Even MOre
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 327
- 541
Wana bodi tupate tafakari ya pamoja na pengine kujenga au kuongeza uelewa juu ya dhana na mantiki ambayo inaweza kuwa ni nadhari ambayo wengi wetu hatuijui vizuri juu ya uwezo au nguvu ya kutenda (Kujua, Kuamuru jambo nk) ya viumbe MAJINI ambao hawaonekani uwepo wao kwa macho yetu ya kawaida ya kibinadamu.
Pengine mimi na wewe tumewahi kusikia juu ya uwezo huo ambao viumbe hawa Majini wanao kulingana na jamii zao na kazi zao. Sasa mada yangu hasa ni kuhusu jamii za Majini yenye ujuzi wa utabibu ambayo kwa mukhtadha niliofanikiwa kupitia pitia katika makala na kuongea na watu wenye uelewa kidogo na elimu ya Majini wanadai jamii ya Majini ya utabibu ndiyo yenye maarifa zaidi na ujuzi mwingi wa kujua mambo mengi ya dunia yetu tunaishi wanadamu leo kwani kwani kwa maelezo wao wanaishi miaka mingi sana, hivyo wanajua mambo mengi yaliyopita na hata yajayo. (Kama kuna masahihisho unaruhusiwa)
Sasa kupitia nadharia hii kuna maswali ambayo binafsi nimekuwa nikishindwa kuelewa juu ya uwezo unatajwa wa viumbe majini ukilinganisha na baadhi ya matukio ambayo yanatokea na kujikuta mtu mwenye hao viumbe anakosa msaa licha ya kuwa na hao viumbe. Ili tuweke sawa ni vema tupate mfano ambao wengi wataelewa vizuri.
Mwaka jana wakati wa Maandamano ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, kulikuwa na patashika za hapa na pale zilizosababisha baadhi ya waandamanaji na wasio kwenye maandamano kupigwa risasi, hapa ikatokea mtu mmoja maarufu ambaye ni Sheikh.......Majini kuuwawa ikidaiwa alikuwa akitokea Kuswali (Inalillah wa Inalillah). Kwa mujibu wa maelezo yake enzi za uhai wake alikuwa akisema yeye anamiliki hawa viumbe MAJINI wenye uwezo mkubwa maelfu kwa maelefu.
Mkanganyiko wangu na maswali juu ya hawa viumbe wenye uwezo wa kujua yaliyopita, yanayo na kuamuru jambo lolote na likatokea, katika tukio hilo:-
1. Je, majini wa ndg huyu hawakuweza kutambua hatari inayokuja mbele ya mmiliki wao (Kiti 😃) punde akitoka Masjid na wakaweza mzuia asitoke kabisa kwa kutumia uwezo wao?
2. Ikiwa hiyo Na. 1 👆🏻ilikuwa too late, hawakuwa na uwezo wa kumkinga na madhara ya risasi kwa kumpoteza katika mazingira yasioonekana kwa wauaji?
3. Ikiwa Na. 2 👆🏻 ilikuwa ngumu, majini kwa hadithi tunazopewa wanauwezo wa kuingia katika roho au mwili wa kiumbe hai chochote na kufanya madhara au kukiamrisha kutenda watakavyo wao, je hapa napo baada ya kuona wameshindwa kumuokoa (walinzi) mpendwa wao, Kiti wao na kuuwawa mbele yao hawakuwa na hasira hata za kuwaingia wauaji ili sasa wabadilikiane waweze kuuwana wao kwa wao?
4. Ama hakunaga upendo wa dhati kati ya MAJINI na WANADAMU na hayo yote juu wanaweza kufanya kama tunavyosikia katika nadharia na story nyingi ila walijua, waliona na hawakutaka kufanya lolote kwakuwa kuna mambo yanayowabana wao kumsaidia mwanadamu katika mambo magumu kama hayo?
Nawasilisha