Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,038
- 9,353
Je Wananchi hawa wanaomfuata Zitto na Kumshangilia nao pia ni Wasaliti?
Sidhani kama kuna mtu yeyote amemzuia kwenda jimboni kwake, ila tunachojaribu kushauri ni busara ipi inayomwongoza ukikumbuka bado yeye ni mtuhumiwa anayeangaliwa kwa jicho la karibu.Hamtaki mtu aende kwao makamanda mbona makubwa!
Wacha kamba wewe Chadema ni mali ya Mtei na Mbowe.CCM Mna Mambo mnashiriki maandamano ya wananchadema. Zitto Kamwe hatakuwa zaidi ya Chadema. Ni CCM pekee ambako kuna wanachama amabo ni zaidi ya CCM. Huku Chadema Zitto ni Mwananchama kama wengine tu.
My friend, unaweza kulinganisha umaarufu wa Shibuda alipokuwa CCM na alionao sasa? Unakumbuka kwamba Shibuda alivimba kichwa hadi kufikia kutangaza kumpinga Kikwete mwaka 2010? Leo yupo wapi? Hata wa kwao huko Maswa wanamwona Msaliti. Mtu aliyejenga umaarufu mkubwa kupitia chama fulani, hawezi kuwa maarufu vilevile kwenye chama kingine. Akina Kangi Lugola hivi sasa wanaweza kuonekana ni mwiba sana kwa serikali kwa kuwa wamo ndani ya chama kinachoitetea serikali. Lakini wakiingia kwenye chama cha CHADEMA let say, wanaweza kuonekana wa kawaida sana, kwa kuwa kila mtu ndani ya CHADEMA anafanya hayohayo. Likewise, Zitto ameweza kuibuka na kuchanuka ndani ya CHADEMA, kwa kuwa sera ya CHADEMA inaruhusu wabunge kusema mambo yote bayana. Lakini siku akiingia chama kingine, ambacho kabla ya jambo kupelekwa hadharani linahitaji kupunguzwa kwanza makali na chama, hatakuwa na lolote jipya. Nawahakikishieni, Zitto akitoka nje ya CHADEMA, tutamsahau.unachokisema si cha kweli,kumbuka kuna shibuda,walifukuzwa ccm na bado alipohama chama alipata nafasi ya kuwa mbunge,wapo wengi na bado wanaendelea kuongoza ktk majimbo yao,hata kama zitto atafukuzwa uanachama,hiyo haitasababisha zitto akose nafasi ya ubunge kama atataka kugombea kwa chama kingine,yaani unapomkataa wewe,wenzako wanasema lini watampata.kwa sababu vyama vinahitaji kushika dola na si kulemba na ili kushika dola ni lazima uwe na watu potential watakaoweza kuvuta wapiga kura
Yuko na chama kipi? mbona sioni hata alama ya chama chochote bendera nk nk, na hao walinzi wake ni judoman ama ni mujahdin, janjaweed ama....
Sidhani kama kuna mtu yeyote amemzuia kwenda jimboni kwake, ila tunachojaribu kushauri ni busara ipi inayomwongoza ukikumbuka bado yeye ni mtuhumiwa anayeangaliwa kwa jicho la karibu.
picha hii inaonyesha kama anajaribu kupambana na chama chake mwenyewe kitu ambacho ni hatari kwake na wala si hatari kwa chama.
Chama? Chanini wakati yeye mwenyewe ni zaidi ya Chama?Yuko na chama kipi? mbona sioni hata alama ya chama chochote bendera nk nk, na hao walinzi wake ni judoman ama ni mujahdin, janjaweed ama....
Aende na bendera za CDM kwani haogopi kupigwa mawe kama katibu mkuu? Kwasasa vijana tunamkubali Zitto kuliko Chama na bendera zake.mbona sioni bendera za chadema
​
Pigo jingine kwa Zitto na team yake.....mkakati wao wavuja.....
Katika hali ya kutafuta jinsi ya kuweza ama kuibomoa ama kutaka kuonyesha kuwa Ana nguvu ndani ya Chadema na haswa kwenye baraza kuu , mambo yafuatayo yameandaliwa na team Zitto kwa kuratibiwa kwa ukatibu sana na watu wa idara kama ifuatavyo;
1. Ni kuwa leo Kigoma , aliyopewa jukumu la kuratibu ziara nzima ni Mwanamama Maria Sarungi, huyu bila Zitto kujua amejikuta anapandikiziwa huyu mama na Chadema makao makuu na amejikuta kuwa kwenye wakati mgumu kwani mipango wanavyofanya yote ina Julikana na mpaka sasa ni kuwa Makao makuu ya Chadema wanafuatilia kila jambo jinsi linavyokwenda. Maria alipopewa jukumu la kuandika hotuba ya Zitto , aliwasiliana na kiongozi mmoja wa makao makuu ya Chadema , na kiongozi huyo ndio aliandika draft ya kwanza na kumpa Maria ili aweze kuiwasilisha kwa Zitto, na ndio itatolewa leo huko Kigoma.
2. Maria na wenzake wameenda mbali kwa kuandaa kinachokatwa Mkakati wa Baraza kuu kwa kuwa na bajeti na kuandaa petition kwa ajili ya kusainiwa na baadhi ya wajumbe wa Baraza kuu kwa hoja kuwa ni ili kushiriki za kuitwa kwa kikao cha Baraza Kuu, waliokuwa katika utekelezaji wakajikuta kwenye wakati mgumu sana kutoka kwa wajumbe , na ndipo walipoamua kuwadanganya wajumbe kuwa fomu hizo za petition zimeandaliwa na Chadema makao makuu, na hivyo zina Baraka zote kuwa ni jambo halali. Kwa mfano leo viongozi wa kusini wameitwa Masasi na aliyepewa jukumu la kuratibu jambo hilo kwa mujibu wa Maria Sarungi ni Chitanda Ali , ila alipoona kuwa hawezi kukubalika kwa wajumbe waliamua kumpa jukumu la mialiko katibu wa Nachingwea ,na kikao cha Masasi kitafanyika leo jumamosi.
3. Zitto, kwa kutokujua amejikuta akifanya mipango yake ambayo inaratibiwa na Makao makuu ya Chadema kwa mkono wanyama , ndio maana hata mpango wa kujaribu kuwafukuza viongozi wa Chadema walioshiriki MAPOKEZI ya Dr.Slaa huko Kigoma , unaelekea kukwama baada ya Makao makuu kuingilia kati, aliyepewa jukumu hilo la kuratibu Kigoma ni Tabibu Alex , japo huwa anapenda kujita Dr.Alex , na ndio hata leo amepewa fomu za kusaini petition kwenye mkutano wa hadhara, na walivyo panga ni kuwa leo hiyo petition haijawekwa utangulizi ili wajumbe na wananchi was iweze kushtuka na ivyo ndivyo itakayokuwa.
4. Bajeti ya mpango huu ni kubwa kwani kwa awamu ya kwanza itahusisha mikoa ya Mwanza, Tabora,Lindi, Mtwara, Tanga,Katavi ambako Mzee Arfi ndio amepewa jukumu, Mwanza jukumu kapewa Wilson Mushumbusi , Chagulani Adams, Tabora jukumu kapewa kijana mmoja kutoka Kaliua huyu sio mwanachama wa Chadema hivyo jina kampuni, Tanga jukumu kapewa Khalid Rashid.......
5. Timu ya Zitto, imejikuta ikimficha Msafiri Mtemelwa mambo mengi kwani wanafikiri yeye kwa kushirikiana na Mwamnyange ndio wanavujisha siri, pasipokujua kuwa wala sio hao ni watu wa jikoni ndio ambao ni majenti wa Makao makuu,
6. Pigo kubwa zaidi ni baada ya Nchimbi uteuzi wake kufutwa na Rais jana , kwani alikuwa ameshaline up baadhi ya ama ocd kwenye wilaya kuhakikisha kuwa mikutano ya hadhara inalindwa na kupewa ulinzi mkali wa kuonyesha kuwa kuna kitu kikubwa......pigo hili limewaadhiri pia media house ya Msacky kwani mpango ulikuwa kamambe.......
mwisho, Moods, ni najua kuwa mmoja wenu ameshirikishwa kwenye mpango huu na tayari amekuwa akitoa taarifa za watu ambao wamekuwa wakiandika na hata saa nyingine kuondoa post za baadhi ya watu , naomba hii ibaki hapa na kama kuna mtu atabisha nitaweka ushahidi hapa hatua kwa hatua.
stay tuned........hotuba itakayotolewa na Zitto nitaiweka hapa baadae , nusu saa kabla ya hotuba yenyewe kutolewa.