Pinda ataka Rais apunguziwe Madaraka

Pinda ataka Rais apunguziwe Madaraka

Mimi nataka kama Ofisi ya Waziri Mkuu inakuwepo, iwe na nguvu ya maamuzi dhidi ya Jairo's ila nafasi ya Makamu wa Rais iondolewe au Viceversa
 
wenye hofu ya kumpunguzia Rais madaraka wanachanganya maneno mawili..........kumpunguzia na kumnyang'anya
 
Mawaziri kutokuwa wabunge ni hoja nzuri kwa mustakabali ya nchi yetu.
 


My Take:
Hili la Pinda najua ni maoni yake na ana haki ya kusema hivyo na ninamuunga mkono kwa kutambua hilo...
La Lubuva lina ukakasi kidogo coz ile dhana ya serikali kutokuwa na dini sijui itakuwa implemented vipi lakini vile vile ni Mungu yupi! Maana wengine mungu wao ni wanyama, miti, vinyago nk. Sasa ni Mungu yupi na aandikwe kwa jina lipi coz kama ni Mungu muumba mbingu na nchi, wengine humwita Allah, Mungu, God, Jah nk.....

"..... Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu"
 
Mi ngependa yaongezwe mfano angekuwa hata na uwezo wa kuvifuta vyama vya siasa vinavyoshabikia vurugu na kuruhusu matumiz mabaya ya ruzuku kama wanaojikopesha.
#uhuru wa maoni.
 


My Take:
Hili la Pinda najua ni maoni yake na ana haki ya kusema hivyo na ninamuunga mkono kwa kutambua hilo...La Lubuva lina ukakasi kidogo coz ile dhana ya serikali kutokuwa na dini sijui itakuwa implemented vipi lakini vile vile ni Mungu yupi! Maana wengine mungu wao ni wanyama, miti, vinyago nk. Sasa ni Mungu yupi na aandikwe kwa jina lipi coz kama ni Mungu muumba mbingu na nchi, wengine humwita Allah, Mungu, God, Jah nk.....

Sioni tatizo la neno Mungu..ndilo la Kiswahili..Allah ni kiarabu, God ni kiingereza. Nadhani sote kwa imani zetu tofauti tunajua Mungu ni Mungu.
 
Mbona hata JK angependa madaraka ya Rais yapunguzwe kuanzia 2015, ni Malecela na mtoto wake labda ili ndugu yao ze utamu aachiliwe au kusamehewa na Raisi na makuwadi wengine ndio fikra zao ni tofauti.

Dah, mkuu unenikumbusha Ze Utamu! Dah, ilibamba sana!

Any way, nirudi kwenye mada, katika vitu ambavyo Jaji Warioba atakera watu ni kutokuingiza kipendele kinachotaka Waziri asiwe Mbunge. Hii imesemwa na karibia kila kundi!
 
Pinda kanena ila huyu mwingine kachemka hilo la mungu katiba itamke vilevile serekali haina dini ila watu wana dini zao kila mtu kwa jinsi atakavyo.
 
Hata aseme nini kwangu mimi namuona MNAFIKI na MSALITI amejua amefulia sasa anatafuta umaarufu wa lala salama
 

......kutambuliwa kwa uwepo wa MUNGU katika shughuli za mahakama na ilitaje jina lake (MUNGU) wazi wazi...


My Take:
.La Lubuva lina ukakasi kidogo coz ile dhana ya serikali kutokuwa na dini sijui itakuwa implemented vipi lakini vile vile ni Mungu yupi! Maana wengine mungu wao ni wanyama, miti, vinyago nk. Sasa ni Mungu yupi na aandikwe kwa jina lipi coz kama ni Mungu muumba mbingu na nchi, wengine humwita Allah, Mungu, God, Jah nk.....
Mkuu, yawezekana umesahau kidogo naomba nikukumbushe kitu muhimu sana.
Je unaikumbuka ile sala inayosemwa mwanzoni mwa kila kikao cha Bunge la TZ? Yule ni Mungu yupi?
Nadhani husemwa...ee mwenyezi Mungu wa rehema, muumba mbingu na nchi........
Basi kama hili limekukumbusha kitu, huyo Mungu anayetakiwa ni huyo.

Kama Bunge linamtambua, wimbo wa Taifa wa TZ unamtambua, basi na Katiba mpya nayo imtambue.
Nadhani yuko sahihi.
 
Sioni kipya katika hoja ya Lubuva, na ninadhani yupo sahihi tu maana kumekuwa na double standards katika mihimili ya utendaji ya serikali. Wakati bungeni wanaanza bunge kwa sala na kwa kumtaja Mungu huyo wa general, mahakama hazifanyi hivyo kabla ya kuanza kusoma hukumu. Ni vema wawe wanaapa mbele za Mungu kwamba watatoa hukumu ya haki.
Kuhusu ni Mungu gani, it doesnt matter, kila mtu atamtaja anayemhusu. Lakini kumfanya mambo kwa uongozi wa Mungu ni jambo la msingi. Mungu anayetajwa bungeni ndiyo huyo huyo atakayetajwa mahakamani. hakuna haja ya kutoa tafsiri nyingi sana juu ya hilo.
 
Pinda ametoa maoni yake vizuri. Jaji Lubuva amepepesa macho! Nchi yetu haina dini!

Kwani ww ni mpagani? Kama nchi haina dini ni kwann viongozi wa serikali wanapoapishwa wanatumia Biblia na Msaafu?pia mbona wkt wa kufungua vikao vya bunge kunakuwa na Dua kuomba baraka ktk shughili zote za siku hiyo?au ni kwann wkt wa shughuli za serikali kama vile siku ya kuwakumbuka mashujaa viongozi wa dini wanaalikwa kutoa Dua? Kumbuka dua zote zinalitaja jina la Mungu aliye muumba wa mbingu na nchi.Tafakari
 
yule jamaa wa Ze Utamuz yuko lupango mandela????


Mbona hata JK angependa madaraka ya Rais yapunguzwe kuanzia 2015, ni Malecela na mtoto wake labda ili ndugu yao ze utamu aachiliwe au kusamehewa na Raisi na makuwadi wengine ndio fikra zao ni tofauti.
 
Nakubaliana na Lubuva. Mungu atajwe katiba. Hata asiyemuabudu Mungu wangu anaye mungu wake.... Hii sio nchi ya kipagani tafadhali. Sasa viapo tutavifanya kwa Mungu yupi? Upinzani kuhusu hili hauna nguvu..
 
Nakubaliana na Lubuva. Mungu atajwe katiba. Hata asiyemuabudu Mungu wangu anaye mungu wake.... Hii sio nchi ya kipagani tafadhali. Sasa viapo tutavifanya kwa Mungu yupi? Upinzani kuhusu hili hauna nguvu..

Mie simuabudu mungu wako na siamini katika kuamini, hivyo sina mungu.

Usifikiri kwa sababu kila mtu kijijini kwako anaamini mungu basi watu wote wanaamini mungu.
 
Wakati Balozi Semfue akitaka rais asipunguziwe madaraka katika katiba mpya, mtoto wa mkulima Mh. Pinda amesema rais ana madaraka makubwa sana na ni vema akapunguziwa madaraka hayo.

Pia ameshauri katiba mpya isiruhusu Waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine kutokana na Bunge (wasiwe wabunge) ili kuwe na checks and balance...

Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi yeye ataka katiba mpya ieonyeshe kutambuliwa kwa uwepo wa MUNGU katika shughuli za mahakama na ilitaje jina lake (MUNGU) wazi wazi...


My Take:
Hili la Pinda najua ni maoni yake na ana haki ya kusema hivyo na ninamuunga mkono kwa kutambua hilo...La Lubuva lina ukakasi kidogo coz ile dhana ya serikali kutokuwa na dini sijui itakuwa implemented vipi lakini vile vile ni Mungu yupi! Maana wengine mungu wao ni wanyama, miti, vinyago nk. Sasa ni Mungu yupi na aandikwe kwa jina lipi coz kama ni Mungu muumba mbingu na nchi, wengine humwita Allah, Mungu, God, Jah nk.....

@Dickson Ng'hily Mkuu na yale Maneno ya liwalo na liwe kisha unatuma vijana kupeleka mtu mabwepande hamkuuliza kama liingizwe kwenye katiba? Kwamba kiongozi atumie secrete service personel kuua watu kwa mateso likubaliwe kikatiba? La, kama halikubaliki Na ikithibitika pasipo shaka kiongozi kataka kuua basi huyo ashughuliwe kisheria bila kujali cheo chake?
 
Mhh? hii mpya. Malecela na Sefue wanapingana na Pinda na Samata. Je wapi wapo sahihi kwa maoni ya wananchi?
Pinda yuko sahihi maana mara kwa mara huwa anapata wakati mgumu kufanya maamuzi mpaka amsubiri rais. Kama mnakumbuka suala la Jairo lilivyomkasirisha lakini hakuweza kumchukulia hatua instantly na mengine mengi. Hivyo yuko sahihi kabisa maana he is a victim of circumstance.
 
Pinda yuko sahihi maana mara kwa mara huwa anapata wakati mgumu kufanya maamuzi mpaka amsubiri rais. Kama mnakumbuka suala la Jairo lilivyomkasirisha lakini hakuweza kumchukulia hatua instantly na mengine mengi. Hivyo yuko sahihi kabisa maana he is a victim of circumstance.
Mkuu nakubaliana nawe! Malecela amekwisha kabisa, kuna jamaa mmoja amesema "kashindwa na kichaa katika kiti cha Ubunge" Sefue nae ni mchumia tumbo, sikumtegemea kusema alichosema. Labda maji ya magogoni yana sumu inayoharibu akili
 
Watu wanafiki tu, ukweli uko wazi na suala si madaraka makubwa ya uraisi bali udhaifu na ubaguzi wa kidini wa huyu tulienae, awamu zilizo tangulia mbona maraisi walikuwa na madaraka haya haya na hayakuonekana makubwa? Ulofa wa huyu aliyopo usitusukume kuifulumusha taasisi ya uraisi, tunaweza tukaiharibu na kuleta migongano isiyo na tija, tusiipime taasisi ya uraisi wa JMT kwa kigezo cha huyu tulie nae, he is absolutely below standard. Kama kweli tunahitaji kuifanyia mabadiliko basi tusubiri hadi mtu makini atakapo kuwepo magogoni ndo tuyapime hayo madaraka ya uraisi.
 
Back
Top Bottom