliokuwa pembeni yangu walikuwa wakiziba pua zao kana kwamba wamesikia harufu mbaya huku baadhi yao wakininyooshea vidole. Ilinibidi kuwa zaidi yam pole Tina mimi.
Mwendo wa dakika kama ishirini ulitosha kabisa kufika mwisho wa kituo. Bado sikuwa na kumbukumbu ni sehemu gani zaidi ya kuendelea kiukodoa macho tu.
“….Binti unaonekana unamatatizo sana ..?”
“..wala mama sina hata tatizo..?”
Hapana mwanangu sura yako inaonesha kabisa unamatatizo kwani nyumbani wapi..?”
Aliendelea kunihoji yule Mama alienilipia nauli kwenye daladala na kwa kipindi hiki tulishuka naye pamoja ambapo alinisogelea nakuanza kuniuliza. Nilimjibu kwa shingo upande lakini hakuridhika zaidi ya kunishika mkono nakukubali kwenda naye huko kwake..
***Unavyodhani huko anapopelekwa Tina kutakuwa salama kweli..? na huyo Mama ni mtu mwema kweli na nini hatma ya Tina katika story hii,..?
***Biggy, Aisha, Baba Latifah na mchungaji James tayari wameshakufa hivi Tina kazi aliobakiza ni kwa Steve bagamoyo, Shebby huko huko Bagamoyo, Vonso, John mdogo wake Jerry ndio watakaofuata je unavyodhani itakuwaje kwa hao watu..
MWISHO