Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Power is nothing without control,magufuri ana kiburi cha kijinga ngoja apigwe pini na M26
 
Pinda kazi ya Uwaziri Mkuu imemshinda sasa anataka kuwafanya na wenzie waonekane kazi imewashinda kama yeye!Namkubali sana Magufuli na Nchi hii ina bahati kwa Waziri mwajibikaji na mchapakazi kama huyu.Watanzania tabia zetu tunazijua ni watu ambao hatupendi kufuata sheria na tumezoea kudekezwa ili hii Nchi iende sharti tuwe na mtu asiye na muda na siasa wala blah blah kama Magufuli.Sadly huyu mtu ambaye Uwaziri Mkuu umemshinda anaanza kuingilia majukumu ya wenzake!!!??
AnatafutA sifa kwakuvunja sheriya.kama aliliona hilo angelipeleka mswada bungeni .kabla halijaleta madhara.ili lirekebishwe.badala ya kuteteya wala rushwa na wabomowa barabara.kwa jeeuri.kiasi muhindi anaonge
ya na kumkashifu waziri.na bunge zima lililotunga hiyo sheriya.kweli raiya tuliopiga kura kuwachaguwa.tumebutwaaaa.sana.
 
Power is nothing without control,magufuri ana kiburi cha kijinga ngoja apigwe pini na M26

Tatizo siyo ujinga wa Magufuri, ni maamuzi ya kishenzi ya Pinda. Anayesubiri utendaji wa waziri, halafu yeye anakuwa refa.
nahisi anapewa chochote na anaowatetea. Mwanza pia alifanya hayo akitaka kutetea Nyamagana iuzwe. Mkuchika akaja juu na kuweka cheo chake cha naibu Katibu mkuu wa CCM.

Nasikia bado kuna kukaa mishap juhudi na ofa ya Fifa ya kuweka nyasi bandia.
 
Simfagilii Magufuli ila nina swali kwa Pinda. Wakati Jairo alipokusanya fedha ya kutoa rushwa Pinda alidai kama angekuwa na uwezo angemsimamisha kazi. Lakini madaktari walipogoma alimsimamisha Blandina kazi. Kama alishindwa kwa Jairo KM anawezaje kwa Magufuli mbunge na waziri mwenziye? Ten siyo mara ya kwanza. Alishaenda tena kijijini kwake akatangua maagizo ya huyu huyu Magufuli Pombe. Wana bifu gani au mzee wa liwalo na liwe ni msahaulifu au ni mwenye kinyongo.
 
hawa mawaziri hawana mawasiliano kila mtu anajiamulia
same kwa waziri makala na mwambene===oh sory nimemtaja mtu asietakiwa kutajwa hadi kifungo chake kiishe
 
Miongoni mwa watu wanaoiumiza ccm ni pamoja na huyu Pinda ni tatizo kubwa,nina mashaka kama kweli yeye ni ccm?! wa pili anayeiumiza ccm yupo nitamtaja siku moja nimechoka,tena hawa wana nyadhifa kubwa sana ndani ya chama lakini hawakisaidii chama wanakiacha kinataka kuangamia,ngoja wamalize muda wao watuachie chama chetu!
 

Kwasababu Rais KIKWETE anamsifia Mama yake Magufuli sana Mwenge ulipokwenda alitokea hadi kwenye TV na pia Rais alimtembelea

Waziri Mkuu Mwenge ulipokwenda alijaribu kumuonyesha Mama yake Iliishia Magazetini haikufika kwenye TV na hakupata HI 5 toka kwa RAIS...

Sasa hapo ndio WHO's WHO? Unajua tena kama KATIBA ikibaki hivyo Kuna URAIS BARA Unajuaje pia PINDA anautaka???

Mods naomba mniwie radhi kiukweli Pinda ni kiongozi mkubwa serikalini lakini ni dhaifu sana!,wewe kiongozi gani unataka kushughulikia watu halafu unatangaza hadharani eti wapigwe tu?!

Wajifunze kwa Mkapa watu walikuwa wanapigwa kimyakimya tu,ndiyo faida ya kuwa na dola sio kila kitu useme hadharani mengine ni kijeshijeshi tu watu wanastuka wameshashughulikiwa.

Waziri gani mkuu eti analizwa na Albino badala ya kutembeza operesheni tokomeza wauaji Albino anamwaga machozi!aaahhhhhhhhhhhh.
 
Wanajuana Makofuli alikuwa amechemka so mtoto wa mkulima akaja kutudanganya tusione kuwa chama ni kibaya walisha chemka kuweka ushuru sawa na rwanda so agenda yao ilikuwa ku recover kwa njia ya kutesa ma kacompun ya usafirishaji ya ndani so huo siyo mpango wa makofuli ni mpango wa chama
 
Kila mmoja anayefuatilia hali ya mambo na masuala mbalimbali hapa nchini,atakubaliana nami ktk hili.
Tujikumbushe mambo machache; wakati fulani Magufuli alitoa amri ya kubomoa nyumba zote zilizoko kwenye line za barabara na alisema hiyo ni kwa mujibu wa sheria,lkn punde si punde mzee wa 'wapigwe tu' akaitangua amri hiyo.Hivi majuzi Magufuli alitoa amri ya wenye malori yaliyoegeshwa barabarani bila utaratibu kuyaondoa lkn alipokuja 'mzee wa M.26 kwamwezi akaiBAN amri hiyo.
Sasa najiuliza kwa nini viongozi hawa wa serikali wanadhalilishana? Maisha ya kuviziana mwenzako aharibu ndipo ujitokeze kumpanchi sio ustaarabu.Kama Magufuli ni mbabe kwa wananchi Pinda naye ni mbabe kwa waziri mwenzake kama siyo hivyo wawili hawa ni wapinzani kila mmoja kwa mwenzake.Tafakari na toa maoni.

Mgogoro wa maadui zako ni ushindi kwako, yanyamaze hayo mkuu
 
Last edited by a moderator:
Nipo tayari kusahihishwa ,nadhani Magufuli ni "diplomatically one man walking disaster" na Pinda anajaribu kufanya "damage control" kwa maagizo ya ikulu/ rejea amri yake ya bomoa bomoa MTWARA ilivyopingwa na Kikwete na, kumuagiza aache ubabe
 
Kufuatia amri ya waziri mkuu Mizengo Pinda kusitisha hadharani agizo la waziri wa Ujenzi na barabara, John Magufuri kuhusu tafsiri na adhabu kwa uzito unaozidi wa magari ya mizigo, watu wengi tunadhani huu ni wakati muafaka sasa kwa Magufuri kujiuzuru nafasi ya uwaziri kwa kuwa agizo la Waziri Mkuu Pinda linaingilia utendaji wa moja kwa moja wa Magufuri na wizara yake lakini pia linakiuka 'sheria' ambayo John Magufuri aliapa kuisimamia.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kwa Magufuri kuingiliwa utendaji wake na Waziri mkuu Pinda. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye zoezi la bomoa bomoa ambapo baadaye Magufuri alitishia kujiuzuru lakini mwisho wa siku aligwaya na kunywea kimya kimya.

Ili kudhihirisha kuwa John Magufuri ni mtu imara na jasiri(kama watu wengi wanavyoamini), huu ni wakati wake sasa kujiuzuru ili kulinda 'heshima' yake kisiasa na kijamii kuhusu dhana ya uwajibikaji.
 
Kufuatia amri ya waziri mkuu Mizengo Pinda kusitisha hadharani agizo la waziri wa Ujenzi na barabara, John Magufuri kuhusu tafsiri na adhabu kwa uzito unaozidi wa magari ya mizigo, watu wengi tunadhani huu ni wakati muafaka sasa kwa Magufuri kujiuzuru nafasi ya uwaziri kwa kuwa agizo la Waziri Mkuu Pinda linaingilia utendaji wa moja kwa moja wa Magufuri na wizara yake lakini pia linakiuka 'sheria' ambayo John Magufuri aliapa kuisimamia.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kwa Magufuri kuingiliwa utendaji wake na Waziri mkuu Pinda. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye zoezi la bomoa bomoa ambapo baadaye Magufuri alitishia kujiuzuru lakini mwisho wa siku aligwaya na kunywea kimya kimya.

Ili kudhihirisha kuwa John Magufuri ni mtu imara na jasiri(kama watu wengi wanavyoamini), huu ni wakati wake sasa kujiuzuru ili kulinda 'heshima' yake kisiasa na kijamii kuhusu dhana ya uwajibikaji.

Akijiuzuru magufuli kesho naeenda lumuba kuchukua kadi ya ccm
 
Back
Top Bottom