Kwanini unauliza hivyo mkuu?BTW
Huyu Qabus hana mke.
Halafu mbona kama huyu Sultani ana Jambia??
![]()
Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman.
Mbona huyu Sultan ana Sime? je kikwete ana nini hapo? hiyo sime (jambia) nishakumbuka picha za biashara ya watumwa, toba
Ikumbukwe kwanza kuwa kuna historical ties kati ya Tanzania na Oman kwa muda mrefu. Pamoja na halo ikumbukwe mambo mawili muhimu:
a. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 Rais Kikwete alipokea karibu dola milioni 2 kwa ajili ya kampeni toka Oman
b. Yule mmiliki wa Dowans aliyekuja wakati ule ni mtu wa karibu sana wa Qaboos; kwa wanaokumbuka yule bwana ana asili ya Zanzibar.
Jibu hoja kwanza hivi:Je una uhakika na hayo?
Mbona usemi Dr Padre Slaa alipokea kiasi gani kutoka Vatican?
Lakin ukitazama na kusoma Historia HAKUNA HATA KIDOGO HISTORICAL TIES baina ya Oman na Tanzania. Bali kuna mengi ya kihistoria baina ya Zanzibar na Oman kama ilivyokuwa Tanganyika na Uingereza
Jibu hoja kwanza hivi:
(a)Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 Rais Kikwete alipokea karibu dola milioni 2 kwa ajili ya kampeni toka Oman
(b)Yule mmiliki wa Dowans aliyekuja wakati ule ni mtu wa karibu sana wa Qaboos; kwa wanaokumbuka yule bwana ana asili ya Zanzibar
Wanajamvi tunataka useme unafahamu au hapana? hizi habari za Slaa na Upadri wake hazijaulizwa, ila ni kweli kabisa (hata kamuulize kikwete mwenyewe) alipokea kiasi cha hela toka Oman na alifanya ziara huko akiwa kama Waziri wa Mambo ya nje, kwa kifupi jibu hoja za mwanakijiji, asante hayo mengine tishia toto
Hoja za kitoto kabisa hata ataekujibu pia mtoto'unaleta habari za kufikirika kisa mmiliki wa dowans ni muoman basi anauhusiano na qaboos,
Kutwa mnawasema waarab kama wao ni watu ambao hawana elimu au washamba sana kisa wanavaa kanzu, kwa taarifa yako hao waarab na ushamba wao na makanzu yao hakuna nchi hata 1 ya kiarabu ambayo sisi tz tunaifikia kwa maendeleo au kwa chochote pamoja na kuvaa suti zetu' acheni chuki zisizo na msingi
PICHA YA KWANZA; kwenye begi kunani??????