Mwili wa Dkt. Kijazi wawasili Dar es Salaam, kuagwa rasmi kesho Karimjee. Kuzikwa Korogwe Jumamosi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,119
Viongozi mbalimbali wako uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiongozwa na waziri mkuu mh. Majaliwa.

Ndege iliyobeba mwili imeshawasili.

Tukio liko mubashara Channel ten na TBC

======

Mwili wa marehemu Dkt. Kijazi utapelekwa hospitali ya Lugalo kuhifadhiwa. Mwili umewasili kutokea mjini Dodoma.

1E8F7C3B-B932-4E91-A7C9-024DACC38B6E.jpeg

PICHAWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wailoshiriki katika kuupokea mwili huo wakimpa pole, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ambaye alikuwa ni mmoja wa Wanafamilia na viongozi wa serikali waliosafiri pamoja na mwili wa marehemu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

=====

Dr. Abbas: Tuendelee kumuombea katibu mkuu kiongozi ambae ametutoka jana na leo tumepokea mwili hapa Dar es Salaam baada ya jana kufariki usiku katika hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kwahiyo taratibu zinaendelea kiserikali na kama mnavyoona tulikuwa na mheshimiwa waziri mkuu.

Utaratibu unaenda kuhifadhiwa kwa muda kidogo Lugalo lakini baadae pia usiku huu utapelekwa nyumbani kwake hapa Dar es Salaam na kwa ratiba leo itakuwa imeishia hapo.

Ratiba ya maziko na mazishi kitaifa itaanza rasmi kesho, tutakuwa na shughuli uwanja wa Karimjee, Dar es Salaam. Wananchi wawahi kuanzia saa moja asubuhi ikiwezekana kwasababu tutakuwa na viongozi wengi lakini misa na shughuli nyingine zitaanza saa tatu kwenda mbele.

Baada ya shughuli ya kesho Karimjee, tutasafirisha kwenda kwao Korogwe mkoani Tanga ambap shughuli ya mazishi na maziko zitafanyika siku ya tarehe 20 ambayo ni Jumamosi.

Alikuwa kiongozi muhimu kwa nchi yetu, cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo kikubwa kwenye utumishi wa umma, ndie alikuwa katibu wa baraza la mawaziri, ndie amekuwa mwenyekiti wa kamati ya makatibu wakuu, ndie ambae kwa sehemu kubwa sana amesukuma mageuzi kwenye utumishi wa umma na naamini michangio yake itaelezwa
 
Viongozi mbalimbali wako uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiongozwa na waziri mkuu mh. Majaliwa.

Ndege iliyobeba mwili imeshawasili.

Tukio liko mubashara Channel ten na TBC
Kesho karimjee tutakuwa na mzee mwenyewe baba la baba a.k.a jiwe ataongoza mamia kwa mamia kuuga.

Swali la kizushi;
Je? Nae atavaa barakoa?
 
Viongozi mbalimbali wako uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiongozwa na waziri mkuu mh. Majaliwa.

Ndege iliyobeba mwili imeshawasili.

Tukio liko mubashara Channel ten na TBC

======

Mwili wa marehemu Dkt. Kijazi utapelekwa hospitali ya Lugalo kuhifadhiwa. Mwili umewasili kutokea mjini Dodoma.

Corona piga majizi yote ya kura mpaka yachanganyikiwe.
 
Ratiba ya maziko na mazishi kitaifa itaanza rasmi kesho, tutakuwa na shughuli uwanja wa Karimjee, Dar es Salaam. Wananchi wawahi kuanzia saa moja asubuhi ikiwezekana kwasababu tutakuwa na viongozi wengi lakini misa na shughuli nyingine zitaanza saa tatu kwenda mbele.
Hivi hao wananchi hawana TV waage wakiwa makwao ? Unajua hizi family affairs watu tumezigeuza kuwa function na kuuza sura, sijui huu utamaduni tumeutoa wapi..., Yaani anatoka Dodoma, anapelekwa uwanjani alafu tena ndio anapelekwa sijui kwao kuzikwa....

Hapo wafiwa ni kupelekeshwa na kusumbuliwa tu.... hususan nyakati hizi za changamoto ambayo hatujui vizuri ni changamoto gani....
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Back
Top Bottom