CCM kwa hili tunamkosea sana Rais Magufuli

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Wanabodi...

Niwasabahi kwa kuwatakia asubuhi njema na natumai mko fresh kabisa.
Kabla sijaenda mbali Mwalimu wangu wa Sheria pale chuo kikuu aliwahi nifundisha kuhusu "ku-declare interest", naomba ifahamike kwamba mimi ni Mwanachama Hai wa Chama Cha Mapinduzi na Mzalendo nambari moja kwa Taifa hili.

Naomba Wana CCM na Watanzania tuwekane sawa kwenye hili sababu linatuhusu wote, nashangaa sana wasomi , wanazuoni na wanachama wa CCM tunafanya kama hatukumbuki, au tumepoteza kumbukumbu sijui .

Mhe Kessy, mbunge wa Nkasi juzi alinukuliwa na vyombo vya habari Bungeni akisema Rais Magufuli aongezewe muda " Atake Asitake", akanukuliwa pia akisema "Asiachiwe huyu, alazimishwe" akaendelea kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye janga la Corona mataifa yote ya nnje yamemkubali.

Na Mhe Spika Ndugai akajibu, ngoja twende kwenye uchaguzi mkuu, tukirudi Mhe Kessy utaleta hili hili Azimio la Rais kuongezewa muda na naamini wote tutarudi, na lazima tutamuongezea muda."

Kiukweli, Binafsi nimesikitishwa sana na hii kauli ya Mhe Kessy kwa hoja zifuatazo,

Mosi, ikumbukwe tarehe 14 januari 2018, Rais Magufuli alikutana Ikulu na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole na hiki ndiko Rais John Magufuli amesema ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na mjadala ambao unaoendelea wa rais kuongezewa kipindi cha kutumikia kutoka miaka mitano hadi saba.

Amesema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni kufuatia Mhe Juma Nkamia mbunge wa Chemba kuibua Hoja ya Kuongezewa Muda wa Urais toka Mitano mpaka saba.

Pia Rais Magufuli alitaka wananchi KUPUUZA mjadala huo.

Ndugu Humprey Polepole nae wakati anaongea baada ya kutoka Kwenye Mkutano na Rais alisema Magufuli aliwataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi, badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM iliyonadiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kupitia kitabu chake cha "Uongozi Bora ba Hatima ya Nchi yetu", Mwalimu Nyerere alishatoa Angalizo kuhusu kuongeza kipindi cha Urais , namnukuu Mwalimu na anaendelea kuonya tena, "Suala hili lilikwishakuamuliwa zamani, na sasa ni sehemu ya Katiba yetu. Uamuzi huo inafaa uheshimiwe. Rais Mwinyi ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Yeye akisema kuwa vipindi viwili havitoshi, na akataka viwe vitatu; Rais wa pili atasema vipindi vitatu havitoshi, na atataka viwe vinne na kadhalika mpaka tufikie Ngwazi (rais wa milele) wa Tanzania," (uk.10).

Kwa hii kauli ya Mwalimu Nyerere wabunge tunakwama wapi?

Ina mana hatujui tunachokisema?

Je, ni kweli hatuna uhakika wa kurudi kwenye Bunge la 12 kwa hiyo tunatamka chochote huku mwishoni ili tupate "Political Empathy"?

Wana CCM wenzangu, lazima ifike mahali tukubaliane na msemo wetu tunaosema kila siku " TUNASIMAMA NA RAIS MAGUFULI,", basi hata kwa hili analosema "Hafikirii hata siku moja kuongeza siku hata moja baada ya kipindi chake kuisha,", " Rais akasema ANAKWAZWA na hafuraishwi na mjadala wa kuongezwa muhula wa uongozi"

Rais Magufuli amenukuliwa mara mbili tofauti akiwajibu wale wote wanaomlazimisha aongeze muda, na Rais wetu hajazunguka kimaneno, kasema plain black and white "SITOONGEZA MUDA HATA WA SIKU MOJA BAADA YA KIPINDI CHANGU KUISHA", nakumbuka hii ilikua disemba 2019 alikua anatoa hotuba mahali.

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Dr Bashiru nae alipokua pale Chemba akimtumbua Katibu wa CCM mkoani Chemba kwa kukosa Kujiongeza kuiva na viongozi wenzake alilisemea hili jambo, akasema " Rais Magufuli atamaliza miaka yake kumi, hiyo tutampa ridhaa badala ya Hapo atafata utaratibu wetu wa kikatiba wa kuachiana vijiti"...

Hivi wabunge wanataka KUTUAMINISHA wana nguvu zaidi ya wananchi waliowachagua?

Hivi Spika wa bunge Ndugu Ndugai anaposema BUNGE TUTAMUONGEZEA muda anaelewa kweli?

Hivi Spika hakumbuki TUME YA JAJI NYALALI(NYALALI'S COMISSION), miaka ya 1998 9 na ile kazi ya kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba?

Kwamba lazima wanachi wafanye kitu tunaita Referendum .,

Kukawa kuna kitu kinapita mtaani kwa jina la "WHITE PAPER"? Chenye lengo la kutaka kujua maoni ya watanzania kuhusu jambo husika la kurekebisha kwenye katiba yetu.

Kwa nini Spika useme " TUTAMUONGEZEA MUDA" maana yake unasahau sisi wananchi wa kawaida na nguvu yetu kwenye maamuzi.

Hivi Mhe Kessy kweli anataka tuamini hajasikia maneno ya Katibu Mkuu wetu Dr Bashiru kuhusu mjadala wa ukomo wa Urais.?, Katibu Mkuu alitamka ameufunga Rasmi disemba 2019 au Mhe Kessy ana nguvu zaidi ya Dr Bashiru??, kitu akishasema Katibu Mkuu wa Chama wewe mwanachama wa kawaida una comply nacho..Hauna haja ya kuropoka tena maana Msimamo wa Katibu Mkuu ni msimamo wa Chama.

Waziri Kabudi nae alishatolea ufafanuzi hili jambo wakati akiwa Katiba na Sheria , akasema vipindi vya Urais ni VIWILI tu vyenye miaka Kumi Kumi ndanu yake.

Simlaumu Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Mizengo Pinda siku ile aliposema "Anatamani Rais Magufuli aongezewe muda wa Urais"..

Mhe Pinda alikua anatoa maoni yake kama mtanzania wa kawaida, kama mimi na wewe, lakini baada ya Rais Magufuli kutoa msimamo wake kuhusu hilo ombi , binafsi sijamsikia Tena ndugu Pinda anakuja kwenye media na kuanza kumbembeleza Rais.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu kutoa maoni, hata wakati Rais Kikwete anamalizia uongozi wake 2009 kulikua na watu wakimtaka Rais Mstaafu Kikwete aongeze muda wa kukaa kwenye Urais..

Waziri wa katiba na sheria mhe Chikawe wakati huo akatoa msimamo kwamba Rais Mstaafu Kikwete hatoongeza tena muda wa Urais.

Narudia tena, Ndugu Juma Nkamia alikua amepeleka hoja yake binafsi ya kuongeza Kipindi cha Urais toka miaka mitano mpaka saba lakini baadae aliitoa hii hoja yake akasema " Ameshauriwa na viongozi wake wa juu wa Chama cha Mapunduzi aitoe na asiendelee na hoja yake japo Nkamia aliileta hoja yake mara mbili lakini alivyoambiwa aitoe, ALIITOA", na hii inaitwa UTII kwa viongozi wako wa CHAMA.

Pia Mhe Mizengo Pinda hakuendelea na hoja yake mara baada ya msimamo wa Rais Magufuli, kwa nini Mhe Kessy anakomaa?, unaweza kuona "countance" (mwonekano) wa Mhe kessy pale Spika Ndugai alipomwambia "Utarudi kwenye Bunge lijalo la 12 na utakua ni wewe mletaji wa Azimio hili".

Ukiisoma Body Language ya Mhe Kessy unaona kabisa anafurahi kusikia atarudi kwenye Bunge lijalo!

Anafurahi kuambiwa atakua mletaji hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Kuongeza ukomo wa Kipindi cha Urais!.

Kifupi mhe Kessy anataka kurudi bungeni, which is okay lakini rudi bungeni with your own expense!, sio unarudi bungeni with expense' of the Nation.

Leo kila mbunge atake Katiba ibadilishwe ili apate debe/upendeleo wa kurudi bungeni toka kwenye Kamati Kuu ya CCM si kila siku tutakua tunabadilisha katiba yetu .

Nkamia alikua anataka ku-copy paste Katiba ya Rwanda ambayo toka 1994 ilikua inasema Kipindi (tenure) ya uongozi wa Urais ni miaka saba saba , lakini Rwanda wamefanya mabadiliko kwenye Katiba yao na kuanzia Mwaka 2024 Rwanda wanarudi kwenye tenure ya miaka mitano mitano, , Rais akae miaka kumi tu madarakani ampishe Mwenzie.

Kifupi Rwanda wanatamani kuwa kama sisi lakini Sisi ndo kwanza Tunataka Rais Aongezewe miaka 10 zaidi kutoka 2025 yaani Rais Magufuli atumikie mpaka 2035.

Mi nampenda sana Rais wangu kwa kazi alizofanya na anazoendelea kufanya.

Naipenda spirit yake ya kujitegemea na "will power" yake kwenye kufanya mambo na maamuzi kama Taifa hakuna sehemu nam-doubt Rais Magufuli.

Ni will-power yake na roho yake ya kizalendo kwa Taifa hili imetufikisha hapa tulipo, maofisi ya serikali yana nidhamu, wanyonge wanasikilizwa na kupewa HAKI.

Rais Magufuli amefanya Maamuzi ya kipekee sana kwenye kushughulikia suala la Corona, ametujengea Roho ya kipekee kwenye Kipindi hiki Taifa limepitia kwenye Huu ugonjwa.

Rais Magufuli kawajibisha wakuu wa mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za serikali pale Rais anapobaini mambo hayaendi!...unakumbuka kuvunjika kwa Daraja pale Morogoro?, unakumbuka Waziri Kamwele alivyochanwa Live kwa kutomuajibisha Meneja wa TANROADS wa mkoa?

Unakumbuka Rais alivyowachana Magereza na TBA pale Ukonga kwenye mradi wa nyumba za jeshi la magereza?

Na akawaambia live atawaletea Kamishina wa MAGEREZA toka JWTZ?

Unakumbuka JKT walivyoendeleza ujenzi wa zile Nyumba na Ukaisha?

Hii ni mifano michache ya Rais Magufuli, bado uthubutu wake wa Kufufua Mashirika ya UMMA kama ATCL .

Sitozungumzia ujenzi wa madaraja, barabara, vituo vya Afya kila kata, Elimu Bure, Mikopo ya Elimu ya Juu n.k maana hivyo kila mtu anavizungumzia.

Binafsi naungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Dr Bashiru , Naungana na Rais Magufuli na Msimamo wa Chama kwa Pamoja Kumruhusu Rais Magufuli apate kipindi cha Pili cha Uongozi kwa miaka mingine mitano mpaka 2025.

Vivaa Magufuli....

Mzee Pius Msekwa alikua mmoja wa wazee walioshughulikia mabadiliko anuwai' yaliyokua yanafanyika kwenye Katiba ya Tanzania toka ile ya 1921 .

Anajua tulikotoka na mabadiliko yote tuliyofanya zaidi ya mabadiliko 12 na alisema wazi kabisa "Toka enzi za Mwalimu tulishazungumzia kuhusu kuongeza muda wa Urais".

Wana CCM na hasa vijana wenzangu wa UVCCM tusimkwaze Mhe mwenyekiti wetu Dr Magufuli, kashasema HAPENDEZWI, ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na hizi kauli zetu huku kwenye mitandao tunapiga kelele za kuongeza muda wa Urais.

Rais Magufuli nae ana maisha yake ya kifamilia, tumuache apumzike na tumshukuru kwa Mchango wake mkubwa kwenye Taifa hili la Tanzania na alishasema Mara Nyingi " Urais ni KAZI NGUMU".

Alishasema analala na mafaili pale IKULU wakati mwingine tafadhali tuheshimu maamuzi yake.

Tuachane na wanasiasa walio tayari kusema lolote mradi mradi tu warudi bungeni hata ikibidi kurudi "in expense" (kwa gharama) ya kubadilisha katiba....

Laiti Rais mstaafu Jakaya Kikwete angesema aongeze muda basi leo hii tusingempata Rais Magufuli, haijalishi kapatikanaje lakini kapatikana na kwa Miaka hii mitano kalinyanyua hili Taifa akiwa na Timu yake aliyoichagua na Kuiamini.

Sasa akisimama Mbunge kama Mhe Kessy akasema "Haoni mtu mwingine wa kutuvusha baada ya Magufuli", mi namshangaa Mhe kessy..sijui alikua anawaza nini.

Nafunga kwa Maneno ya Rais Magufuli anasema " MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU"...

Na ameshasema zaidi ya mara moja, na viongozi wa Chama na serikali wameshaongea kuhusu kuongeza muda basi TUSIMKWAZE mpendwa wetu Rais Magufuli.

Tutashinda Uchaguzi huu Mkuu wa oktoba na Chaguzi zingine Miaka mingine sababu tunaaminika na wananchi.

Ndugu Humprey Polepole aliulizwa siku swali kwenye redio unadhani siku CCM ikiondoka madarakani tatizo litakua nini?

Na napenda jibu alilotoa, "Kwa sasa CCM haitotoka madarakani kwa mabadiliko haya tuliyofanya", Lakini huko baadae CCM ikianza kudharau wananchi basi itaanguka na kuondoka madarakani"

Tueshimu Msimamo wa Rais Magufuli kuhusu kutokuongeza muda wa Urais na tumshukuru Kwanza yeye na serikali yake kwa kazi nzuri waliyofanya ndani ya miaka mitano na tusimame nae kwenye hii miaka mingine mitano mpaka 2025.

Nimeona Niliseme hili wazi na tafadhali moderators msiunganishe huu uzi na nyuzi zingine maana haufanani na nyuzi zingine maana hamkawii kunikwaza asubuhi

"MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA TANO".

NB: Kwa maoni au ushauri usisite kumuandikia muandishi kwenye barua pepe : godjohn8@gmail.com
 
Tatzo la wabunge wa hivi linatokana na sisi wananchi kuwarudisha hivi tunashindwa nini kuwagomea wasirudi tena awamu ijayo? Kwanini wabunge wanakua juu ya wananchi ambao kimsingi ndo waajiri wao? Nazan ifike muda sasa hawa wabunge wawaheshimu waajiri wao.
 
We naye, gazeti loote Hilo unajidai kujali na kuheshimu mtazamo wa Magu kwa hili...huu nao ni unafiki, Kwani Mambo yote yanayosemwa na Magufuli umekuwa ukiyakubali, kuyaheshumu, na kuyatii? Hilo la kuongezewa muda siyo la Magu, ni la watz na Magu kwa hili Hana choice! Na kwa kweli anatendewa haki!
 
Hongera kwa maoni na mtazamo wako kwa mujibu wa katiba, sio vibaya kwa wanaoshauri hilo pengine ubaya ni kupoka mamlaka ya wananchi hasa kwa namna ya uzungumzaji wa wabunge, hoja ya namna hii ikipelekwa bungeni si itapata fursa ya referendum?wananchi watapewa fursa ya kukubali au kukataa, uhuru wa maoni , mawazo, fikra ni pamoja na tusiyoyapenda na tuyapendayayo, binafsi naamini uongozi ni kujitolea na ni uzalendo, Mbona Nyerere alikaa miaka 23, Katiba sio biblia kwa nia na utashi jumuishi inaweza badilishwa, kama kiongozi anafaa why say no?uhakika wa kupata viongozi wenye maadili na kuendeleza maendeleo upo? pengine yafaa mjadala hapo mbeleni wa why no na why yes? Tusiogope mijadala tuvae ujasiri tuzungumze na kila mtu aheshimiwe kwa maoni ndio matunda ya utashi na uhai wetu
 
Huu ndio uzalendo na hawa ndio wazalendo!.
Asante mtoa mada very exhaustive, very objective with ample references
P
Na wew uache unafiki uwe objective kama nguri.Waandishi nguri kama nyie muwe msaada kwa jamii badala yake umejaa unafiki huku ukitumia literal terms ambazo hazina impact kwa jamiii.You are neither part of ruled nor rulers.Your hypocricy ruin your intergrity as senior journalist
 
Huu ndio uzalendo na hawa ndio wazalendo!.
Asante mtoa mada very exhaustive, very objective with ample references
P

Basi mwenyewe hapo unaona / kujiona una Akili kweli kweli na umeandika cha maana kabisa na Kiingereza chako cha Kujifunzia Ukubwani kabisa.
 
Huu ndio uzalendo na hawa ndio wazalendo!.
Asante mtoa mada very exhaustive, very objective with ample references
P

P.
Mtoa mada ameongea Ukweli na Uzalendo mtupu.
Tatizo ni hawa wenzetu wa CCM kujifanya WANAMPENDA MAGUFULI KULIKO TANZANIA....!!!Huu ni wendawazimu na wehu!!

Ushauri kwa Rais Magufuli:
RAIS MAGUFULI ATALIVUNJA BUNGE LA JMT TAREHE 19.06.2020 NINAOMBA AFANYE YAFUATAYO;
  1. AMKEMEE SPIKA NDUGAI NA WABUNGE WOTE WANAOTAKA RAIS AONGEZEWE MUDA.
  2. ATANGAZE RASMI MTU YEYOTE ATAKAYE SIKIKA ANATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA ASHTAKIWE KWA UCHOCHEZI.
Kama Magufuli hatafanya Kati ya hayo 2 au yote basi Watanzania wajue na Yeye yuko nyuma na Ni sehemu ya Mpango huo OVU.
 
Asante sana Pascal....

Tanzania Yetu sote.

Nijikite kwenye uzi wako namba moja. Nayaheshimu mawazo yako, na kwa kiwango fulani umejitahidi kwa kiwango cha kuridhisha kuongea ukweli, hata kama ni ukweli wa upande mmoja. Ninaona fika umekwepa kuongea ukweli halisi kutokana na mambo ya mahaba niue, ndio maana umeshindwa kujua ni wapi Kessy, na Ndugai wanapata jeuri ya kutaka kumuongezea muda Magufuli.

Ninapinga na kukataa kwa nguvu zangu zote kuwa Magufuli hataki kuendelea kukaa madarakani. Anataka sana, ila anatumia mbinu za Hadaa kuwa hataki. Sababu kubwa hasa ya kuwa anataka kuendelea kukaa madarakani iko wazi. Yeye ndio anayeagiza chaguzi za nchi hii zinajisiwe kwa faida yake binafsi, na chama chake. Toka ameingia madarakani, box la kura limedharaulika kupita maelezo, na viongozi wanaopatikana, hawapatikani tena kwa ridhaa ya umma, bali kwa utashi wake. Sasa kama viongozi wanaopatikana wanapatikana bila ridhaa ya umma, unategemea hawatamuongezea muda wa kukaa madarakani? Kama hao viongozi wameshajua kuwa wakimsifia na kusema akae madarakani zaidi, watarudi tena bungeni maana hamna uchaguzi, kwanini wasiseme akae madarakani zaidi?

Ni kweli Magufuli ni mchapakazi kwa asili, na kuna baadhi ya mambo anafanya vizuri, ila hafanyi hayo kwa hisani bali ni wajibu wake. Lakini Magufuli kwa asili ni mtu mwenye uchu wa madaraka, na hilo halijifichi. Na huwa anatumia mbinu zote, hasa hasa chafu ili kupata madaraka, kwani hana uwezo wa kushawishi kupata kura. Kama utakuwa ni mkweli, fuatilia alipokuwa mbunge, ni mara ngapi alishinda kwa njia ya kura, na ni mara ngapi alikuwa mbunge bila njia ya kura, na alifanya nini ili kuupata huo ubunge. Na Magufuli pia sio mtu mkweli, bali amejaa hadaa, visasi na mambo mengine ambayo si vyema kuyasema hapa, na anaweza kufanya lolote ili kupata madaraka, ikiwemo kufanya mauaji. Hao akina Kessy na Ndugai wanajua Magufuli anataka nini, ndio maana wanasema hayo bila woga.
 
Tatzo la wabunge wa hivi linatokana na sisi wananchi kuwarudisha hivi tunashindwa nini kuwagomea wasirudi tena awamu ijayo? Kwanini wabunge wanakua juu ya wananchi ambao kimsingi ndo waajiri wao? Nazan ifike muda sasa hawa wabunge wawaheshimu waajiri wao.

Kama wanapata ubunge bila ridhaa ya wananchi, ni wazi watafanya wayatakayo na sio watakayo wananchi.
 
Hongera kwa maoni na mtazamo wako kwa mujibu wa katiba, sio vibaya kwa wanaoshauri hilo pengine ubaya ni kupoka mamlaka ya wananchi hasa kwa namna ya uzungumzaji wa wabunge, hoja ya namna hii ikipelekwa bungeni si itapata fursa ya referendum?wananchi watapewa fursa ya kukubali au kukataa, uhuru wa maoni , mawazo, fikra ni pamoja na tusiyoyapenda na tuyapendayayo, binafsi naamini uongozi ni kujitolea na ni uzalendo, Mbona Nyerere alikaa miaka 23, Katiba sio biblia kwa nia na utashi jumuishi inaweza badilishwa, kama kiongozi anafaa why say no?uhakika wa kupata viongozi wenye maadili na kuendeleza maendeleo upo? pengine yafaa mjadala hapo mbeleni wa why no na why yes? Tusiogope mijadala tuvae ujasiri tuzungumze na kila mtu aheshimiwe kwa maoni ndio matunda ya utashi na uhai wetu

Kwa nature ya serikali hii, iko tayari kuruhusu mijadala? Toka umemjua Magufuli umewahi kumuona kwenye mjadala wowote? Usipendekeze kisichowezekana. Sasa hivi ni mwendo wa shuruti, hayo ya mjadala ni kama kutaka kuhalalisha tu matakwa ya mtu.
 
Hakuna haja ya kuhoji wana ccm kwa sbb hao hao walishaamua na najua mwenyekiti yupo radhi kwa hili angekua hapendi kweli, usingesikia hata mbunge mmoja ananyanyua mdomo wake wangeshaonywa direct kwenye vikao vya chama. Otherwise ni janja janjà tuu. Maneno ya Mange Kimambi yanaenda kutimia katiba itabadilishwa kwenye hiko kipengele ngoja tusubiri si kitambo sana.
 
P.
Mtoa mada ameongea Ukweli na Uzaoendo mtupu.
Tatizo ni hawa wenzetu wa CCM kujifanya WANAMPENDA MAGUFULI KULIKO TANZANIA....!!!Huu ni wendawazimu na wehu!!

Ushauri kwa Rais Magufuli:
RAIS MAGUFULI ATALIVUNJA BUNGE LA JMT TAREHE 19.06.2020 NINAOMBA AFANYE YAFUATAYO;
  1. AMKEMEE SPIKA NDUGAI NA WABUNGE WOTE WANAOTAKA RAIS AONGEZEWE MUDA.
  2. ATANGAZE RASMI MTU YEYOTE ATAKAYE SIKIKA ANATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA ASHTAKIWE KWA UCHOCHEZI.
Kama Magufuli hatafanya Kati ya hayo 2 au yote basi Watanzania wajue na Yeye yuko nyuma na Ni sehemu ya Mpango huo OVU.

Yeye sio tu kuwa ni sehemu ya huo mpango ovu, bali ndio hasa kinara wa hilo, ila kwa kujificha. Na hivi anavyochezea box la kura, ni wazi ataweka watu watakaofanikisha hilo.
 
Wanabodi...

Niwasabahi kwa kuwatakia asubuhi njema na natumai mko fresh kabisa.
Kabla sijaenda mbali Mwalimu wangu wa Sheria pale chuo kikuu aliwahi nifundisha kuhusu "ku-declare interest", naomba ifahamike kwamba mimi ni Mwanachama Hai wa Chama Cha Mapinduzi na Mzalendo nambari moja kwa Taifa hili.

Naomba Wana CCM na Watanzania tuwekane sawa kwenye hili sababu linatuhusu wote, nashangaa sana wasomi , wanazuoni na wanachama wa CCM tunafanya kama hatukumbuki, au tumepoteza kumbukumbu sijui .

Mhe Kessy, mbunge wa Nkasi juzi alinukuliwa na vyombo vya habari Bungeni akisema Rais Magufuli aongezewe muda " Atake Asitake", akanukuliwa pia akisema "Asiachiwe huyu, alazimishwe" akaendelea kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye janga la Corona mataifa yote ya nnje yamemkubali.

Na Mhe Spika Ndugai akajibu, ngoja twende kwenye uchaguzi mkuu, tukirudi Mhe Kessy utaleta hili hili Azimio la Rais kuongezewa muda na naamini wote tutarudi, na lazima tutamuongezea muda."

Kiukweli, Binafsi nimesikitishwa sana na hii kauli ya Mhe Kessy kwa hoja zifuatazo,

Mosi, ikumbukwe tarehe 14 januari 2018, Rais Magufuli alikutana Ikulu na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole na hiki ndiko Rais John Magufuli amesema ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na mjadala ambao unaoendelea wa rais kuongezewa kipindi cha kutumikia kutoka miaka mitano hadi saba.

Amesema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni kufuatia Mhe Juma Nkamia mbunge wa Chemba kuibua Hoja ya Kuongezewa Muda wa Urais toka Mitano mpaka saba.

Pia Rais Magufuli alitaka wananchi KUPUUZA mjadala huo.

Ndugu Humprey Polepole nae wakati anaongea baada ya kutoka Kwenye Mkutano na Rais alisema Magufuli aliwataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi, badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM iliyonadiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kupitia kitabu chake cha "Uongozi Bora ba Hatima ya Nchi yetu", Mwalimu Nyerere alishatoa Angalizo kuhusu kuongeza kipindi cha Urais , namnukuu Mwalimu na anaendelea kuonya tena, "Suala hili lilikwishakuamuliwa zamani, na sasa ni sehemu ya Katiba yetu. Uamuzi huo inafaa uheshimiwe. Rais Mwinyi ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Yeye akisema kuwa vipindi viwili havitoshi, na akataka viwe vitatu; Rais wa pili atasema vipindi vitatu havitoshi, na atataka viwe vinne na kadhalika mpaka tufikie Ngwazi (rais wa milele) wa Tanzania," (uk.10).

Kwa hii kauli ya Mwalimu Nyerere wabunge tunakwama wapi?

Ina mana hatujui tunachokisema?

Je, ni kweli hatuna uhakika wa kurudi kwenye Bunge la 12 kwa hiyo tunatamka chochote huku mwishoni ili tupate "Political Empathy"?

Wana CCM wenzangu, lazima ifike mahali tukubaliane na msemo wetu tunaosema kila siku " TUNASIMAMA NA RAIS MAGUFULI,", basi hata kwa hili analosema "Hafikirii hata siku moja kuongeza siku hata moja baada ya kipindi chake kuisha,", " Rais akasema ANAKWAZWA na hafuraishwi na mjadala wa kuongezwa muhula wa uongozi"

Rais Magufuli amenukuliwa mara mbili tofauti akiwajibu wale wote wanaomlazimisha aongeze muda, na Rais wetu hajazunguka kimaneno, kasema plain black and white "SITOONGEZA MUDA HATA WA SIKU MOJA BAADA YA KIPINDI CHANGU KUISHA", nakumbuka hii ilikua disemba 2019 alikua anatoa hotuba mahali.

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Dr Bashiru nae alipokua pale Chemba akimtumbua Katibu wa CCM mkoani Chemba kwa kukosa Kujiongeza kuiva na viongozi wenzake alilisemea hili jambo, akasema " Rais Magufuli atamaliza miaka yake kumi, hiyo tutampa ridhaa badala ya Hapo atafata utaratibu wetu wa kikatiba wa kuachiana vijiti"...

Hivi wabunge wanataka KUTUAMINISHA wana nguvu zaidi ya wananchi waliowachagua?

Hivi Spika wa bunge Ndugu Ndugai anaposema BUNGE TUTAMUONGEZEA muda anaelewa kweli?

Hivi Spika hakumbuki TUME YA JAJI NYALALI(NYALALI'S COMISSION), miaka ya 1998 9 na ile kazi ya kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba?

Kwamba lazima wanachi wafanye kitu tunaita Referendum .,

Kukawa kuna kitu kinapita mtaani kwa jina la "WHITE PAPER"? Chenye lengo la kutaka kujua maoni ya watanzania kuhusu jambo husika la kurekebisha kwenye katiba yetu.

Kwa nini Spika useme " TUTAMUONGEZEA MUDA" maana yake unasahau sisi wananchi wa kawaida na nguvu yetu kwenye maamuzi.

Hivi Mhe Kessy kweli anataka tuamini hajasikia maneno ya Katibu Mkuu wetu Dr Bashiru kuhusu mjadala wa ukomo wa Urais.?, Katibu Mkuu alitamka ameufunga Rasmi disemba 2019 au Mhe Kessy ana nguvu zaidi ya Dr Bashiru??, kitu akishasema Katibu Mkuu wa Chama wewe mwanachama wa kawaida una comply nacho..Hauna haja ya kuropoka tena maana Msimamo wa Katibu Mkuu ni msimamo wa Chama.

Waziri Kabudi nae alishatolea ufafanuzi hili jambo wakati akiwa Katiba na Sheria , akasema vipindi vya Urais ni VIWILI tu vyenye miaka Kumi Kumi ndanu yake.

Simlaumu Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Mizengo Pinda siku ile aliposema "Anatamani Rais Magufuli aongezewe muda wa Urais"..

Mhe Pinda alikua anatoa maoni yake kama mtanzania wa kawaida, kama mimi na wewe, lakini baada ya Rais Magufuli kutoa msimamo wake kuhusu hilo ombi , binafsi sijamsikia Tena ndugu Pinda anakuja kwenye media na kuanza kumbembeleza Rais.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu kutoa maoni, hata wakati Rais Kikwete anamalizia uongozi wake 2009 kulikua na watu wakimtaka Rais Mstaafu Kikwete aongeze muda wa kukaa kwenye Urais..

Waziri wa katiba na sheria mhe Chikawe wakati huo akatoa msimamo kwamba Rais Mstaafu Kikwete hatoongeza tena muda wa Urais.

Narudia tena, Ndugu Juma Nkamia alikua amepeleka hoja yake binafsi ya kuongeza Kipindi cha Urais toka miaka mitano mpaka saba lakini baadae aliitoa hii hoja yake akasema " Ameshauriwa na viongozi wake wa juu wa Chama cha Mapunduzi aitoe na asiendelee na hoja yake japo Nkamia aliileta hoja yake mara mbili lakini alivyoambiwa aitoe, ALIITOA", na hii inaitwa UTII kwa viongozi wako wa CHAMA.

Pia Mhe Mizengo Pinda hakuendelea na hoja yake mara baada ya msimamo wa Rais Magufuli, kwa nini Mhe Kessy anakomaa?, unaweza kuona "countance" (mwonekano) wa Mhe kessy pale Spika Ndugai alipomwambia "Utarudi kwenye Bunge lijalo la 12 na utakua ni wewe mletaji wa Azimio hili".

Ukiisoma Body Language ya Mhe Kessy unaona kabisa anafurahi kusikia atarudi kwenye Bunge lijalo!

Anafurahi kuambiwa atakua mletaji hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Kuongeza ukomo wa Kipindi cha Urais!.

Kifupi mhe Kessy anataka kurudi bungeni, which is okay lakini rudi bungeni with your own expense!, sio unarudi bungeni with expense' of the Nation.

Leo kila mbunge atake Katiba ibadilishwe ili apate debe/upendeleo wa kurudi bungeni toka kwenye Kamati Kuu ya CCM si kila siku tutakua tunabadilisha katiba yetu .

Nkamia alikua anataka ku-copy paste Katiba ya Rwanda ambayo toka 1994 ilikua inasema Kipindi (tenure) ya uongozi wa Urais ni miaka saba saba , lakini Rwanda wamefanya mabadiliko kwenye Katiba yao na kuanzia Mwaka 2024 Rwanda wanarudi kwenye tenure ya miaka mitano mitano, , Rais akae miaka kumi tu madarakani ampishe Mwenzie.

Kifupi Rwanda wanatamani kuwa kama sisi lakini Sisi ndo kwanza Tunataka Rais Aongezewe miaka 10 zaidi kutoka 2025 yaani Rais Magufuli atumikie mpaka 2035.

Mi nampenda sana Rais wangu kwa kazi alizofanya na anazoendelea kufanya.

Naipenda spirit yake ya kujitegemea na "will power" yake kwenye kufanya mambo na maamuzi kama Taifa hakuna sehemu nam-doubt Rais Magufuli.

Ni will-power yake na roho yake ya kizalendo kwa Taifa hili imetufikisha hapa tulipo, maofisi ya serikali yana nidhamu, wanyonge wanasikilizwa na kupewa HAKI.

Rais Magufuli amefanya Maamuzi ya kipekee sana kwenye kushughulikia suala la Corona, ametujengea Roho ya kipekee kwenye Kipindi hiki Taifa limepitia kwenye Huu ugonjwa.

Rais Magufuli kawajibisha wakuu wa mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za serikali pale Rais anapobaini mambo hayaendi!...unakumbuka kuvunjika kwa Daraja pale Morogoro?, unakumbuka Waziri Kamwele alivyochanwa Live kwa kutomuajibisha Meneja wa TANROADS wa mkoa?

Unakumbuka Rais alivyowachana Magereza na TBA pale Ukonga kwenye mradi wa nyumba za jeshi la magereza?

Na akawaambia live atawaletea Kamishina wa MAGEREZA toka JWTZ?

Unakumbuka JKT walivyoendeleza ujenzi wa zile Nyumba na Ukaisha?

Hii ni mifano michache ya Rais Magufuli, bado uthubutu wake wa Kufufua Mashirika ya UMMA kama ATCL .

Sitozungumzia ujenzi wa madaraja, barabara, vituo vya Afya kila kata, Elimu Bure, Mikopo ya Elimu ya Juu n.k maana hivyo kila mtu anavizungumzia.

Binafsi naungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Dr Bashiru , Naungana na Rais Magufuli na Msimamo wa Chama kwa Pamoja Kumruhusu Rais Magufuli apate kipindi cha Pili cha Uongozi kwa miaka mingine mitano mpaka 2025.

Vivaa Magufuli....

Mzee Pius Msekwa alikua mmoja wa wazee walioshughulikia mabadiliko anuwai' yaliyokua yanafanyika kwenye Katiba ya Tanzania toka ile ya 1921 .

Anajua tulikotoka na mabadiliko yote tuliyofanya zaidi ya mabadiliko 12 na alisema wazi kabisa "Toka enzi za Mwalimu tulishazungumzia kuhusu kuongeza muda wa Urais".

Wana CCM na hasa vijana wenzangu wa UVCCM tusimkwaze Mhe mwenyekiti wetu Dr Magufuli, kashasema HAPENDEZWI, ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na hizi kauli zetu huku kwenye mitandao tunapiga kelele za kuongeza muda wa Urais.

Rais Magufuli nae ana maisha yake ya kifamilia, tumuache apumzike na tumshukuru kwa Mchango wake mkubwa kwenye Taifa hili la Tanzania na alishasema Mara Nyingi " Urais ni KAZI NGUMU".

Alishasema analala na mafaili pale IKULU wakati mwingine tafadhali tuheshimu maamuzi yake.

Tuachane na wanasiasa walio tayari kusema lolote mradi mradi tu warudi bungeni hata ikibidi kurudi "in expense" (kwa gharama) ya kubadilisha katiba....

Laiti Rais mstaafu Jakaya Kikwete angesema aongeze muda basi leo hii tusingempata Rais Magufuli, haijalishi kapatikanaje lakini kapatikana na kwa Miaka hii mitano kalinyanyua hili Taifa akiwa na Timu yake aliyoichagua na Kuiamini.

Sasa akisimama Mbunge kama Mhe Kessy akasema "Haoni mtu mwingine wa kutuvusha baada ya Magufuli", mi namshangaa Mhe kessy..sijui alikua anawaza nini.

Nafunga kwa Maneno ya Rais Magufuli anasema " MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU"...

Na ameshasema zaidi ya mara moja, na viongozi wa Chama na serikali wameshaongea kuhusu kuongeza muda basi TUSIMKWAZE mpendwa wetu Rais Magufuli.

Tutashinda Uchaguzi huu Mkuu wa oktoba na Chaguzi zingine Miaka mingine sababu tunaaminika na wananchi.

Ndugu Humprey Polepole aliulizwa siku swali kwenye redio unadhani siku CCM ikiondoka madarakani tatizo litakua nini?

Na napenda jibu alilotoa, "Kwa sasa CCM haitotoka madarakani kwa mabadiliko haya tuliyofanya", Lakini huko baadae CCM ikianza kudharau wananchi basi itaanguka na kuondoka madarakani"

Tueshimu Msimamo wa Rais Magufuli kuhusu kutokuongeza muda wa Urais na tumshukuru Kwanza yeye na serikali yake kwa kazi nzuri waliyofanya ndani ya miaka mitano na tusimame nae kwenye hii miaka mingine mitano mpaka 2025.

Nimeona Niliseme hili wazi na tafadhali moderators msiunganishe huu uzi na nyuzi zingine maana haufanani na nyuzi zingine maana hamkawii kunikwaza asubuhi

"MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA TANO".

NB: Kwa maoni au ushauri usisite kumuandikia muandishi kwenye barua pepe : godjohn8@gmail.com
AISEE ; HILI POVU LOTE LA NINI? KILA MTANZANIA ANAYO HAKI YA KUTOA MAONI YAKE. WATANZANIA TUKIAMUA INAWEZEKANA MAANA MBONA KILA MTU ANAYAONA MAZURI YANAYOFANYIKA. TATIZO LENU MNAFIKILIA HUYU MH. AKIONGEZEWA MUDA WA UONGOZI, ILE NDOTO YENU YA KUTUPIGA KWA MARA NYINGINE BUSINESS AS USUAL HAMTAPATA KITU. HAPO NAKUONA JINSI UNAVYOFANYA MAZOEZI YA MUHULA WAKE UKIISHA UANZE KUANZISHA MAKAMPUNI YA HEWA YA MIFUKONI. SASA NAKWAMBIA HIYO KITU SAHAU, HAPA TUNAKWENDA NA MAGUFULI AWAMU HADI NNE, LIWE JUA IWE MVUA SISI TUNASEMA MAGUFULI ATOSHA KWA AWAMU NNE MFULULIZO
 
Hongera kwa maoni na mtazamo wako kwa mujibu wa katiba, sio vibaya kwa wanaoshauri hilo pengine ubaya ni kupoka mamlaka ya wananchi hasa kwa namna ya uzungumzaji wa wabunge, hoja ya namna hii ikipelekwa bungeni si itapata fursa ya referendum?wananchi watapewa fursa ya kukubali au kukataa, uhuru wa maoni , mawazo, fikra ni pamoja na tusiyoyapenda na tuyapendayayo, binafsi naamini uongozi ni kujitolea na ni uzalendo, Mbona Nyerere alikaa miaka 23, Katiba sio biblia kwa nia na utashi jumuishi inaweza badilishwa, kama kiongozi anafaa why say no?uhakika wa kupata viongozi wenye maadili na kuendeleza maendeleo upo? pengine yafaa mjadala hapo mbeleni wa why no na why yes? Tusiogope mijadala tuvae ujasiri tuzungumze na kila mtu aheshimiwe kwa maoni ndio matunda ya utashi na uhai wetu
Uko sahihi sana Mkuu, kwa mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977 na mabadiliko yake inasema na nainukuu..

____
98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha
masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na
aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya
sheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanza
kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura
za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili
ya Wabunge wote;
(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti

Mwisho wa kunukuu.

Kama Mhe Kessy akirudi bungeni, atapeleka hilo Azimio lake Bungeni...Bunge litajadili na kupiga kura kama ilivyoelekezwa na Katiba baadae kura zikitosha kama ilivyoelekezwa kwenye aya hapo basi Bunge litaruhusiwa kutunga sheria ya kubadilisha masharti ya katiba (likiwemo sharti la ukomo wa urais )

Wakimaliza wataleta huku chini kwa wananchi kwa ajili ya referendum.

Hatuogopi kuingia kwenye majadiliano kuhusu Ukomo wa Urais, kuongeza au kupunguza bali Tunaetaka Kumuongezea muda ameshasema mara nyingi hataki .

Kwa nini tunafosi?

Kama tunaetaka abaki hataki, basi tuache hizi habari.....

Kama mbeleni huko tukiona kama Taifa tuna haja ya kufanya extension ya muda wa Urais basi tukae tuzungumze.

Lakini kwa Rais Magufuli kashatuambia hataki na tunamkwaza.

Then we should stop...kama ambavyo Katibu Mkuu alisema "Amefunga" huu mjadala kwa Rais Magufuli.
 
Back
Top Bottom