View attachment 80635
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda
amependekeza katika Katiba
mpya ijayo, madaraka ya Rais
yapunguzwe hasa katika
shughuli za uteuzi wa
viongozi.
Akizungumza jana baada ya
kutoa maoni mbele ya
wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Pinda
alisema muda aliokaa
madarakani na Rais Jakaya
Kikwete, ameona ana mambo
mengi na ndiyo maana
anapendekeza si lazima kila
jambo liende kwake.
"Ni vema machache yabaki
kwake. Kwa mfano uteuzi wa
nafasi mbalimbali vipewe
vyombo vya kufanya uteuzi
huo," alisema bila kufafanua
nafasi ambazo Rais anatakiwa
kuacha kuteua. Kuhusu nafasi
ya Waziri Mkuu, alisema hiyo
ni ya utendaji na kwa sasa
Waziri Mkuu lazima awe
mbunge na kutokana na hali
hiyo, anapendekeza itazamwe
vizuri.
Alifafanua kuwa Waziri Mkuu
atajikuta akilazimika kuangalia
zaidi Serikali huku jimbo
analowakilisha likilala kwa
kukosa usimamizi mzuri.
Kutokana na hali hiyo,
alipendekeza mawaziri
wasitokane na wabunge, ili
wafanye kazi vizuri ya
kusimamia majimbo yao
wakisaidiana na wananchi.
Uhuru wa Bunge, Mahakama
Alisema Bunge na Mahakama
ni vyombo muhimu
vinavyostahili kupewa nafasi
ya kutosha.
Alizungumzia mifuko
iliyoundwa ya Bunge na
Mahakama na kutaka
itambuliwe kikatiba na Katiba
ielekeze ni namna gani
itumike. Kuhusu kinga ya
mbunge, alisema ni vizuri
itamkwe kwenye Katiba kuwa
mbunge ana kinga, lakini ibaki
bungeni tu si azungumze nje
na kinga ya Bunge iendelee
kumlinda.
Akizungumzia Muungano,
Pinda alisema tangu azaliwe
hadi anapata akili mwaka
1964, alikuta Muungano na
ndicho kitu pekee anachoweza
kukisemea vizuri kwa kuwa
umejenga udugu, muungano
na ukaribu.
"Hapakuwa na huyu ni mgeni,
au huyu ametoka huku au
kule," alisema akizungumzia
Muungano wa Serikali mbili
ulivyo. Alikiri kuwa kuna kero
nyingi za Muungano na
kupendekeza kuwa dawa ya
kero hizo si kuua Muungano,
bali kitafutwe chombo
kitakachoshughulikia
matatizo.
Alipendekeza Serikali zibaki
mbili lakini iundwe tume ya
kushughulikia matatizo
yaliyopo. Pia akapendekeza
kuundwe Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Tanzania Bara kama
ilivyo Zanzibar na vyama
vyote vipate ushiriki. Mafuta,
gesi Akizungumzia rasilimali za
Taifa za mafuta na gesi, Pinda
alisema haoni shida mafuta
kuchimbwa Zanzibar na
kusafirishwa Bara au
kuchimbwa Bara na
kusafirishwa Zanzibar kwa
kuwa atavuka tu kununua na kurudi.
Chanzo: Habari leo.
Ninakupongeza kwa kuwa na ujasiri wa kuzungumza maneno kama hayo ktk maoni yako. Wako ambao ama kwa kuogopa ama utashi wao wameonelea Rais abakiwe na madaraka aliyonayo ama kuongezewa ilihali waliowengi wanaona Rais hawezi kuubeba mzigo alionao.
Mambo yameongezeka pamoja na vitengo mbalimbali hivyo ni lazima Rais apunguziwe mzigo.