Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Ndugai alishasema atalinda ubunge wao, mwanasheria mkuu kasema wasiguswe, kazi ipo, utawala hawaelewi kuwa unawakera watu wengi sana, wapige hesabu, kura walizoiba+kura walizotangaza za upinzani, karibu 50%ya kura zote, bado wanajifanya manunda!
 
Mkuu uko sahihi, lakini Magufuli haheshimu katiba. Cecil Mwambe alijiondoa cdm akajiunga ccm kabisa, kisha akaitwa na spika kuendelea na bunge. Wabunge wa ccm walipomuuliza yuko bungeni kwa uwakilishi wa chama kipi, alisema ameitwa na spika. Na kweli akaendelea kuwa mbunge!
Yaani nchi inaendeshwa kishabiki Kama Simba na Yanga. Ushabiki wa kisiasa unapelekea viongozi wakengeuke na kukipa kisogo kiapo cha kuilinda katiba ya nchi hii.
Hakuna kiongozi anayekemea uvunjifu wa katiba kwenye awamu hizi )(5&6)
Zaidi wana tanguliza mbele matakwa binafsi na ya chama chao.
Ukishangaa ya mussa...
 
Wanaenda mahakamani kupinga hayo maamuzi afu mahakama inatengua maamuzi ya chadema ya kuwavua uanachama wao mpaka shauri lao litakaposikilizwa hivyo wataendelea kuwa wabunge.

Hii ni kwa mujibu Wa sheria
Rejea issue ya Zitto Kabwe kufukuzwa chadema lakini akabaki kuwa mbunge.
Rejea pia issue ya Cecil Mwambe.
Sasa hata wakienda mahakamani suala si lipo wazi chadema haijateua mbunge yeyote hao walioapishwa wametoka wapi?
 
Mkuu uko sahihi, lakini Magufuli haheshimu katiba. Cecil Mwambe alijiondoa cdm akajiunga ccm kabisa, kisha akaitwa na spika kuendelea na bunge. Wabunge wa ccm walipomuuliza yuko bungeni kwa uwakilishi wa chama kipi, alisema ameitwa na spika. Na kweli akaendelea kuwa mbunge!
Wacha iwe hivyo historia itamuhukumu huyo mvunja sheria na katiba ya nchi aliyoapa kuirumiki.na bichwa lake kama fenesi.
 
You all know Jiwe. Atatumia miguvu wabaki bungeni.
Anajulikana kwa hilo atumie tu miguvu wabaki Bungeni lakini hawatakuwa wabunge halali na Kanuni za Bunge zitabidi zibadilishwe kuwaruhusu waingie Ukumbini maana wasio wabunge wanaruhusiwa kuingia kwenye Public Gallery tu. Bunge dhaifu chini ya Spika dhaifu na agizo toka juu chochote kinawezekana!
 
Mzee msekwa angeulizwa,
He, iwapo CCM wakiamua kuwapeleka kina Halima Mdee na henhw lake mahakamani ili wakaweke zuio la kupingwa kufukuzwa uanachama,

He, wataendelea kuwa wabunge?
Cc.
Cha ajabu Leo jumamosi utasikia mahakama zimefunguliwa na tayali kina Covid 19 wameshafungua mashitaka.
..au hata kesho jumapili unaweza sikia pingamizi limepelekwa mahakamani!!
 
Imekiukwa misingi mingapi ya Katiba ndani ya utawala huu, itakuwa jambo "dogo" tu hili? Utawala wa awamu hii utawala wa sheria sio kipaumbele na mwenye mamlaka alishasema muhimili wake umejichimbia "chini zaidi" kuliko ile miwili iliyobaki. Ndio maana "mtumishi" wake kwenye ule muhimili "mdogo" alisema "Nitatumia GHARAMA zozote kuwalinda" (sijui kwa maslahi yapi!). Nadhani hapa kwenye "gharama zozote" mhimili uliojichimbia chini zaidi utahusika, na dalili zinaonekana.
 
View attachment 1636761

Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa Wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu Mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.

"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.
View attachment 1636763

CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
Jamani ariewapisha nahisi atawarinda. akuna Chakatiba wa.ra Cha sheria wa taznania bado wapowapo
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Jamani mjomba atatumariza tujipage bawacha taifa ssje. hatali
 
Angalau kuna Mzee moja wa ccm aliyekuwa na ujasiri wa kusema ukweli na kuheshimu katiba! Ila ajue kuwa Wenzake hasa spike wa sasa, hawana habari na katiba!
 
View attachment 1636761

Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa Wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu Mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.

View attachment 1637156

"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.
View attachment 1636763

CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television

Moja ya mitihani migumu kabisa anayoweza kukabiliana nayo binadamu ni kutafsiri matendo fulani kwa jicho la kisheria.

Sheria sio sawa na Hisabati ambayo majibu yake ni yale yale, liwake jua au inyeshe mvua. Kihisabati, 2+2=4, no matter what. Katika sheria, mambo ni tofauti. Mwanasheria yeyote anajua fika kwamba akitaka kuumba maoni thabiti juu ya jambo fulani ni muhimu sana akawa na ufahamu kamili wa facts na circumstances za jambo analotaka kulitolea maoni. Bila hiyo picha kamili, mwanasheria itabidi akubali kubeba risk kubwa zaidi ya kutoa naoni ambayo yanaweza kuwa sio sahihi.

Sina uhakika wa kina cha ufahamu wa Mzee Msekwa juu ya jambo alilolitolea maoni. He knows what he knows and he doesn’t know what he doesn’t know!
 
Mzee Msekwa kazungumzia ideal situation (kwa electrians wanaita kitu ideal wire ambayo haina resistance. Hivi ni wapi ipatikane wire bila resistance)
 
Wamesahau hao wale Ni wabunge ukweli wote utajulikana kadiri sinavyosogea Kama Chadema ilifanya hivyo kuwakomoa imejikomoa yenyewe.Kwisha habari yao , Chadema wivu unawasumbua
Ulimsikiliza PIUS MSEKWA??? Fanya hivyo utaelewa tu,Mara hii wanalumumba mnawapambania COVID 19 barabara na hii inathibitisha kuwa nyie ndo mmewaponza
 
Kwani kamaanisha yeye au ni vifungu vya katiba? Atapigwa biti kwani yeye ndio kaandika hiyo katiba? Hili ni suala la kikatiba uwe unataka au hutaki otherwise badilisha sheria.
Wenzako hawatakagi watu wajue.Wanataka watu waendelee kuwa mbumbumbu hasavwa mambo ya katiba na sheria ili wawe wanajifanyia watakalo.Kwao ujinga wa wengi ni mtaji muhimu sana.Kwa hiyo Pius ajiandae tu hamna namna.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Pius Msekwa pamoja na kuwa wakati mwingine anatetea mambo yasiyo sahihi yanayofanywa na ccm, nimetambua kuwa inapokuja kwenye katiba hababaiki!
 
Back
Top Bottom