Stephano Mwandiga
Member
- Dec 14, 2013
- 78
- 24
hali hii ni kawaida kabisa rakini inatakiwa zitto aitumie nafasi hii kujishusha mana akizidi kujifanya anapandisha mapembe hali yake kisiasa itakuwa mbaya zaidi au kupotea kabisa ktk siasa za tz, namshauri azingatie yafuatayo
1/ Asichanganyikiwe na kulewa sifa ya watu kumpokea kwa mabango, mana yeye ni mbunge na mtu maarufu na watu wa kigoma bado wako kwenye mhemuko wa tuhuma alizo nazo ndani ya CHADEMA
2/Sio wote wanaompokea ni wake, ni lazima zitto ajue kunawatu wameenda kumpima kama anastahili kusamehewa na chama au chama kimpige msumali wa moto kichwani, na wengine ni wana ccm ambao wanataka alewe sifa kuwa anakubalika na kupandisha mapembe zaidi then mwisho wamtose
3/Busara imtangulie mbele kuliko jeuri, ajaribu kuwa mtu wa kujishusha mana sio mbowe wala slaa wanao muangalia ktk mkutano wake wa leo bali ni watanzania wapenda maendeleo na uhuru wa kweli ambao wote kama sio wengi imani yao iko kwa CHADEMA Ko watu hawa hawako tayari kumshabikia yeye na kuacha taasisi ife
4/ Uchaguzi wa maneno na watu atakaoshirikiana nao katika mkutano huo,
KI MSINGI AJUE CHADEMA BADO IMEMUWEKA KWENYE MATAZAMIO NA NI MTUHUMIWA WA MAKOSA 11 KWA KATIBA YA CHADEMA
TAASISI KWANZA USHABIKI KWA MTU UWE KITU CHA MWISHO HIKI NDICHO WANAKIGOMA WANATAKIWA KUKIJUA