Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Magufuli hakuelewa kwamba wenye malori ndio wenye ccm, Tanzania yetu bana wenye fedha wanasauti kuliko serikali

Na huo ndio ukweli wenyewe,Na baadhi yao wako ndani ya Serikali yenyewe au ndugu/watoto wa vigogo wa Serikali.
 
Pinda anatumiwa tu,Magufuli anaharibu dili za wajanja wachache kwa manufaa ya Taifa hili.
 
Bado Maguguli ana afadhali sana, anasimamia kazi kwa mujibu wa sheria. Sheria haifutwi kwa kuandika barua au agizo la barabarani. Tatizo ni kwamba mabasi na malori hayo ni ya wafanyaboahara wakubwa na wanasiasa wenye influence kubwa CCM. Ni ngumu kushughulika na watu wa aina hiyo kama wewe ni dhaifu au wakubwa wa serikali ni dhaifu. Hongera Magufuli, tunatambua mchango wako tangu awamu ya tatu ya uongozi. Huyu jamaa alikuwa huru akiwa waziri wa ujenzi katika awamu ya tatu kuliko sasa, sijui kwa nini
 
Samahani nitaanza kwa kumkumbuka Mwl J. K. Nyerere. Nimetanguliza samahani maana hapa jukwaani na mtaani watu wanasema hawataki kusikia habari zake, kwa kisingizio kuwa kwani wengine hawapo. Wanasahau kuwa mzee huyu akuishia kuongoza tu, aliandika vitabu vingi pia, ambavyo kwa wasomaji wa vitabu wanapata mawazo mengi ya ku quote toka kwake.
Labda niulize je mnakumbuka azimio la Arusha lilikuwa linasema nini juu ya kiongozi mfanyabiashara? Hamjui kuwa Pinda anahisa kwenye mabasi ya usafirishaji nimesahau jina lake wadau watanikumbusha hapa. Kwa jinsi hiyo kweli mlitegemea yeye amuunge mkono Magufuli kwa hatua hiyo! Kwani Magufuli kaanzisha kitu kipya? Yeye katekeleza matakwa ya sheria tu. Hivi barabara zikiwa zinaharibika mapema nani anaumia zaidi. Obvious ni mwananchi wa kawaida maana serikali itakopa hela ili kuzifanyia matengenezo badala ya kutumia hela hizo kurekebisha huduma zingine kama afya, maji, shule, umeme vijijini n.k. Mfanyabiashara yeye haimuumiizi hilo atakuwa na uwezo wa kwenda hospitali anayotaka, maji anajichimbia kisima umeme ataweka solar kila kitu anaweza kukifanya bila tatizo. Wewe unayesubilia serikali itimize wajibu wake kwako ndo utaumia. Ni nini faida ya kuwa na viongozi wasiosimamia sheria sasa. Kama tungefuata azimio la Arusha, Pinda asingekuwa hapo. Matokeo yake tuliruhusu azimio la Zanzibar lifanye kazi kimyakimya.
 
Magufuli namfananisha kama Mbwa anayebweka lakini hana meno,,,Anatumia mabavu kuliko Akili ona sasa anavyojidhalilisha m/ume ameshatoa tangazo magari yapige mzigo kama kawaida na watafute suluhu. Magufuli alisema hakai na mtu yeyote yule na nina pata shida sana jamaa akiwa Rais maana ana amri za kijeshi.

hana amri za kijesh ila anapenda sifa za kijinga,mwenzie mwakyembe analalamika UCHUMI umeyumba
 
Pinda kazi ya Uwaziri Mkuu imemshinda sasa anataka kuwafanya na wenzie waonekane kazi imewashinda kama yeye!Namkubali sana Magufuli na Nchi hii ina bahati kwa Waziri mwajibikaji na mchapakazi kama huyu.Watanzania tabia zetu tunazijua ni watu ambao hatupendi kufuata sheria na tumezoea kudekezwa ili hii Nchi iende sharti tuwe na mtu asiye na muda na siasa wala blah blah kama Magufuli.Sadly huyu mtu ambaye Uwaziri Mkuu umemshinda anaanza kuingilia majukumu ya wenzake!!!??
hapa sikubaliani na wewe hata kidogo. Hivi unajua ni jinsi gani MAGUFULI WAKO analitia hili Taifa hasara! Hivi gari ya 3.5tons inaweza kubeba kubeba uzito wa kuharibu barabara hata ya Kiwango cha Changarawe tu! Kwa kifupi ni kuwa barabara zetu zinatengenezwa chini ya kiwango ni biashara ya kulindana baada ya kina magufuli kuvuta hesabu ndefu. Open your eyes Mtanzania mwenzangu! Tunatapeliwa na lkuibiwa na kina magufuli tusidanganywe na vikelele vya ajabu ajabu wakati tunaibiwa
 
Magufuli alikua anasimamia hii sheria ya kua all trucks yenye axles 6X4 ipime hivi
Axle ya mbele cabin tani 8
Axle za diff zipime tani 18
Axles za tela zile 3 zipime jumla tani 24
Na ukijumlisha total tonnes za gari zima iwe 50
(8+18+24=50).
Kwahyo ukitoa uzito wa gari tani 20 basi ubebe mzigo usiozidi tani 30.
Hii sheria ilibadilishwa lakini sina uhakika ni lini
Ikaja hii total tonnes ipime 56(9+22+25=56)badala ya 50.sasa kww mda mrefu imetumika ikaonekana magufuli roads zake zinaharibika na ikaja issue ya TATOA KULIA NJAA KUA MZEE AKIWEKA TUPIME 50 badala ya 56 tatoa itawakata sana.
Example unatoka na shaba tani 26 zambia au kongo ni zaidi ya 1500KM na kila tani unasafirisha kwa $120 hivo biashara inakua kichaa.
Pia issue ya mizani kupima uzito tofauti ni kwamba hata hizi matuta yanasababisha mzigo kucheza ndani ya containers na kutobalance axles weight na kusabisha axles kupimwa weight tofauti na ilivyopangwa.
NB:kelele zote za nini why tusitumie railways kusafirisha mizigo kama wenzetu nchi za america wana treni inapakia kontena hata 100 kwa safari moja.
 
Pinda,pindua,pindisha!mbona jina linajieleza?kaanza mizengwe pita pindisha!habari ndo hiyo

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Watanzania m tutaendelea kubaki nyuma siku zote kwasababu ya umbumbumbu wetu na kukosa kwetu maarifa.Leo hii mtu anayechapa kazi tunaanza kumuona adui tunasahau kwamba Serikali ya awamu ya nne imejaa Viongozi wazembe na mafisadi hasa kule kwenye cream.Magufuli huyu huyu chini ya mchapakazi mwenzie Mkapa alifanya mambo makubwa mpaka akatokea kuwa kipenzi cha Watanzania leo hii anafanya kazi ile ile lakini katika mazingira magumu kweli kwasababu walio juu yake ni watu wadhaifu mno na walioshindwa kabisa kumudu kazi zao kule.Rais ni dhaifu na hana ubavu wa kuwajibisha wasaidizi wake wazembe na Waziri Mkuu naye ndio hovyo kabisa bora hata Fisadi Lowassa alikuwa na afadhali.
 
Mmoja anafata sheria,mwingine mnafiki tu anajiita mtoto wa mkulima wakati anasweka kibindoni zaidi ya mil.35 kwa mwezi!
Tumefika hapa kwa sababu hata wale tuliowapa majukumu ya kulinda sheria WANAWALINDA wavunja sheria!
 
liwalo na liwe Magufuli asitishe tu kwani tumemchoka, watu hawa ni hatari sana, badala ya kumwongezea meno waziri mwenzie yeye anaruhusu huaribifu. +kumbukwe kwamba kiwango cha lami tunacho kitumia tanzania ni cha hali ya chini kufuatana gharama za ujenzi, hivyo ili nchi yote iweze kufikika tunashea kitu tulichonacho, sasa anakuja hawa matajiri wanyanganyi wanatuharibia barabara kwa kisingizio cha hoja nyepesi, haya sasa barabara ina mashimo hawa wenye maroli wanatumia masaa mangpi njiani.?
Huyu Pinda kakosea sana angewaacha tuangalie mwisho wao kwani nao wanamikopo, wafanyakazi na n,k
 
Serekali ya Jk imekosa nidham.Viongozi wanafanya kazi ya kupimana ubavu.
 
Kila mmoja anayefuatilia hali ya mambo na masuala mbalimbali hapa nchini,atakubaliana nami ktk hili.
Tujikumbushe mambo machache; wakati fulani Magufuli alitoa amri ya kubomoa nyumba zote zilizoko kwenye line za barabara na alisema hiyo ni kwa mujibu wa sheria,lkn punde si punde mzee wa 'wapigwe tu' akaitangua amri hiyo.Hivi majuzi Magufuli alitoa amri ya wenye malori yaliyoegeshwa barabarani bila utaratibu kuyaondoa lkn alipokuja 'mzee wa M.26 kwamwezi akaiBAN amri hiyo.
Sasa najiuliza kwa nini viongozi hawa wa serikali wanadhalilishana? Maisha ya kuviziana mwenzako aharibu ndipo ujitokeze kumpanchi sio ustaarabu.Kama Magufuli ni mbabe kwa wananchi Pinda naye ni mbabe kwa waziri mwenzake kama siyo hivyo wawili hawa ni wapinzani kila mmoja kwa mwenzake.Tafakari na toa maoni.
Tatizo hapani kwamba mtoa mada hujajiridhisha na facts sorrounding the issues, unaongea kama uko kijiweni.
 
Hivi huyu Magufuri ni yule aliyemuuzia nyumba Kimada pale Ubungo na mdogo wake aliyekuwa akisoma UDSM au ni mwingine nisije nikawa nimechanganya watu. Ni huyu kweli?
 
Uamuzi wa waziri Magufuli ulikuwa ni wa kujitafutia sifa za kijinga kwa gharama za kuhujumu uchumi wa nchi.

Kwa taarifa yenu weigh bridges za Tanroads zina variations za ajabu. Unakuta transporter anapima mzigo mzani wa Kibaha anapata readings X, akipima mzigo huo huo Chalinze bila kuongeza hata kilo moja anapata readings Y, akipima mzani wa Msata anapata readings Z!

Hili ninalisema kwa uhakika kwakuwa nimepata ku deal nao hao watu wa weigh briges (Tanroads). Kwahiyo transporters kutolipia hiyo variation ya 5% ilikuwa ni sawa kabisa.

Hivi Dr. Magufuli hajui kwenye sharia zetu, most of its section ni copy and paste? hazifanyi kazi kabisa......msomi aliesoma huko kwa MaCCM lazima upate shida kusimamia unayoamini based on professional ethic.
 
Magufuli aliwahi kutoa Amri, Nyumba pembezoni mwa barabara ya kutoka customs bukoba mjini kuelekea stendi zibomolewe kupisha Upanuzi wa barabara/double road, Pinda akaingilia kati kwa kusema ukizivunja hizi unakuwa umekarudisha kamji ka bukoba nyuma sana, ni heri itafutwe route nyingine ijengwe barabara hii.

Pamoja na kufanya mambo kwa mujibu wa sheria, lakini Magufuli anahitaji busara zaidi, Sheria zipo kwa ajili ya watu na si watu kwa ajili ya sheria. Uhalali wa sheria unakuja pale unaposimamia maendeleo bora ya raia na si kutumika kuwarudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom