PICHA: Yaliyojiri Karimjee katika kumuaga Regia Mtema

Nichukue fursa hii kukushukuru ndugu yetu kwa kutuwekea picha hizi, tutazidi kukushukuru kama utazidi kutuwekea za huko Ifakara, Mungu awatangulie mfike salama na kumuweka ndugu yetu kipenzi Regia na mrejee salama.Viongozi wote na jamii nzima kifo cha Regia ni funzo kubwa kwetu. Kuwa unapotenda mema hasa kwa kupigania haki na usawa unakaa mioyoni mwa watu.
 
DSC_0481.jpg


Nimeipenda sana hii, lol

Huyu jamaa wa katikati apunguze kuvaa maskafu hata sehemu zisizo stahili...
 
mkuu n00b, heshima sana mkuu. Watu wa aina yako wapo wachache sana mkuu. Tuna jitahidi kupiga [picha na vi-simu na vi-kamera vyetu, tunajitahidi kuweka picha hapa, lakini kuna watu ambao hawa-appreceate hata kidogo.

Mtu wetu eltoro amejitahidi kuweka picha hapa, lakini kuna watu humu wamekuja kuponda kwamba hazina quality......mpuuzi mmpja hivi.....mwingine kaja na advert ya blog eti watu wakaangalie picha huko........mods kama mnataka kunipiga ban, you are welcome.....lakini tabia ya kuingia jf na kubeza jitihada za watu binafsi (hawalipwi - hata max and co, hamuwalipi) ni upumbavu na u-kenge!!!!!


again, thanks n00b, thanks eltoro, thanks the finest na wengine wote.


hao watu wapotezee tulio wengi tumeridhika na wengine huwa hatutembelei huko tuko jf nyumbani tunapata kila kitu.
 
Aksante mkuu Noob.
kazi nzuri na wengine tumeshiki japo kwa picha.

Ubarikiwe!
 
Wana JF kweli mmetuwakilisha vyema, hizo tshirt nimezipenda, ni kumbukumbu nzuri, tuli huku mikoani tunapataje wakuu? I would love to have one. Pia niliuliza kuhusu kuwasilisha Rambirambi how can we do it tuliopo huku mikoani?
 
Kinachonishangaza ni ongezeko la viongozi wetu wanaopewa ulinzi kwa kodi zetu. Kulikoni?
 
Mbona kama kuna fujo hapo????????

hakuna fujo mkuu...vijana wengi walijitokeza kuupokea mwili... mwili uliwasili saa nne lakini kwa kuwa kulikuwa na watu wengi waliojitokeza kuupokea mwili ilibidi mbowe asimame awatulize vijana maana wengi walikuwa kama hawaamini hivi.....mwili uliingia ndani saa tano usiku....
 
Back
Top Bottom