Kila mmoja anayefuatilia hali ya mambo na masuala mbalimbali hapa nchini,atakubaliana nami ktk hili.
Tujikumbushe mambo machache; wakati fulani Magufuli alitoa amri ya kubomoa nyumba zote zilizoko kwenye line za barabara na alisema hiyo ni kwa mujibu wa sheria,lkn punde si punde mzee wa 'wapigwe tu' akaitangua amri hiyo.Hivi majuzi Magufuli alitoa amri ya wenye malori yaliyoegeshwa barabarani bila utaratibu kuyaondoa lkn alipokuja 'mzee wa M.26 kwa
mwezi akaiBAN amri hiyo.
Sasa najiuliza kwa nini viongozi hawa wa serikali wanadhalilishana? Maisha ya kuviziana mwenzako aharibu ndipo ujitokeze kumpanchi sio ustaarabu.Kama Magufuli ni mbabe kwa wananchi Pinda naye ni mbabe kwa waziri mwenzake kama siyo hivyo wawili hawa ni wapinzani kila mmoja kwa mwenzake.Tafakari na toa maoni.