Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 70,945
- 93,884
[h=2][/h]
Wapo wanaodhani tunatangaza utalii huku wengine wakidhani tunahonga wanyama wetu kwa jamaa hawa. Sijui jamaa atapewa kanzu au msuli? Maana jezi keshapewa sana. Kesho msishangae kusikia ndege nyingine ikisafirisha wanyama hai na hakuna atakayeguswa. Wengi walidhani angalau Kikwete angeulizia ni kwanini Falme za Kiarabu zinatuibia wanyama. Je anaogopa kuambiwa kuwa tuliwauzia kwa ufisadi wetu? Nini tafsiri ya picha hii?
Mkuu nadhani Falme za Kiarabu(UAE) na Oman ni mamlaka mbili tofauti ingawa zote zapatikana middle east.
Kama sikosei hao Oman ndio waliotukwapulia twiga...najua kwa nchi zenye msimamo wa dhati tungekuwa tushavunja uhusiano wa kidiplomasia na hao watu kwa kitendo hicho, lakini kuonesha tulivyo mbumbumbu, Rais wetu ndiye anakuwa mstari wa mbele kwenda kuwakenulia meno na kutoa tunu zenye maslahi na jambo lile lile lililozua utata.
Shame on you JK....upo kama msukule vile!!