Ama kweli watanzania wasanii ninyi. Yaani Pinda kiboko kwa sababu ametoa mkwara kwa viongozi wa serikali za vijiji. Mbona huo mkwara mi naweza kuutoa hata bila kuwa na cheo cha usaidizi wa waziri!! Eti vigogo
Mie nilidhani eti Pinda kawaweka ndani EL, BM, ZM, OM, DB, na AK. Kumbe yale yale tu ya kila siku yanayoturudisha nyuma. Kila anayeteuliwa anaenda kuwapiga mkwara makatibu kata. Nchi inauzwa na akina Jetu
Udikteta umepitwa na wakati, ulikuwapo enzi hizoooo. Sasa hivi watu wanakwenda kisheria, hawezi kukurupuka tu akawatia watu ndani. Watakao patikana na hatia sheria itafata mkondo wake. Huwezi kufunga watu kwa tuhuma. Uchunguzi umefanyika, tume ya uchunguzi ni upande mmoja wa sheria na watuhumiwa ni upande mwingine wa sheria. Kuhusu swala la Richmond, Pinda kisha weka wazi hilo na "task force" yake ya kisheria kaitangaza bungeni na ipo kazini na hatma ya watuhumiwa wa Richmond itajulikana on or before the next bunge session.
Vilevile amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watendaji vijijini kuwakamata wananchi na kuwaweka ndani kwa madai ya kutotoa michango, akisema kuwa kamwe hakuna sheria inayoruhusu unyanyasaji huo kwa wanyonge.
Kuwaambia watu wasio wajibika ni udikteta? Huenda TZ inahitaji dikteta mpenda maendeleo. Wengi wetu tumezidi maneno mengi lakini vitendo hakuna. Lazima ifike mahali, viongozi ambao hawana uwezo wa kudeliver wang'olewe mara moja.
Halmashauri za wilaya zina pesa nyingi tu ambazo laiti zingelitumiwa vizuri, kungelikuwa na aina fulani ya maendeleo huko wilayani. Tatizo ni wizi na capacity ndogo ya watendaji.
Wasiwasi wangu tu ni kwamba Pinda alikuwa huko kama miaka miwili na hakufanya la maana.
Mungu ibariki Tanzania...haya mapambano ya fikra yamechelewa sana kuanza...natumai tutafika tu, majeshi mbele.
2008-03-03 20:09:21
Na Mwandishi Wetu, Mpanda
Aidha, Bwana Pinda akaagiza kuwa kuanzia sasa, wakaguzi wa mahesabu watue kwenye maeneo hayo na kukagua mapato na matumizi ili yeyote atakayebainika kutumia pesa hizo isivyo halali, achukuliwe hatua kali za kisheria.
Isije ikawa kusema tu wengi walikuwepo wakasema tena sana lakini matendo hakuna hata tone. ndio maana serikali hasa watendaji wa ngazi za juu wanadharauliwa na watendaji wao wa chini kabisa kwa sababu hawafuatilii maelekezo wanayoyatoa kwao. Watu watakuwa waoga pale watakapoona wenzao tena sio wa kubahatisha wanawajibishwa kikweli kweli na sio kudanganya wananchi.
Na ili mikakati hii ifanikiwe ni muhimu sana hata big fish wachukuliwe hatua madhubuti za kisheria. Itakuwa rahisi sana kwa viongozi wa chini kuwa makini na kazi zao kama wataona wakubwa wao wanachukuliwa hatua. Nina hakika watajiuliza maswli kama who am i kama El ameweza kuwajibishwa, i mean seeing the big potatos fall kutaweza kuwaogopesha watendaji wadogo.``Pinda kiboko. Kwa kuvalia njuga ufisadi huu unaofanyika kila kukicha katika manispaa na vijiji vyetu, ni wazi kwamba sasa mafisadi watakiona,`` amesema Bw. Daud Elias, mkazi wa Mpanda ambaye naye alihudhuria mkutano huo wa hadhara.
``Kauli yake inaonyesha wazi kuwa walaji sasa hawana chao. Wengi wataswekwa ndani ama kufilisiwa mali walizojilimbikizia kwa njia za kifisadi,`` akaongeza mkazi mwingine wa Mpanda aliyejitambulisha kama Mama Adam.
Hivi karibuni, Serikali imekuwa katika zoezi kabambe la kupambana na vitendo vya kifisadi, ambavyo kila kukicha vinaigharimu mabilioni ya pesa.
SOURCE: Alasiri
Ni kweli vijijini kuna Uharamia mkubwa unaofanywa na watendaji wa SISIEMU wa huko vijijini kwa baraka za SISIEMU Taifa.
Nimewahi kumsoma mtu mmoja akilezea kwamba,Ukiwa kijijini ofisi ya SISIEM yaweza geuka Jela, Mahabusu Chumba cha kutesea, dangulo la kudharirishia mama zetu na Mahakama ya hakimu mkazi dakika yeyote.
Sishangai,ushenzi huu ndizo nyenzo muhimu za kuimarisha Umoja na Amani iliyo sera ya SISIEMU nchi nzima.
Kwa Lugha nyingine MH Pinda anapingana na utekelezaji wa ilani ya SISIEMU ya kuto kumwangalia Mtanzania yeyote usoni, ni kumkoma tu.
Huko vijijini SISIEMU siyo chama cha siasa ni Serikali ni Jela na ni nyumba ya Hitler, mahali pa kutesea na kudharirisha utu wa watu.
MH Pinda Anatafuta umaarufu kwa Soft Target na kujitangaza kuwa yeye ni Maximan, kwa sababu kila akipiga shabaha analenga Bull.
Arudi toka huko mpanda aje apambane na Uoza wa pale Dar.
Hongera MH Pinda, lakini ni vema uonyeshe makucha kwa vitendo siyo siasa za majukwaani tu.
Wameshaanza; walifanya hivihivi JK alipoingia. Alikuwa hata akikohoa wanasema: JK kiboko, JK mwisho wa yote, etc; lakini sasa.... Yetu masikio na macho!
umenena ukweli fundi, matatizo ya watz wakawaida sio EPA wala RDC, nimisako ya kodi bubu, uhuni wa makarani wa mahakama, kutoaji upepo wa matrafiki na ajali za barabarani, kupanda kwa ada za vyuo na bei ya saruji, ukiritimba katika mashauri ya mirathi, kizunguzungu katika ofisi za ardhi, wazimu wa upatikanaji wa hati miliki, upigwaji mimba watoto wa shule, dhuluma za wanunuzi wa pamba na korosho, kutimuliwa wananchi katika ardhi yao kupisha uwekezaji usiowanufaisha, dhuluma kwa vibarua, etc.