Wafanyabiashara Mpanda walalamikia Jeshi la Polisi jinsi linavyoendesha Oparesheni zake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Baadhi ya Wafanyabiashara katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelilalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha oparesheni zake za kusaka waharifu ambapo katika siku za hivi karibuni baadhi ya Wananchi wamekuwa wakipigwa na jeshi hilo hasa katika nyakati za jioni na kuleta hofu kwa jamii.

Emily John, Richard Sunzu na Paul Masoud ni baadhi ya Wafanyabiashara ambao wametoa malalamiko hayo katika kikao cha wadau wa uwekezaji kilichofanyika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambapo Wadau wengi wameilalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha oparesheni zake huku baadhi ya Wananchi wakipata hofu ya kutembea nyakati za jioni hasa kuanzia saa moja jioni.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema usalama katika wilaya hiyo ni wa kutosha na utaendelea kuwepo huku akiwahakikishia Wafanyabiashara kuendelea na kufanya shughuli za biashara zao katika hali ya amani na utulivu.

Aidha, hatua nyingine Jamila amewaomba wawekezaji kuendelea kujitokeza katika wilaya hiyo ili uwekezaji katika Nyanja mbalimbali uweze kuleta manufaa kwa kwa jamii na Taifa zima.
 
DC hajajibu suala la polisi,yeye anasema usalama upo wa kutosha,sasa kama upo wa kutosha,operesheni yanini?
Hivi vyombo vya ulinzi na usalama, sometimes vinazingua katika utendaji kazi wake,unanyanyasaje mlipa kodi?
Ujinga mtupu.
Majuzi JWTZ Kawe,leo PT huko,sijui inakuaje?
 
Baadhi ya Wafanyabiashara katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelilalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha oparesheni zake za kusaka waharifu ambapo katika siku za hivi karibuni baadhi ya Wananchi wamekuwa wakipigwa na jeshi hilo hasa katika nyakati za jioni na kuleta hofu kwa jamii.

Emily John, Richard Sunzu na Paul Masoud ni baadhi ya Wafanyabiashara ambao wametoa malalamiko hayo katika kikao cha wadau wa uwekezaji kilichofanyika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambapo Wadau wengi wameilalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha oparesheni zake huku baadhi ya Wananchi wakipata hofu ya kutembea nyakati za jioni hasa kuanzia saa moja jioni.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema usalama katika wilaya hiyo ni wa kutosha na utaendelea kuwepo huku akiwahakikishia Wafanyabiashara kuendelea na kufanya shughuli za biashara zao katika hali ya amani na utulivu.

Aidha, hatua nyingine Jamila amewaomba wawekezaji kuendelea kujitokeza katika wilaya hiyo ili uwekezaji katika Nyanja mbalimbali uweze kuleta manufaa kwa kwa jamii na Taifa zima.

Mwanangu wa form 6 amawezakuwa na bitter IQ
 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema usalama katika wilaya hiyo ni wa kutosha na utaendelea kuwepo huku akiwahakikishia Wafanyabiashara kuendelea na kufanya shughuli za biashara zao katika hali ya amani na utulivu.
Mkuu wa polisi kwa upande wake amesemaje?
 
Back
Top Bottom