Tupende tusipende, bado Tanzania inahitaji viongozi wenye nusu ya hulka ya Hayati Magufuli

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Habari wana JF, natumaini wote baadhi yenu ni wazima wa afya, na wale wasiyokuwa wazima afya, nawaombea mtakuwa wazima afya pia.

Kabla sijasema sana napenda kuweka wazi kuwa mimi siyo mnazi wa Chama chochote cha siasa ila ni kijana tu niliyefanikiwa kuwepo na kutambua mambo kwa uhalisia wake toka awamu ya mzee mkapa, jk, jpm na sasa SSH, kwaiyo ninaweza kwa kiasi changu kuelewa mambo fulani kwa kiasi changu. Kwa mtizamo huo nimegundua uongozi wa nchi siyo swala jepesi sana, na nyakati zote unapokuwa kiongozi wa nchi, viongozi wengi waliopo chini yako hutazama kwa kiasi kikubwa attitude ya kiongozi wa juu, zaidi ya maneno yake na maagizo yake katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Sipendi kurudi nyuma na kutazama sana awamu za nyuma zaidi, napenda nianze hapo tu kwa JPM.

Pamoja na mabaya yake as individual, ila ukweli ni kwamba at least kwa miaka 10 Tanzania ilimuhitaji na bado inahitaji kiongozi mwenye kaliba ya JPM. Aliwezakutoa msimamo, miongozo, masmuzi na kufuatilia na kuhakikisha matakwa yake yametimizwa na kwa hakika Kuna mambo yalionekana wazi kufanikiwa zaidi, kama uwajibikaji kwa viongozi wa umma, utekelezaji wa miradi tena kwa muda uliopangwa, kuwawajibisha viongozi wazembe bila aibu, wala kificho, kusimamia rasilimali za nchi yetu kwa manufaa maana ya taifa, kuliko wakati huu tuliopo na hii kwa kiasi ilifanya nchi yetu ikaanza kuonekana as a sleeping giant who is now waking up.

Kwa kiasi kikubwa pia hata mawaziri na viongozi wengine walijitahidi kwenda na mwendo wa JPM maana kupitia attitude yake ilikuwa wazi there was no joke. Ila kwa wakati huu wa SSH ni wazi na inaonekana kwa watanzania wote kuwa now is a joking time. Mawaziri wanafanya wanachojisikia, juzi SSH alikuwa anafungua barabara sehemu fulani ila hata urefu wa barabarani iyo alikuwa hajui, waziri incompetent kama Mwigulu leo kapewa wizara nyeti fedha, tunachohudia ni utoto kabisa kwa kiongozi mwenye PhD kushindwa ku-analyze vyanzo tofauti vya mapato na kuisadia serikali kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wake, zaidi ya yote akili yake imeishia kwenye tozo.

Pamoja na ukame na mabadiliko ya hali hewa duniani, bado wakati wa JPM tuliweza kupata umeme wa uhakika chini na waziri Kalemani na wenzake, Leo ndugu yetu Makamba amepewa wizara, umeme kukatika tumeshazoea, ila najiuliza kama ni kweli hawa viongozi waliopo sasahivi wana nia ya dhati ya kurahisha mazingira ya kupata maendeleo kwa wananchi, Makamba anatambua kila nusu saa inayopita bila umeme ni kiasi gani kinapotea kwenye sekta ya biashara, uzalishaji, usindikaji, ufungashaji, uhifadhi na hata sekta nyingine hapa nchini? Kama lengo la dhati la Rais SSH ni kuleta maendeleo, ameshawai hata kumwita huyo waziri na kumuhoji haya yote kama kiongozi mkuu wa nchi? Je yeye mwenyewe haoni sababu ya kujiuzulu kwa kushindwa kazi maana kujiuzulu ni sehemu ya uwajibikaji?

Hayati Magufuli alifikisha umeme kwenye Vijiji takiribani 9000 Kati ya 12000, je Kati ya vijiji elfu 3000 vilivyobaki, yeye amegusa hapo vingapi? Ni Imani yangu kuwa pamoja na ubaya wa JPM as individual bado hitaji la viongozi wenye kaliba yake ni kubwa hasa kwa nchi yetu na naamini later or sooner tutapata mtu mwingine kama yeye na siyo lazima atoke chama tawala na maendeleo yataoneka. Kama kweli Tanzania inahitaji mabadiliko na maendeleo ya kweli ni wakati sasa wa kuachana na vyama na kutafuta individuals wenye capability, tuwape nafasi na ushirikiano tutoke hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom