Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,469
- 1,697
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa mtendaji wetu mkuu wa serikali yetu tukufu inayo ongozwa na Mama yetu mpendwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nakuomba kwa moyo mweupe na wa huruma kubwa ya watanzania wengi wanaolilia maendeleo yetu na ya vizazi vyetu kwa dhati kuwafukuza na ikibidi kuwafungulia mashtaka watu wote walio husika katika kuchelewesha mradi wetu wa Machinjio ya Vinguti.
Enough is enough! Watanzania tunasema; "tumechoka" kuwa na watumishi na watendaji wa serikali wa aina hii wasiojitambua na kujua nini ni majukumu yao ya uwajibikaji katika kutoa huduma ambazo ni chachu ya maisha na maendeleo yetu na ya vizazi vyetu vya baadae.
Sisi sote tunatambua kuwa ongezeko la watu nchini kwa mwaka ni kubwa sana kiasi ambacho kwa upande mwingine tunahitaji kuwa na Balance ya vitu ambavyo vitatuwezesha sisi kuwa na uwezo wa kuwapatia vijana wanao maliza elimu kulingana na uwezo wao ajira ili kujikimu maisha yao na ya falmilia zao.
Sasa tukiwa na watu kama hawa ambao wanafanya kazi zao kwa kusuasua kama hivi, hilo kwangu na mbele ya watanzania wengi wanao penda maendeleo ya kweli ni kitu ambacho hakiwezi kukubalika. Hali hii ya utendaji wa kazi usiokuwa wa ufanisi mkubwa kama huu ni hujuma ya uchumi ambao una maafa makubwa kwenye maisha, amani, umoja na maendeleo ya watanzania na nchi yetu kwa ujumla. Watu wanaofanya hila ya namna hii kwa makusudi, hawana budi kuadhibiwa vikali ili liwe fundisho kwao na kwa wengineo wote wenye malengo kama haya ya makusudi ya kuya hujumu maisha yetu na yale ya vizazi vyetu baadae.
Mimi nakaa na kuwaza sana, jinsi hawa watu wanavyo fanya matendo ya kiuaji kama hayo, hivi wanafikiri nini hasa kwenye akili zao? Ina maana wao hawaoni wala kusikia matatizo ambayo vijana wetu wengi wanakabiliana nayo siku hadi siku ya kuhangaika mitaani na maofisini wakitafuta ajira ili waweze kujikimu na maisha yao?
Huyu mama wa National Hounsing na wahusika wengine wa huu mradi walikwisha mahidi Hayati Rais Magufuli alipokwenda kuukagua huo mradi miaka miwili iliyopita kuwa mpaka kufikia mwezi 12/2020 ulitakiwa uwe umesha kamilika. Kwa bahati mbaya tarehe iligonga na mradi haukuwa umekamilika. Naomba tujikumbushe kidogo na hii clip ya ziaara ya kushitukiza ya Hayati Rais Magufuli;
Baada ya Hayati Rais Magufuli akafuatia mkuu wa Mkoa wa wakati ule Mh. Paul Makonda kuutembelea huo mradi, ahadi nyingine ya kukamilika kwa mradi ikatolewa na wananchi na hasa wakazi wa Dar es salaam wakawa na matumani ya ajira na shughuli nyingine za biashara na matamanio ya kupata nyama bora na salama kutokana na mradi huo, hiyo kama ilivyo kawaida haikutokea tena. Ushahidi ni hii clip ya mkuu ya mkoa Mh. Paul Makonda;
Baada ya Mh. Paul Makonda, aliyekuwa mkuu wa mkoa mwingine wa Dar es salaa Mh. Kunenge naye aliutembela huo mradi, kwa mara nyingine tena naye alipigwa mzinga wa ahadi ya kukamilika soon;
Na hatimaye wewe Waziri Mkuu mwenyewe nawe ulisha utembaelea mara mbili huo mradi mara zote ukapigwa date za kukamilika kwake mwaka huu na wao bila hata ya haibu, kama kawaida ilivyo ukadanganywa danganywa na pilika pilika zao za uongo za hapa na pale wakijifanya wanafanya majaribio ya kuchinja ng'ombe nawe ukauingizwa mkenge wa ahadi zao za uongo. Ukakubali kuwa tarehe moja ya mwezi saba mwaka huu, ndiyo altumatum ya huo mradi kuwa umekamilika.
Jana tarehe nane mwezi huu mkuu wa mkoa wa sasa wa Dar es salaam Mh. Makalla naye kawashitukizia kwa kuutembelea huo mradi kwa mara nyingine tena na tena kama kiongozi, cha kushangaza ni kwamba mambo ni yale yale na hakuna uhakika wa kumalizika kwa huo mradi soon.
Kama ilivyo kawaida mkurugenzi "Chauongo" wa National Housing anakuja na mengine tena. Sasa hivi ni Boiler ndiyo tatizo na mengineyo kadha wa kadha yamejitokeza ambayo huko nyuma hatukuyasikia.
This is ridiculous and it is disgusting kuona watanzania wenzetu wachache waliopewa uaminifu na wananchi kuwatumikia kwa ufanisi ulio tukuka wanafanya mambo ya kijinga na ya kuwafedhehesha viongozi wetu, wakati watu wenye mamlaka ya kiutendaji kwa mujibu wa katiba na sheria zetu wapo na haya mambo wanayaangalia tu na hawachukui hatua zozote zinazo paswa.
Mimi najiuliza hivi wakati wanaanza kuutekeleza huo mradi hakukuwa na Milestone ya maendeleo ya huo mradi ambao uliwawezesha hao wahusika kutambua kitu gani kianze lini na kiishe lini? Mpaka leo tunasikia mambo mengine ambayo hata hatukuyasikia huko nyuma?
Waziri mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa hivi ile barabara na vile vizimba walivyo kuahidi kujengwa na pia pavements wataanza lini na kukamilisha lini? Mambo kama haya waziri mkuu unataka yaendelee mpaka lini ili wewe na serikali yako uweze kuchukua hatua stahiki?
Waziri mkuu na mawaziri wengine husika watendaji wa aina hii ni mfano mbaya wa matumizi ya pesa za umma na utendaji mbovu wa watumishi wa serikali? Sio kitu cha ku-tolerate hata kidogo.
Mh. Waziri Mkuu inakuwaje nyie kama viongozi wetu tuliowapa mamlaka ya kutuongoza mnawaacha hawa watumishi na watendaji wasio taka kuwajiba kuendelea kututendea mambo mabaya kama haya? , Mnajua mambo mnayo waonyesha wananchi kwa vitendo vyenu vya kuendelea kuufumbia macho ufanisi mbovu wa watumishi wa serikli na mashirika ya umma mlio wachagua? Kuna haja kweli ya kuendelea kuwahurumia hawa watu kutuwakilisha sisi katika positions walizo nazo za utendaji ambazo zinaonekana kuwa hawaziwezi na kuleta taswira mbaya kwa wananchi na hasa vijana wetu tunao wategemea kutuongoza baadae?
Hawa watu wanajua kweli kuwa kitendo chao cha kukuhadaa wewe waziri mkuu na viongozi wengine ni ukiukwaji wa sheria ya kuto tii amri ya viongozi wenye mamlalaka juu? Hawajui kuwa kisheria ni kitu ambacho hawatakiwi kukifanya?
Mimi najiuliza hivi wao wanaujuzi au maarifa ya aina gani ambayo yanaifanya nchi ya watu takriban milioni sitini isiwe na watu wengine wenye maarifa hayo waliyo nayo wao? What is so special with them, kiasi kwamba tunawang'ang'ania wao waendelee na utendaji ambao hauna tija kwenye maisha na maendeleo ya jamii yetu?
Nitashangaa sana kama nitasikia kuwa hakuna hatua yoyote iliyo chukuliwa juu ya watendaji wa mradi huu. Itaonekana kuwa Waziri Mkuu unauza sura katika mambo kama hayo, lakini ukweli wake ni kwamba huna lengo dhahiri la kutatua tatizo hilo. Ni kitu ambacho hakikubaliki Waziri wetu. Hayo mambo wanayoyafanya ni subortage ya uchumi na maendeleo ya watanzania. They should stop doing it!
Naomba kwa unyeyekevu mkubwa kuwasilisha mada yangu! Asanteni sana!