DC Mpanda awataka Wananchi wanaoishi maeneo ya Hifadhi ya Misitu kuondoka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baadhi ya Wakazi Kijiji cha Kimani, Kata ya Ugala Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wametoa malalamiko yao ambayo yanawataka kuhama katika eneo wanaloishi.

Grace Julius na Simon Daluso wametoa malalamiko katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya ambapo wamesema wamekuwa wakiambiwa kuhama katika maeneo yao ambayo yanadaiwa kuwa Hifadhi ya Msitu wa Kijiji.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo, Mohamed Ramadhan amesema eneo hilo linatambulika kuwa ni Hifadhi ya Msitu huku Godfrey Msumari kutoka Ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania, Wilaya ya Mpanda (TFS) akiwaomba Wananchi kutokuwa na haraka katika maamuzi na badala yake wasubiri maelekezo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amewataka kuondoka katika maeneo hayo ya Hifadhi ya Msitu huku akisisitiza Sheria ya Misitu kutumika kwa wale wote waharibifu wa miti.

Mbali na hayo Jamila ameagiza uongozi wa Kata ukishirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha wale wote wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Msitu huo kupatiwa maeneo mengine ya kuishi na kufanyia shughuli za kilimo.
 
Back
Top Bottom