Pinda kiboko

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
2008-03-03 20:09:21
Na Mwandishi Wetu, Mpanda

Wale waliodhani Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Mizengo Pinda ni mtu laini laini, basi wameula wa chuya kwani mzee ni mchungu kuliko hata shubiri na tayari ameanza kufyatua makucha yake na kuwaonyesha watendaji wababaishaji kuwa, yeye ni kiboko na kamwe hawatapumua chini ya uongozi wake.

Bwana Pinda ambaye wanaomfahamu wanamuelezea kuwa ni mtu mpole na asiyependa kabisa kujihusisha na dili chafu za kifisadi, ameonyesha makucha yake hayo baada ya kuwanyaka mafisadi wapya kibao na kuamuru hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Akihutubia mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika wilayani Mpanda jana, Bw. Pinda amewataja mafisadi hao kuwa ni pamoja na vigogo walio katika ngazi za manispaa, Serikali za vijiji na zile za mitaa.

Akasema katika maeneo hayo, kuna baadhi ya viongozi ambao hujilimbuikizia mali haramu, kwa kuchota mapesa yanayotolewa na Serikali na kuchangiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kama shule.

Aidha, Bwana Pinda akaagiza kuwa kuanzia sasa, wakaguzi wa mahesabu watue kwenye maeneo hayo na kukagua mapato na matumizi ili yeyote atakayebainika kutumia pesa hizo isivyo halali, achukuliwe hatua kali za kisheria.

Vilevile amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watendaji vijijini kuwakamata wananchi na kuwaweka ndani kwa madai ya kutotoa michango, akisema kuwa kamwe hakuna sheria inayoruhusu unyanyasaji huo kwa wanyonge.

``Pinda kiboko. Kwa kuvalia njuga ufisadi huu unaofanyika kila kukicha katika manispaa na vijiji vyetu, ni wazi kwamba sasa mafisadi watakiona,`` amesema Bw. Daud Elias, mkazi wa Mpanda ambaye naye alihudhuria mkutano huo wa hadhara.

``Kauli yake inaonyesha wazi kuwa walaji sasa hawana chao. Wengi wataswekwa ndani ama kufilisiwa mali walizojilimbikizia kwa njia za kifisadi,`` akaongeza mkazi mwingine wa Mpanda aliyejitambulisha kama Mama Adam.

Hivi karibuni, Serikali imekuwa katika zoezi kabambe la kupambana na vitendo vya kifisadi, ambavyo kila kukicha vinaigharimu mabilioni ya pesa.

Mikataba bomu inayoingiwa na baadhi ya vigogo Serikalini kama ule wa Richmond, manunuzi feki na ulipaji mapesa wa kitapeli kama uliofanyika katika akaunti ya madeni ya nje, EPA ni baadhi ya vitendo hivyo vya kifisadi ambavyo Waziri Mkuu Pinda alishaapa kupambana navyo.

SOURCE: Alasiri
 
Ama kweli watanzania wasanii ninyi. Yaani Pinda kiboko kwa sababu ametoa mkwara kwa viongozi wa serikali za vijiji. Mbona huo mkwara mi naweza kuutoa hata bila kuwa na cheo cha usaidizi wa waziri!! Eti vigogo
Mie nilidhani eti Pinda kawaweka ndani EL, BM, ZM, OM, DB, na AK. Kumbe yale yale tu ya kila siku yanayoturudisha nyuma. Kila anayeteuliwa anaenda kuwapiga mkwara makatibu kata. Nchi inauzwa na akina Jetu
 
Udikteta umepitwa na wakati, ulikuwapo enzi hizoooo. Sasa hivi watu wanakwenda kisheria, hawezi kukurupuka tu akawatia watu ndani. Watakao patikana na hatia sheria itafata mkondo wake. Huwezi kufunga watu kwa tuhuma. Uchunguzi umefanyika, tume ya uchunguzi ni upande mmoja wa sheria na watuhumiwa ni upande mwingine wa sheria. Kuhusu swala la Richmond, Pinda kisha weka wazi hilo na "task force" yake ya kisheria kaitangaza bungeni na ipo kazini na hatma ya watuhumiwa wa Richmond itajulikana on or before the next bunge session.
 
Kuwaambia watu wasio wajibika ni udikteta? Huenda TZ inahitaji dikteta mpenda maendeleo. Wengi wetu tumezidi maneno mengi lakini vitendo hakuna. Lazima ifike mahali, viongozi ambao hawana uwezo wa kudeliver wang'olewe mara moja.

Halmashauri za wilaya zina pesa nyingi tu ambazo laiti zingelitumiwa vizuri, kungelikuwa na aina fulani ya maendeleo huko wilayani. Tatizo ni wizi na capacity ndogo ya watendaji.

Wasiwasi wangu tu ni kwamba Pinda alikuwa huko kama miaka miwili na hakufanya la maana.
 
Vilevile amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watendaji vijijini kuwakamata wananchi na kuwaweka ndani kwa madai ya kutotoa michango, akisema kuwa kamwe hakuna sheria inayoruhusu unyanyasaji huo kwa wanyonge.

Hivi unadhani kwa mwanakijiji wa Matombo ni adha ipi inamgusa sana? Ya ufisadi wa Richmond au hii ya kamatakamata ya viongozi wa kijiji? Hapa ndipo wapinzani wanapochemsha maana ni haya tunayoyaona madogo ndiyo kero kubwa kwa watanzania wengi na si hizi tulizozishikia bango. Richmond itamuumaje wakati hajawahi hata siku moja kuota kuwa atapata umeme? Ni haya masuala ya kijamii ambayo sisi wasomi tunayapuuzia ndiyo ya msingi kwa watanzania wengi.
 
Mungu ibariki Tanzania...haya mapambano ya fikra yamechelewa sana kuanza...natumai tutafika tu, majeshi mbele.
 
FM, you never cease to amaze me!!

Ikumbukwe pia kuwa pia Mhe Pinda pia amesitisha mambo ya kamata kamata za kukusanya michango kule vijijini kuruhusu watu waende kulima (nampa sio tano, ni kumi kabisa!!!). Najua wengi tunataka mabadiliko overnight (am sure mi ni mmojawapo) lakini kama FM alivyosema hapo juu wakuu, kuna maamuzi ambayo yanatugusa sisi wa mijini (apprx 10% ya waTz) na kuna mengine ya wale wenzetu wa vijijini (90% ya wote).....(FM nadhani tupo pamoja).. Hivyo nina uhakika kuna strategic approaches ambazo JK na Pinda watakuwa wanazifuata katika maamuzi ili ku-balance pande zote mbili za waTz!!

Nina uhakika kwamba wengi tunajua nguvu aliyonayo Mtendaji kata/kijiji/mwenyekiti wa kijiji na viongozi wa namna hii kule vijijini, wacha kabisa usiseme hawa jamaa wakiwa na operesheni kuna wanavijiji wanaishia kulala nje au wakati mwingine vijiji vya jirani manake hawa waheshimiwa ni wa kuogopewa!!!

Viva JF, viva Viongozi waadilifu, viva waTanzania!!!
 
Enzi zile alikuwa hana meno sasa kapewa rungu tungoje utekelezaji.
All the best Mh Pinda
 
Kuwaambia watu wasio wajibika ni udikteta? Huenda TZ inahitaji dikteta mpenda maendeleo. Wengi wetu tumezidi maneno mengi lakini vitendo hakuna. Lazima ifike mahali, viongozi ambao hawana uwezo wa kudeliver wang'olewe mara moja.

Halmashauri za wilaya zina pesa nyingi tu ambazo laiti zingelitumiwa vizuri, kungelikuwa na aina fulani ya maendeleo huko wilayani. Tatizo ni wizi na capacity ndogo ya watendaji.

Wasiwasi wangu tu ni kwamba Pinda alikuwa huko kama miaka miwili na hakufanya la maana.

Yaani vitendo huvioni mpaka vya kuwajibika kwa waziri mkuu?
 
2008-03-03 20:09:21
Na Mwandishi Wetu, Mpanda

Aidha, Bwana Pinda akaagiza kuwa kuanzia sasa, wakaguzi wa mahesabu watue kwenye maeneo hayo na kukagua mapato na matumizi ili yeyote atakayebainika kutumia pesa hizo isivyo halali, achukuliwe hatua kali za kisheria.

Isije ikawa kusema tu wengi walikuwepo wakasema tena sana lakini matendo hakuna hata tone. ndio maana serikali hasa watendaji wa ngazi za juu wanadharauliwa na watendaji wao wa chini kabisa kwa sababu hawafuatilii maelekezo wanayoyatoa kwao. Watu watakuwa waoga pale watakapoona wenzao tena sio wa kubahatisha wanawajibishwa kikweli kweli na sio kudanganya wananchi.

``Pinda kiboko. Kwa kuvalia njuga ufisadi huu unaofanyika kila kukicha katika manispaa na vijiji vyetu, ni wazi kwamba sasa mafisadi watakiona,`` amesema Bw. Daud Elias, mkazi wa Mpanda ambaye naye alihudhuria mkutano huo wa hadhara.

``Kauli yake inaonyesha wazi kuwa walaji sasa hawana chao. Wengi wataswekwa ndani ama kufilisiwa mali walizojilimbikizia kwa njia za kifisadi,`` akaongeza mkazi mwingine wa Mpanda aliyejitambulisha kama Mama Adam.

Hivi karibuni, Serikali imekuwa katika zoezi kabambe la kupambana na vitendo vya kifisadi, ambavyo kila kukicha vinaigharimu mabilioni ya pesa.

SOURCE: Alasiri
Na ili mikakati hii ifanikiwe ni muhimu sana hata big fish wachukuliwe hatua madhubuti za kisheria. Itakuwa rahisi sana kwa viongozi wa chini kuwa makini na kazi zao kama wataona wakubwa wao wanachukuliwa hatua. Nina hakika watajiuliza maswli kama who am i kama El ameweza kuwajibishwa, i mean seeing the big potatos fall kutaweza kuwaogopesha watendaji wadogo.
 
Wameshaanza; walifanya hivihivi JK alipoingia. Alikuwa hata akikohoa wanasema: JK kiboko, JK mwisho wa yote, etc; lakini sasa.... Yetu masikio na macho!
 
Ni kweli vijijini kuna Uharamia mkubwa unaofanywa na watendaji wa SISIEMU wa huko vijijini kwa baraka za SISIEMU Taifa.

Nimewahi kumsoma mtu mmoja akilezea kwamba,Ukiwa kijijini ofisi ya SISIEM yaweza geuka Jela, Mahabusu Chumba cha kutesea, dangulo la kudharirishia mama zetu na Mahakama ya hakimu mkazi dakika yeyote.

Sishangai,ushenzi huu ndizo nyenzo muhimu za kuimarisha Umoja na Amani iliyo sera ya SISIEMU nchi nzima.

Kwa Lugha nyingine MH Pinda anapingana na utekelezaji wa ilani ya SISIEMU ya kuto kumwangalia Mtanzania yeyote usoni, ni kumkoma tu.

Huko vijijini SISIEMU siyo chama cha siasa ni Serikali ni Jela na ni nyumba ya Hitler, mahali pa kutesea na kudharirisha utu wa watu.

MH Pinda Anatafuta umaarufu kwa Soft Target na kujitangaza kuwa yeye ni Maximan, kwa sababu kila akipiga shabaha analenga Bull.

Arudi toka huko mpanda aje apambane na Uoza wa pale Dar.

Hongera MH Pinda, lakini ni vema uonyeshe makucha kwa vitendo siyo siasa za majukwaani tu.
 
Sasa kwa nini hawa waheshimiwa wapinzani hawako huko kuwatetea hawa wanyonge dhaidi ya udhalimu huo? Au wanangojea ifike siku ya uchaguzi waingie kwa vishindo kwa helikopta? Nakumbuka umoja wa wanawake aliouanzisha Tibaijuka ulivyokuwa na nguvu kwa sababu alianzia kwenye grassroots, kushughulikia matatizo ya wanawake wa kawaida! Kwa nini hawa wenzetu hawako huko ambako wote tunajua kuna matatizo kibao?
 
Hongera PM Pinda kwa mwanzo mzuri ila uwe makini manake watanzania watakufuatilia every step you make manake wametoka kuumia sana na Richmond na kidonda hakijapona vizuri.MKOME NYANI KWA UTARATIBU NA BUSARA YA HALI YAJUU ....USISAHAU KUMKOMA NYANI HUYO MCHANA KWEUPEEEEEEEEEEEE.
 
Unaponunua gazeti la Alasiri inabidi ununue kwa sababu unalipenda siku zote, sio ununue kwa sababu ya vichwa vya habari vya siku hiyo, vinginevyo utakuwa disappointed sana. Wanakuza mno mambo!
 
Wameshaanza; walifanya hivihivi JK alipoingia. Alikuwa hata akikohoa wanasema: JK kiboko, JK mwisho wa yote, etc; lakini sasa.... Yetu masikio na macho!

Kwa kweli wengine walienda mbali zaidi JK ni chaguo la Mungu, anamvuto kuliko baba wa taifa...hao hao sasa hivi midomo iko wazi baada ya kuona jamaa ni msanii tu...anapiga risasi maiti (kufukuza kazi Balalli aliyejiuzulu)

MP naye itakuwa hivyo hivyo, binafsi si mfagilii kabisa, si ni huyu amesema kufanya kosa ni kulirudia...what is that?

Anyway source ya habari ni gazeti la udaku ALASIRI
 
umenena ukweli fundi, matatizo ya watz wakawaida sio EPA wala RDC, nimisako ya kodi bubu, uhuni wa makarani wa mahakama, kutoaji upepo wa matrafiki na ajali za barabarani, kupanda kwa ada za vyuo na bei ya saruji, ukiritimba katika mashauri ya mirathi, kizunguzungu katika ofisi za ardhi, wazimu wa upatikanaji wa hati miliki, upigwaji mimba watoto wa shule, dhuluma za wanunuzi wa pamba na korosho, kutimuliwa wananchi katika ardhi yao kupisha uwekezaji usiowanufaisha, dhuluma kwa vibarua, etc.
 
Na katika sehemu kubwa ya haya hakuna anayewasemea hao wananchi wa kawaida. Sasa kwa nini wasimfurahie huyo ambae angalau amelizungumzia ingawa ametoka kwenye chama tawala?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom