Pinda ataka Rais apunguziwe Madaraka

Pinda ataka Rais apunguziwe Madaraka

Natamani Upinzani wachukue nchi huku madaraka ya Rais yawe makubwa hivi hivi ... 2020 si mbali ... tuvute subira
 
Naamini hivi sasa wao ndio wanaisoma namba kuliko hata wapinzani kwa anayoyafanya Magufuli.

Sina shaka hivi sasa nao wameanza kuonja machungu ya madaraka makubwa ya kikatiba aliyonayo raisi na pengine wanatamani yapunguzwe na sitashangaa kuwasikia wakidai hadharani madaraka ya raisi yapunguzwe au hata kuwatumia wapinzani.

Muosha, huowoshwa.
Usifikili watanzania wote ni misukule, tunaelewa unavyojaribu kipiga kiki chama cha majipu(CCM) hakuna jipya ccm ni ile ile,ni usanii tu usiona maana wa kukonga mashabiki misikule. wengi tunaona na tunaelewa usanii tupu unaofanyika. majiccm yote lao moja usidanganyike

ccm haitakuja ibadilike kamwe! alafu tabia ya kung'ang'ania madaraka ilikwisha pitwa na wakati! wenzetu wanapambana na maendeleo ccm inakomaa kupora ushindi kila chaguzi ujinga mtupu. Naogopa huko mbele ccm italeta vita nchini na ubaguzi kama tabia hii itaendelea

NB: watanzania wote bara na visiwani tuwe wavumilivu tulinde amani yetu, tupaze sauti za amani kudai haki, tupuuze ubaguzi unaoenezwa na chama cha majipu(ccm) lengo lao ovu sana!!!!
 
Yeye ni fisadi kila mtu anajua so hana jipya.hii ni danganya toto
 
Nasema hivi kwa sababu kadhaa ambazo ni:-

Teuzi anazofanya zingeondolewa kwenye mamlaka yake na badala yake zihamie NEC ili wapigiwe kura. Mfano, wakuu wa wilaya na mikoa wapigiwe kura na wale anaokwenda kuwaongoza. Hii itapunguza yaliyojitokeza juzi kwenye kuapisha wakuu wa wilaya yasijitokeza.

Na pia udanganyifu wa kumjua badala ya kujua nini utaisha. Japo hatujui waliompachika huyu jamaa wamechukuliwa hatua gani kwa makosa ya wazi na kukusudia na yenye madhara kwa Rais kama kungekuwa na nia ovu japo inaweza kuwa ilikuwepo mtandao huo uondolewe haraka sana.

Kwa nafasi za utendaji za wakurugenzi zitangazwe na kuombwa. Majaji nao waombe nafasi hizo ili kuleta uwajibikaji sahili. Mengine ongezeeni.
 
Wakati Balozi Semfue akitaka rais asipunguziwe madaraka katika katiba mpya, mtoto wa mkulima Mh. Pinda amesema rais ana madaraka makubwa sana na ni vema akapunguziwa madaraka hayo.

Pia ameshauri katiba mpya isiruhusu Waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine kutokana na Bunge (wasiwe wabunge) ili kuwe na checks and balance...

Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi yeye ataka katiba mpya ieonyeshe kutambuliwa kwa uwepo wa MUNGU katika shughuli za mahakama na ilitaje jina lake (MUNGU) wazi wazi...

My Take:
Hili la Pinda najua ni maoni yake na ana haki ya kusema hivyo na ninamuunga mkono kwa kutambua hilo...La Lubuva lina ukakasi kidogo coz ile dhana ya serikali kutokuwa na dini sijui itakuwa implemented vipi lakini vile vile ni Mungu yupi! Maana wengine mungu wao ni wanyama, miti, vinyago nk. Sasa ni Mungu yupi na aandikwe kwa jina lipi coz kama ni Mungu muumba mbingu na nchi, wengine humwita Allah, Mungu, God, Jah nk.....
Pinda Yuko CCM, ni chama Cha KINYONGA wa KIJANI na MANJANO, isikupe tabu ukimsikia sasa akisema madaraka ya Rais yaongezwe Badala ya kupunguzwa.

By the way, wanapoteza muda, Irudishwe mezani Rasimu alosimamia WARIOBA ndo tuanzie marekebisho hapo, tukifanya hivyo miaka 2 inatosha tunapata KATIBA mpya.
 
Back
Top Bottom