Piga ua inabidi tu'develop' critical/intelligent thinking

Piga ua inabidi tu'develop' critical/intelligent thinking

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Posts
5,906
Reaction score
4,128
Ndugu wana jamiiforums. kichwa cha habari kinajieleza vizuri. Tuna shida katika kujenga hoja, ila tuko vizuri katika kutoa maoni. Na hii ndiyo concern yangu katika post hii. Watu wengine, kwa mfano, wakitoa maoni yao kuhusu jambo fulani, wanataka uwaamini kwa asilimia 100 kwa hilo jambo wanalokwambia. Kwa mfano

Ukiuliza wana uhakika gani na jambo hilo, most likely watauliza: "kwa hiyo huniamini?" Lakini wewe ulitaka tu ku'verify' akupe vyanzo vya taarifa yake ili na wewe uweze kutafuta ukweli kuhusu jambo uliloambiwa.

Lakini matokeo yake, unakuta unaingia mgogoro na mtu wako wa karibu kwa kudhani humwamini, na unaanza kusikia habari ofisini au sehemu nyingine kwamba "huyo ni mtu mkubwa hukupaswa kumuuliza a'verify' taarifa anazokupa." By the way, mimi kwa mfumo wangu wa elimu nilioupitia siku za huko nyuma, nimeweza kukubali kanuni ya Rene Descartes. Alikuwa French Mathematician, scientist and philosopher.

Hivyo, the likelihood ni kwamba mtu akisema jambo fulani mbele yangu, lazima niulize "how do you know?" Lengo sitaki kulishwa matangopori. Je, na wewe ulishawahi kukabiliana na situation kama yangu, na je wewe huwa unafanyaje Concretely, mtu hawezi kuja kwangu na kuniambia "mkeo anachepuka" nikamwamini.

Ingawa inaweza kunisaidia kuchunguza kwanza kabla ya kuamini hivyo kwa sababu kuna mambo mengi nilishaamini ambayo si kweli, na kuna baadhi sikuamini na yakawa kweli. Kwa hiyo, ndiyo maana kwangu verification ni jambo muhimu sana.
 
"Thinking is difficult that's why many people judge" Carl Jung

Watu wengi hatupendi kushugulisha akili zetu. Nashangaaga sana humu mtu analeta hoja watu baadala ya kujibu hoja wanatukana, mtu akipingwa kwa hoja yake anaona kana kwamba imetendeka dhambi isiyosameheka.... (Mambo yanayoshangaza kweli).

Na tatizo la mtu kuamini kwamba kile anachokijua au kukiamini yeye ni bora zaidi kuliko cha wengine ni ujinga pia. Mtazamo wako ni moja kati ya mitazamo ya watu wengine (ila kuna watu wengi wanajiona wao ndio wao wengine kama takataka).
 
mtu hawezi kuja kwangu na kuniambia "mkeo anachepuka" nikamwamini.
Naunga mkono hoja, hutakiwi kuamini kila kitu unachoambiwa, ila kuna vingine, hata ukiambiwa, far the sake of piece and tranquility usiviamini!.
Mimi ni Mkatoliki wale tulioendelea endelea kama Sir George Kahama, nikiwa DC kwenye party ya ubalozi wa Tanzania, kuna mbongo akanifuata na kuniambia wife wako hapa anachepuka na mtu anyechepuka nae tuko naye hapa kwenye hii party, nikuonyeshe?.

Kwanza nilimuuliza ananiambia hivyo ili iweje?, nilimshukuru kwa taarifa, nikamwambia asante sihitaji kumjua wala kuyajua hayo!.

Akatoka na kuwaambia watu kuwa mimi nimelogwa vibaya!.
P
 
Tusiwadharau sana watu aisee hawa Watanzania wenzetu.

Watu wakiamua kuhoji na kureason mambo magumu hapa kuna baadhi au kundi au Taasisi zinachukia kwa kuwa mfumo au tabia zetu hazipendi kusikia mambo magumu na yanajulikana.

Watu wanajua kama hujui ni wewe.
 
Kwani dini ipo Tanzania pekee mkuu? Mbona nchi nyingine kwenye hii mada ya Israel na Iran wanachangia points bila kujali imani zao za kidini?. Hata Papa Leo huwa anawachana vizuri viongozi wakristo wakizingua

Mtoa mada kaongelea critical thinking ya wanajf sio wanadunia wote, so nimechangia kwa muktadha huo sio nje ya context yake
 
Dercartes doubted even for his own existence! "Cogito ego sum" I think therefore I'm " let us use critical thinking about Christianity! Is resurrection a historical event? Do you believe in order to understand or you understand in order to believe? But for Africans if you doubt about foreign religion, you will be regarded as a fool.
 
Back
Top Bottom