PICHA: Yanayojiri Kigoma katika mapokezi ya Zitto

PICHA: Yanayojiri Kigoma katika mapokezi ya Zitto

Status
Not open for further replies.
kamanda kamua ili watu wakujue kama we ni mwanasiasa bora na sio usaliti wanaokuhusisha. Cha kushangaza wakina mama ndo wengi, kwanini zitto anapendwa hivi?
 
Kua uyaone.. .yaani leo ccm wanaungana kumtetea Zit to?????!!!!haya kila la heri ila mkishindwa kubalini matokeo na mrudi kijijini maana hatokuwepo wa kuwalipa tena kwa ujinga huu

n kamanda wao wa.UVCCM ndio.mratibu huko Kigoma. Mwampamba
 
Sasa mbona hamna polisi?Au ina maana kwamba kuna uhakika wa usalama?
 
cha msingi hapa ni kutokufanya jambo kwa ajili ya kumridhisha mtu,ni kufanya jambo kwa ajili ya matakwa yako na jamii kwa ujumla na si kufanya jambo kwa ajili ya kikundi cha watu wachache.
zitto acheni aende kigoma,anakwenda kama mbunge na hakuna mwenye uwezi wa kuzuia mbunge kuongea na wapiga kura wake,anaelewa kuwa anamashitaka 11,lakini hii haizui yeye kama mbunge kutokujibu hoja zilizosemwa awali ambazo ni za upotoshaji juu yake,atazisema tu maana zilisemwa ktk jimbo lake na yeye anakwenda kuzijibu ktk jimbo lake.maana haiwezekani ukasemee ktk jimbo lake na then umwambie eti unamashitaka 11 na utabidi uyasemehe ktk kikao,mbona wewe umesemea sababu zilizomvua uongozi ktk jimbo lake? mwacheni tu mbunge aende kuongea na wapiga kura wake na kuweka sawa yale yote yanayoleta sintofahamu juu yake,maana wapiga kura wake wanahitaji kuelewa

Mtorela!

Kwanza pole maana najua ulikuwa huamini kuwa swahiba wako angeweza kuchukuliwa hatua hasa kupitia maandiko yako kule mtaa wa pili.

Pili, acha kufanya propaganda za kijinga kupitia maandiko yako! Swahiba wako hajazuiwa kukutana na wapiga kura wake na wala hakuna siku baada ya yeye kuvuliwa nyadhifa zake chadema waliyotamka kuwa haruhusiwi kwenda jimboni kuongea na wapiga kura wake. kama una ushahidi wa yeye kuzuia kwenda kigoma uweke hapa. Acha kupotosha!

Yeye akiamua anaweza kufanya mikutano mpaka Lumumba akisubiria stahili yake inayomfaa kwa namna kamati kuu itakavyo amua.

Usema kuwa tuhuma 11 zilisemwa kwenye jimbo lake?! zilisemwa na nani na lini?! tumia usomi wako na exposure uliyoipata kwa kuongea kwa facts usiwe unazomoka tu kama mtu ambaye hajui mlango wa darasa. Hayo mashtaka unayosema yasemwa jimboni kwake niyapi?!

Pole sana, ungekuwa unampenda sana rafiki unge mshauri asi betray coarse. Sikio likesha kufa halisikii tena dawa.
 
Zitto bado ni mwanachadema nini knawafurahisha ccm kwa mwanachadema kupokelewa vizuri jimboni wake?
Waambie vile vile hata wanaCHADEMA wanaokasilishwa kwa mwanaCHADEMA kupokelewa vizuri jimboni kwake.

Hata mimi ninashindwa kuelewa hii LOGIC.
 
​

Pigo jingine kwa Zitto na team yake.....mkakati wao wavuja.....
Katika hali ya kutafuta jinsi ya kuweza ama kuibomoa ama kutaka kuonyesha kuwa Ana nguvu ndani ya Chadema na haswa kwenye baraza kuu , mambo yafuatayo yameandaliwa na team Zitto kwa kuratibiwa kwa ukatibu sana na watu wa idara kama ifuatavyo;
1. Ni kuwa leo Kigoma , aliyopewa jukumu la kuratibu ziara nzima ni Mwanamama Maria Sarungi, huyu bila Zitto kujua amejikuta anapandikiziwa huyu mama na Chadema makao makuu na amejikuta kuwa kwenye wakati mgumu kwani mipango wanavyofanya yote ina Julikana na mpaka sasa ni kuwa Makao makuu ya Chadema wanafuatilia kila jambo jinsi linavyokwenda. Maria alipopewa jukumu la kuandika hotuba ya Zitto , aliwasiliana na kiongozi mmoja wa makao makuu ya Chadema , na kiongozi huyo ndio aliandika draft ya kwanza na kumpa Maria ili aweze kuiwasilisha kwa Zitto, na ndio itatolewa leo huko Kigoma.
2. Maria na wenzake wameenda mbali kwa kuandaa kinachokatwa Mkakati wa Baraza kuu kwa kuwa na bajeti na kuandaa petition kwa ajili ya kusainiwa na baadhi ya wajumbe wa Baraza kuu kwa hoja kuwa ni ili kushiriki za kuitwa kwa kikao cha Baraza Kuu, waliokuwa katika utekelezaji wakajikuta kwenye wakati mgumu sana kutoka kwa wajumbe , na ndipo walipoamua kuwadanganya wajumbe kuwa fomu hizo za petition zimeandaliwa na Chadema makao makuu, na hivyo zina Baraka zote kuwa ni jambo halali. Kwa mfano leo viongozi wa kusini wameitwa Masasi na aliyepewa jukumu la kuratibu jambo hilo kwa mujibu wa Maria Sarungi ni Chitanda Ali , ila alipoona kuwa hawezi kukubalika kwa wajumbe waliamua kumpa jukumu la mialiko katibu wa Nachingwea ,na kikao cha Masasi kitafanyika leo jumamosi.


3. Zitto, kwa kutokujua amejikuta akifanya mipango yake ambayo inaratibiwa na Makao makuu ya Chadema kwa mkono wanyama , ndio maana hata mpango wa kujaribu kuwafukuza viongozi wa Chadema walioshiriki MAPOKEZI ya Dr.Slaa huko Kigoma , unaelekea kukwama baada ya Makao makuu kuingilia kati, aliyepewa jukumu hilo la kuratibu Kigoma ni Tabibu Alex , japo huwa anapenda kujita Dr.Alex , na ndio hata leo amepewa fomu za kusaini petition kwenye mkutano wa hadhara, na walivyo panga ni kuwa leo hiyo petition haijawekwa utangulizi ili wajumbe na wananchi was iweze kushtuka na ivyo ndivyo itakayokuwa.


4. Bajeti ya mpango huu ni kubwa kwani kwa awamu ya kwanza itahusisha mikoa ya Mwanza, Tabora,Lindi, Mtwara, Tanga,Katavi ambako Mzee Arfi ndio amepewa jukumu, Mwanza jukumu kapewa Wilson Mushumbusi , Chagulani Adams, Tabora jukumu kapewa kijana mmoja kutoka Kaliua huyu sio mwanachama wa Chadema hivyo jina kampuni, Tanga jukumu kapewa Khalid Rashid.......


5. Timu ya Zitto, imejikuta ikimficha Msafiri Mtemelwa mambo mengi kwani wanafikiri yeye kwa kushirikiana na Mwamnyange ndio wanavujisha siri, pasipokujua kuwa wala sio hao ni watu wa jikoni ndio ambao ni majenti wa Makao makuu,


6. Pigo kubwa zaidi ni baada ya Nchimbi uteuzi wake kufutwa na Rais jana , kwani alikuwa ameshaline up baadhi ya ama ocd kwenye wilaya kuhakikisha kuwa mikutano ya hadhara inalindwa na kupewa ulinzi mkali wa kuonyesha kuwa kuna kitu kikubwa......pigo hili limewaadhiri pia media house ya Msacky kwani mpango ulikuwa kamambe.......


mwisho, Moods, ni najua kuwa mmoja wenu ameshirikishwa kwenye mpango huu na tayari amekuwa akitoa taarifa za watu ambao wamekuwa wakiandika na hata saa nyingine kuondoa post za baadhi ya watu , naomba hii ibaki hapa na kama kuna mtu atabisha nitaweka ushahidi hapa hatua kwa hatua.


stay tuned........hotuba itakayotolewa na Zitto nitaiweka hapa baadae , nusu saa kabla ya hotuba yenyewe kutolewa.

Sasa tatizo nini ziara yake kusimamiwa na wana CHADEMA ukizingatia na yeye ni mwana CHADEMA
 
Akitoka Kigoma aende Arusha,Mbeya,Ifakara,Iringa na Mwanza kukagua uhai wa chama
 
Wapelekee walevi wenzio wagongo matapishi yako haya
Wakati unaona kuwa ni ulevi, wenzako wameshachanganyikiwa na wanalaumiana kutokana na Maria kuwahujumu, na ndio wametambua kumbe alikuwa na Kisasi na Dr.Kitila baada ya 2010 kumwondoa kwa aibu kwenye kamati ya kitaifa ya kampeni kuwa alikuwa Mamluki.....kaamua kuwakomesha na kuvuruga Dili Lao hili....
 
Sasa tatizo nini ziara yake kusimamiwa na wana CHADEMA ukizingatia na yeye ni mwana CHADEMA
Mkakati umevujishwa makusudi ili kuukwamisha , nimeanzisha thread ili kumsaidia moods wanaunganisha ........
 
Wakati unaona kuwa ni ulevi, wenzako wameshachanganyikiwa na wanalaumiana kutokana na Maria kuwahujumu, na ndio wametambua kumbe alikuwa na Kisasi na Dr.Kitila baada ya 2010 kumwondoa kwa aibu kwenye kamati ya kitaifa ya kampeni kuwa alikuwa Mamluki.....kaamua kuwakomesha na kuvuruga Dili Lao hili....

asante kamanda , cdm ni taasisi imara sana .
 
kamanda kamua ili watu wakujue kama we ni mwanasiasa bora na sio usaliti wanaokuhusisha. Cha kushangaza wakina mama ndo wengi, kwanini zitto anapendwa hivi?

kwani JK naye si anapendwa sana na wakina mama au?
 
Mama yangu, duuh Zitto kamfunika Slaa, naamini hakuna wa kumtingisha Zitto chadema, dkt slaa hakufikia hata nusu ya hao watu.
 
aliyevaa gwanda la kiccm huyo ana mantiki yoyote cdm bora tumuengue kwani anatuletea nuksi tu hapa
 
Waliokuwa wanakutana leo Masasi wanalaumiana pia baada ya kujulishwa kuwa mkakati umevuja , Maria Kikaangoni , yuko Kigoma ......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom